Ni hatua gani za kufuata ili nipokee mzigo (gift parcels) kutoka nje ya nchi?

Mercenary Army

JF-Expert Member
Jun 2, 2017
269
603
Naona wadau wengi wanaenda nje ya mada kunitahadharisha juu ya utapeli wa wanaijeria, nashukuru sana kwa maonyo yao ila ningependa mnisaidie/ wanisaidie juu ya nilichouliza tu hayo mengine waniachie mimi.
 
Mkuu upo hatarini kutapeliwa. Angalia usije ukaambiwa utume pesa ndiyo utumiwe. Mkuu kaa jonjo. Kwa mimi ninavyo fahamu kama ni vitu vya kawaida akuna garama za ziada za kulipia isopo kuwepo karama za utumaji tuu ndyo zitakazo lipwa.

Pia wewe unaweza ukamwambia akutumie uje ulipe hapa hapa nchini ukiwa unavopokea. Kwa maelezo zaidi subir wadau wanakuja
 
Mkuu upo hatarini kutapeliwa. Angalia usije ukaambiwa utume pesa ndiyo utumiwe. Mkuu kaa jonjo. Kwa mimi ninavyo fahamu kama ni vitu vya kawaida akuna garama za ziada za kulipia isopo kuwepo karama za utumaji tuu ndyo zitakazo lipwa. Pia wewe unaweza ukamwambia akutumie uje ulipe hapa hapa nchini ukiwa unavopokea. Kwa maelezo zaidi subir wadau wanakuja
Mkuu mtumaji wa mizigo hiyo kila kitu analipia yeye hivyo kaniomba nimwambie tu ni njia gani anaweza kutuma vitu hivyo kwa urahisi nikavipata,hivyo suala la kunitapeli ati nitume hela niko nalo makini sana
 
Unaenda kutapeliwa believe me. Hao ni wa Nigeria wapumbavu sana walinifata f akaniambia nimtafute kwenye e-mail tumechat kwa mda kidogo then akaniambia amenipenda na mengine kama hayo (alinitumia picha ya mtoto wa kike mzuri kweli) Mimi namchora tu hajui kama Mimi ndio tapeli mkuu, tumechat nae then akaniambia ananitumia vitu vya thamani kama tv, friji, iPhone na mengineyo akasema anaendugu yake ni sister (nun) kwahiyo nimtafute nijue nitavipataje.

baada ya kumtafuta huyo sister akaniambia anazo zawadi zangu cha kufanya akaniambia nimtumie pesa ili avitume akanielekeza jinsi ya kumtumia hiyo pesa ..nikamwambia hakuna hela ya kupumbavu kama hiyo kama vipi anitumie then vikifika nitamrudishia hela yake, hakupatikana tena wala hakujibu e-mail.

Ndugu sumu aionjwi ila kama ni ndugu yako au mtu unamfahamu kutoka senegal zipo njia mbalimbali za kutuma...kama hajakuomba hela yoyote pia wako wajuvi watakuelekeza.
 
Mkuu kuwa makini, uko njiani kupigwa hela!...utaambiwa mzigo umetumwa afu utakwama njiani,picha ndio litaanzia hapo!
 
Unaenda kutapeliwa believe me. Hao ni wa Nigeria wapumbavu sana walinifata f akaniambia nimtafute kwenye e-mail tumechat kwa mda kidogo then akaniambia amenipenda na mengine kama hayo (alinitumia picha ya mtoto wa kike mzuri kweli) Mimi namchora tu hajui kama Mimi ndio tapeli mkuu...
Mkuu mimi huyu ni ndugu yangu kabisa ndio maana sina wasiwasi nae na nishakubaliana nae alipie kila kitu
 
HELA SITUMI MKUU
Mbona unaleta mambo ya chandimu hapa? Mtumiwa mzigo unaulizia taratibu za nini wakati mtumaji ndiye anatakiwa aulize huko aliko? Na kama mtu ameshapata akili ya kusafiri kwenda nje ya nchi basi hawezi kukosa akili za kutumua mzigo?

Mbona hili liko straight foward kabisa. Ukitaka kutuma mzigo nenda posta ya nchi uliyopo, kama hujui taratibu ulizia watakuelekeza. Pia kuna makampuni mengi yanashughulikia na utumaji wa mzigo eg DHL, UPS, FedEx etc.

Huyo ndugu yako ni mshamba kiasi gani mpaka akuulize wewe na wewe uje ufungue thread? Hata uki-search kwa kutumia Google ''how to send percels to Tanzania unapata mawakala wengi? Angalia sana usije kuwa umeingia kwenye 18 za matapeli maana wengi ndiyo huchota watu akili na kuwafanya mazuzu kabisa.
 
Shukran sana mkuu kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom