Ni hisia tu: EL atakuwa Katibu Mkuu wa CCM

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
1,045
Muda huu unaopita, jk anamalizia kutangaza Baraza la Mawaziri. Mpaka dakika hizi za nyongeza, jina la EL bado halijatokea. Na kwa kuangalia tu kwamba Wizara zinanazoendana na HARAKATI zake zimekwisha tajwa zoote. Sitarajii jina lake liitwe kwenye nafasi zilizobaki. Napata HISIA labda EL anausubiria Ukatibu Mkuu wa ccm?! Kiti ambacho awali kilionekana kumsubiri Kinana hapo 2012

Ni HISIA tu, niongozeni kwenye YAFUATAYO
 
Atarudi tena na kusema kuna wizara ameisahau, ndipo utakapolisikia jina la EL. Si uliona mwenyewe alishaisahau wizara moja?
 
Atamteua Januari Makamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM. Si ukoo wao unahusiana na Mkoa huo? Babake kawahi kuwa Mkuu pale kwa atayawza.

Juu ya January, niruhusuni niunge mada nyingine hapa.

Wana JF, kwa sababu hamkupata dondoa naamini nalotaka kuwajuza ni wachache tu waliopata kulijua au kulisikia.
January ALITUKAMIA sana JF. Alikuwa anazungumza mipango ya kulinyamazisha jukwaa hili pamoja na media zingine kama vile tayari alikuwa na MAMLAKA achilia UWAZIRI ulioishia kwenye ndoto katika AWAMU hii. Hii ilijitokeza siku moja nikiwa kiwanja ghafla akaingia MPIGANAJI toka humu JF (ANAFAHAMIKA). January naye alikuwa kiwanja kile kumwona tu akaanza KUSHUSHA VITISHO; "Mnajifanya mnaipinga serikali na hiyo JF yenu, subiri niingine madalakani. Nitahakikisha mnatoweka na vijalida kama MwanaHalisi. Nashngaa viongozi wa serikali wakiandikwa JF wanatetemeka. Mimi hamnitishi"

Ndoto ya madalaka makubwa ilimlevya hata akasahau FADHILA ya JF kumtangaza yeye pamoja na blog yake. Nani angemjua January kwa kiwango cha sasa kama JF haikuchangia kwa kiasi kikubwa?! Tabia za vijana tuliofikiri wanaaminika kumbe wanabadilika kimsimamo baada ya kupanda migongo yetu na kutwaa madalaka inazidi kuongezeka.
 
Muda huu unaopita, jk anamalizia kutangaza Baraza la Mawaziri. Mpaka dakika hizi za nyongeza, jina la EL bado halijatokea. Na kwa kuangalia tu kwamba Wizara zinanazoendana na HARAKATI zake zimekwisha tajwa zoote. Sitarajii jina lake liitwe kwenye nafasi zilizobaki. Napata HISIA labda EL anausubiria Ukatibu Mkuu wa ccm?! Kiti ambacho awali kilionekana kumsubiri Kinana hapo 2012

Ni HISIA tu, niongozeni kwenye YAFUATAYO

Mkuu umeniwahi sana, EL kujiweka sawa na 2015 lazima awe na position ya kum influence, na post pekee nionavyo mimi iliyobaki ni ya Katibu mkuu CCM.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom