Ni heri kuwa masikini unayejari utu, kuliko tajiri mwenye kudharau utu

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,398
319
Katika maisha ya mwanadamu kuna mambo makuu matatu (3) unayopaswa kuwa nayo na muhimu mno

1. kujari utu

2. unyenyekevu + utii

3. Busara

haya ni mambo mwenye nayo, huwa tajiri kuliko kuwa na mali, na pesa
kwa sababu kuwa na mali nyingi mara nyingi huleta kiburi na jeuri,
hivyo ni heri kuwa mtu wa kawaida kuliko kuwa tajiri usiyejari utu wa mtu na kukosana Mnyaazi M'ngu. Mambo haya matatu, mtaji ni wake ghali mno maana ni lazima ukubari dharau, ujinga, kujifanya hujui ili kila wakati upate elimu ambayo ni msaada wako na mtaji wa amani yako na uhuru na kujipunguzia maadui na kuwa rafiki wa Mungu na wanadamu pia.
Lakini huwa tuko tayari kuutafuta utajiri kwanza, ili kujilimbikizia jeuri na kiburi, kuijenga dharau kwa watu ambao wataonekana kuwa hawana mbele zako, na kwa sababu ya kutaka kuwa tajiri ili kujionesha kwa wayu ndiyo maana basi mtu yuko tayari hata kuua mwanadamu mwenziye il amiliki pesa, hapo tayari amejianda mfuko mkubwa wa jeuri kwa maana ukawajari watu wasiyo nacho kwa sababu ya njia ambazo ulitumia kujipatia pesa.....MUNGU SAIDIA MIMI NIWE MKOSA UTAJIRI NISIJE NIKAKUKOSEA
 
Back
Top Bottom