Zegota
JF-Expert Member
- Jun 5, 2020
- 274
- 584
Nakumbuka ilikuwa mwaka jana, Ndugu yangu mmoja alikuwa amemaliza kidato cha sita na alikuwa huko sitimbi.
Akanipigia simu ili nimsaidie upatikanaji wa cheti chake cha kuzaliwa ili aombe mkopo baada ya matokeo kutoka kama vigezo vilivyokuwa vimeainishwa.
Nikawazamia RITA, nikajaza fomu zao kwa majina sahihi ya ndugu yangu then nikalipia gharama zilizohitajika nikairudisha ile fomu na nikapewa muda wa kwenda kuchukua cheti.. baada ya kupata cheti, dogo akaniambia nimsaidie wakihakiki ili majina yatumwe bodi ya mkopo.
Nikauliza wale staff walionipa kile cheti lengo la kuhakiki vile vyeti vya kuzaliwa kwa wanaoenda kuendelea na masomo ya chuo, wakaniambia ni kuweza kutambua vyeti visivyo halali. Nikawapa kile cheti nikidhani watakiingiza kwenye mfumo moja kwa moja maana wamekitoa wao muda si mrefu na kunipa, wakaniambia. Mr Zegota hapa unatakiwa ulipie Tsh 3000/= ili tuhakiki hiki cheti kujua kama sio feki.
Hili jibu lilifanya nibaki nimeduwaa yaani wamenipa cheti mda huohuo halafu wananiambia kwamba natakiwa nilipie kuhakikiwa kama ni halali, Nikaona kama haileti mantiki vile. Baada ya kuendelea kuwabana na maswali kutaka kujua kiundani jamaa wakaonesha kukasirika na kupanick.
Nikaona isiwe kesi, nikalipa kwa Tigo pesa kwa malipo ya serikali nikaendelea na process zingine walizonielekeza za kuhakiki, Mpaka leo bado nashangaa ina maana RITA wana mitambo fake mle ndani ya kutengeneza vyeti vya kuzaliwa?
By the way, hii ndio Bongoland.
Leta kisa chako cha huduma uliyopata na ukabaki kushangaa kutoka kwa hizi ofisi za hapa nchini za umma au binafsi.