Ni huduma gani au ofa gani ya mitandao ya simu uliwahi kuifurahia?

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,504
646
Mimi sitakaa nikasahau enzi zile za mabundi night ya Voda ambapo sh.200 ulikuwa unagonga unlimited internet kuanzia saa nne usiku hadi asubuhi. Tulienjoy sana wajanja night. Na baadaye ilipanda hadi sh.500.

Na baada ya miaka kadhaa waliniambia niweke kiasi chochote cha fedha kwenye akaunti yangu ya M-Pesa ili nipate one week unlimited internet nikadhani masihara, nikaweka 2000, aisee nilienjoy sana.

Hizo ni baadhi tu.

Sent from my cupboard using mug
 
Nakumbuka pia kwenye miaka ya 2007 au 2008 kama sijakosea enzi hizo hakukuwa na vifurushi nilikuwa naweka vocha ya 500 natumia ikibaki sh 10 nalazimisha simu kuconnect kwenye internet ikishaanza kuchezesha ile mishale ya gprs, nalaunch Opera mini nakula mzigo unlimited internet hata week nzima sasa shida iliyokuwepo ni download speed maana ilikuwa ile ya G na Edge ila nilienjoy sana.

Ila hiyo haikuwa huduma bali ilikuwa loophole kwenye mtandao.

Sent from my cupboard using mug
 
-Airtel vocha za 200, lengo ni kukupa internet kwa saa 1 Ila kukawa na bug unapata internet unlimited siku nzima

-tigo internet lite 9000 kwa mwezi, lengo kukupa speed ndogo unlimited Ila ilikuwa ukituma neno mara mbili ina unlock full speed. Hii ilinisomesha chuo miaka 3.
 
PD Proxy na TunnelGuru, sitozisahau, naunga na voda 4G, mwendo wa 10MB/s tu mwezi mzima

nilikua nashusha akina GTA-V za 60GB , watchdog, the witcher 3 ya 50GB, Just Cause, nacheza nafuta, kesho nazishusha tena kmmmmk
Mm nlitumiwa ya tgo 2012 ilikuwa noma
 
-Airtel vocha za 200, lengo ni kukupa internet kwa saa 1 Ila kukawa na bug unapata internet unlimited siku nzima

-tigo internet lite 9000 kwa mwezi, lengo kukupa speed ndogo unlimited Ila ilikuwa ukituma neno mara mbili ina unlock full speed. Hii ilinisomesha chuo miaka 3.
Hivi chief zile social bundle za Tigo Gb16 kwa mwezi bado zipo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom