Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Kuna kanuni zilizowekwa kwa mjibu wa sheria ya uchaguzi wa namna ambavyo wagombea wanatakiwa kuzifuata wanapofanya kampeni kushawishi kura za wananchi. Kabla ya kuteuliwa na NEC wagombea hawa waliapa mbele ya mahakimu au majaji kuwa watazingatia kanuni na maadili hayo yaliyowekwa kwa mjibu wa sheria.
Kuna mgombea fulani ambaye ni wazi kabisa katika kampeni zake hazingatii kabisa hizo kanuni, taratibu na maadili aliyoapa kufuata. Lugha na maneno anayotumia dhidi ya mgombea mwenzake hayakubaliki hayakubaliki hata kidogo na ni kinyume na maadili yaliyowekwa na sheria hiyo. Ni maneno makali yenye kuuzi, kufedhehesha na kumudhalilisha (defarmatory) mgombea mwenzake.
Anatumia lugha ya kibabe yenye kuchochea uvunjifu wa amani. Amekuwa akirudia rudia kuwa ana watu wengi nyuma yake (wafuasi wake) na kwamba wasijaribu kumugusa maana moto watakaouwasha hakuna atakaye weza kuuzima. Bahati nzuri wale wa upande mwingine wamejitahidi sana kuwa wavumilivu na wastaarabu.
Sasa ni nani mwenye mamlaka ya kutiepusha tusifike pabaya? Jee Tume yetu ya uchaguzi inayo mamlaka ya kumchukulia hatua zipi za kisheria mtu kama huyu? Je, ina mamlaka ya kumpa onyo kali, karipio au kufuta uteuzi wake wa kuwa mgombea kabla hajawasha huo moto anaousema?