Ni heri Tanzania ingeendelea kutawaliwa na Mkoloni ili tupembuke akili

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe nanyi.

Wakati Joe Biden akiwa ameshinda kiti cha Urais wa Marekani akiwa na miaka 78 Makamu wake mtarajiwa Bi Kamala Harris alitoa hotuba nzuri iliyosisimua watu wengi sana.

Kamala akiwa binti aliyezaliwa na wazazi wote wahamiaji waliotoka nje ya Marekani yaani Baba mwenye asili ya Jamaica na mama mwenye asili ya India alitoa hotuba kali sana huku akisifia Uzuri wa Marekani kuwa ukiwa na ndoto yeyote ile Marekani unaweza kuitimiza haijalishi unatoka familia gani, au wewe ni nani au umetoka kwenye background gani au ni mtu wa namna gani. Hii kwa Wamarekani wanaita American dream.

Hili limejidhihilisha kuanzia kwa Joe Biden hadi kwa Kamala Harris.

Kwa Joe Biden amekuja kushinda Urais wa Marekani akiwa na miaka 78, huku akiwa alishajaribu mara mbili huko nyuma kuwa Rais na kushindwa.

Kwa Kamala amekuwa Makamu wa Rais huku akiwa ni mtoto wa wahamiaji.

Ila kwa Tanzania leo hii Magufuli akiwa anahutubia baada ya kuwaapisha Majaliwa, Kabudi na Mpango amesema kitu ambacho kwa watu wenye akili ni jambo ambalo linahuzunisha na kuumiza sana.

Amesema watu walio na umri mkubwa kumzidi hawawezi kuwa Marais na hata kama wana hizo ndoto basi wazifute. Alienda mbele na kuwataja Lukuvi na Kabudi

Hii inamaanisha nini?

Hii inamaanisha kwa Tanzania chini ya Magufuli na CCM mtu hata akiwa na ndoto yake ya kuwa mtu fulani au kufanikisha jambo fulani basi hiyo ndoto yake hawezi kuifanikisha hadi ipate ridhaa ya watu fulani wenye uwezo wa kuamua hatma yake.

Hii ina maanisha pia kwa Watanzania ndoto zetu tulizonazo juu ya maisha yetu wala haziamuliwi na Mungu bali mtu mkuu anayechukua madaraka.

Kwa hali ni Bora Tanzania tungeendelea kutawaliwa na Wazungu mpaka tupate akili na kustaarabika ndio wangetuachia tujitawale.

Na kwa hali hii ndio maana hatutakuja kupata maendeleo ya kweli ya kwetu hadi pale tutakapojua na kukubaliana kuwa CCM ndio mchawi wa ustawi wa Tanzania.
 
Wakoloni walichimba madini lakini walikumbuka kurudisha pesa katika kuendeleza jamii. Walijenga shule, hospitali, barabara, waliweka maji na umeme.

Ajira zilikuwepo kwani walifanya kilimo cha biashara na kuajiri vijana wengi tu.

Tusingepata uhuru 1961, 3/4 ya nchi ingekua na barabara za lami.
 
Mtu ambae ameshaonesha mara nyingi hafuati sheria, yeye hujiamulia mambo yake kutegemeana na vile alivyoamka.

Huko CCM vijana wanajua wanawekwa na wazee, ndio maana kila siku kuomba misamaha hata kama hawajui makosa yao.

Wameamua kuishi kwa kujipendekeza, wanafanya matendo ya ajabu kwa watanzania wenzao (wapinzani) ili watimize hizo ndoto zao, akina Heri James.

Kweli tulikuwa na kiherehere cha kumfukuza mkoloni, atleast akili za mkoloni mweupe zingetusogeza mbele zaidi kimaendeleo.
 
Wakoloni walichimba madini lakini walikumbuka kurudisha pesa katika kuendeleza jamii. Walijenga shule, hospitali, barabara, waliweka maji na umeme.

Ajira zilikuwepo kwani walifanya kilimo cha biashara na kuajiri vijana wengi tu.

Tusingepata uhuru 1961, 3/4 ya nchi ingekua na barabara za laki.
Watu weusi hatukupaswa kuwai kujitawala. Kuna shida sana kwenye akili ya mtu mweusi.
 
Tanzania kupata uhuru 1961 ilikuwa sawa na binti wa miaka 14 kutaka kujitegemea na kutoka nyumbani kwa wazazi wake wa hiari.

Makuzi yanakuwa shida; kudumaa ki mwili na akili vinamsonga.

Kinachofanyika sasa ni kuua kabisa fikra za vijana hasa hawa wa CCM ili wabaki kushabikia tu yote yanayofanywa na wazee wao hata kama ni ya kulinajisi Taifa.
 
Hata Kamara Haris atapata mpaka watu flani aka wajumbe waridhie, so ni kawaida kwa Trump, kwa Biden , Obama wote walipata ridhaa ya wajumbe! Mbona vijana wengi tu wametimiza ndoto wakati wa JPM!
Unamaanisha nini? Ni watu gani hadi waridhie ndo Kamara apate? Unaposema Obama hadi watu fulani waridhie unamaanisha nini??! Hivi lumumba huwa mna akili kweli?
 
Hivi wewe leo ndo unajua? Maisha ya mtz yanamliwa na kikundi au watu fulani, hata wakisema kesho unatakiwa kufa na utakufa bila kubisha mwenyewe 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tanzania kupata uhuru 1961 ilikuwa sawa na binti wa miaka 14 kutaka kujitegemea na kutoka nyumbani kwa wazazi wake wa hiari.

Makuzi yanakuwa shida; kudumaa ki mwili na akili vinamsonga.

Kinachofanyika sasa ni kuua kabisa fikra za vijana hasa hawa wa CCM ili wabaki kushabikia tu yote yanayofanywa na wazee wao hata kama ni ya kulinajisi Taifa.
Alafu mbaya zaidi mtu kaongea statement kwa kujipa mamlaka ya Mungu badala wasikitike wenyewe wanacheka cheka tu!
 
Hivi ww leo ndo unajua ? Maisha ya mtz yanamliwa na kikundi au watu fulani, hata wakisema kesho unatakiwa kufa na utakufa bila kubisha mwenyewe 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Yani mzee Lukuvi kaambiwa hawezi kuwa Rais na binadamu mwenzake na kabudi, badala wasikitike yenyewe inajichekesha tu!! Yaani hii nchi inabidi irudi kwa wakoloni watu wafunguke akili
 
Unafikiri tunapenda kustaafu miaka 60 wakati tuna nguvu?

Tuna malengo mengi kama hao wazee wagombea urais

Sema tu vyakula vya kibongo bongo upevu na ufanis wa kazi huwaga mzuri pindi unapokuwa kijana kwenye nguvu..
 
Mkuu kwa hili nakubaliana nawe.
Hata ukiangalia South Africa aliyepata uhuru jana tu wako vizuri.

Tukubali tukatae tumefanya haraka ya kupata uhuru..
Kweli kabisa. Waangalie Zimbabwe, walifukuza wazungu wakawanyang’anya mashamba. Wameshindwa kuyaendeleza na Zimbabwe ikafa kwa uzalishaji chakula. Sasaivi wanawarudishia wazungu mashamba yao
 
Mkoloni huyohuyo ALITOA ELIMU kwa watoto wa VIBARAKA WAKE na WATOTO WA MACHIFU aliokuwa "anashirikiana" nao kujinufaisha KIUCHUMI.....

Ni wapi mkoloni alitoa elimu njema na bora kwa WANANCHI WOTE wa lililokuwa KOLONI LAKE?!!!

Ni wapi mkoloni alijenga HOSPITALI BORA kwa wananchi WOTE?!!!

Nakukumbusha ya kwamba JIJINI DAR ES SALAAM hakukuwa na HOSPITALI kwa ajili ya WAZAWA Mpaka pale "mhindi" mmoja mwenye UTU alipoguswa na kuamua kutoa eneo kukajengwa KITUO CHA AFYA pale POSTA STESHENI ambako at least WAZAWA waliweza kupata PANADOL na DAWA YA VIDONDA GV....

Halafu baadaye sana ndio akatokea muhindi mwingine Mzalendo KUTUJENGEA pale SEWA HAJI(Leo muhimbili).

Hebu jiulize ni kwanini watoto wa MACHIFU Pekee ndio waliopata elimu kubwa:
1.Hayati Mwalimu NYERERE
2.Hayati Abdallah Fundikira
3.Hayati Hamza Mwapachu
4.Hayati Adam Sapi Mkwawa
5.Ukoo Wa kina Mirambo
6.Ukoo wa Marealle
7.Ukoo wa Sina na Meli
👆👆👆
Halafu zitazame familia hizo,je si familia za viwango vya JUU Mpaka LEO?!!!
 
Tanzania kupata uhuru 1961 ilikuwa sawa na binti wa miaka 14 kutaka kujitegemea na kutoka nyumbani kwa wazazi wake wa hiari...
Kwani kuondoka kwa WAKOLONI hiyo 61 kulitarajiwa na WAZAWA?

Kwa hiyo kwa nchi zilizobaki chini ya ukoloni mpaka leo(SYCHELLES) ama zilizochelewa sana kupata UHURU ziko Katika UBORA waupendao zaidi yetu?

MSUMBIJI?!!!

ANGOLA?!!!

Unadhani wakoloni WANGECHELEWA kutoka na kutuachia NCHI YETU haraka ndio tungekuwa na AMANI UTULIVU NA MAENDELEO BORA zaidi ya SASA?!!!!
 
Back
Top Bottom