Ni hatari sana ,usifanye hivi gari yako itawaka moto

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,167
Wakuu kumekuwa na mtimdo sasa hivi wa kupimp gari na kufunga taaa taa nyingi sana za urembo kwenye gari..ikiwa pamoja na kutoa taa kubwa original za kuja na gari na kufunga zingine ili gari iwe na mwanga mkali zaidi..wengine hufunga taa za boostar ni hatari sana usifanye hivyo kwenye gari zenu wengi wao zinaishia kuwaka moto..

Naongea hivi nikiwa na ushahidi wakushuhudia kuona na nazungumza kwa ushahidi au vigezo vya kitaalam.
Sina nia ya kuharibu bishara ya wanao fanya shughuli hizo hapana lkn hapa tunaambiana ukweli na kutaadharishana..
Hatari ipo hapa ..wengi wana funga taa za booster unakuta mtu gari yake ilikuwa na taa kubwa high 60W na beam 55W.

Anakwenda kubadilisha taa na kufunga bulb za mchina zenye 900W beam na 1000W high.
Waya ule ule uliokuwa unapitisha umeme kwenda kwenye bulb ya 55W leo hii unapitisha current kwenda kwenye bulb ya 900W unategemea nn hapo?? Kama sio gari kuwaka moto??..

Wengine wanatoa bulb za kawaida na kufunga bulb za booster ukifika kwenye taa ambayo imefungwa bulb ya booster ikiwa imewaka shika au sogea karibu na kioo cha taa huwa kinakuwa cha moto sana..sasa kuna utofauti wa quality ya kioo cha taa ya kawaida na ya booster..na taa ya booster inaproduce joto kali sana ambalo kutokana na taa yenyewe haikuwa mahususi kwa bulb hiyo huishia kuungua na kuunguza gari.

Janga jingine ni ukaaji wa hizo bulb za modification kwenye majumba ya taa kwa kuwa sio original yake so mafundi huwa wanaforce na kinachotokea nikuunguza jumba la taa na mwishowe gari nzima..

Kuna ishu pia ya bulb na booster za kichina nyingi ni low quality kabisaa na low price.huwa vicontrol vya booster vinaungua sababu waya zinazotumika huwa zinakuwa ni zile za low quality kabisaa ukilinganisha na mzigo zinaobeba..
Kama kuna wataalam au wenye uelewa kidogo tuu na umeme wananielewa vizuri zaidi.

POWER. P
VOLTAGE. V
CURRENT. I
RESISTOR. R

Hasa hapo kunakitu kinaitwa factor afecting resistor..

Mfano:

Umefunga bulb ya 900w lkn waya ambao unapitisha umeme mwanzo ulikuwa unapitisha umeme wa kwenda kuwasha /tumika kwenye bulb ya 55W.

Ili bulb ya 900W iweze kuwaka inahitaji current nyingi sana zipite kinachotokea wakati current zinaforce kupita kwenye waya ndio hapo waya unapata moto na kuungua na kuunguza gari..

Nimekutana na kesi nyingi sana za namna hiyo.ndio maana nikaona sio mbaya nikashare hapo..
 
Hii thread mzuri kama hii ilikuwa wapi? tokea December 13 inakuja kuonekana leo?

Asante sana kwa ushauri maana nilikuwa na mpango wa kufunga hizo taa kwenye carina ti
 
Upo sahihi kabisa mkuu na elimu wasipewe wamiliki tu wa vyombo vya moto ata mafundi wanatakiwa kujua hilo kwa usalama wa kazi zao
 
NIMEFUNGA TAA ZA BUSTA KWENYE BAMPA LAMPS ZA GRANDE GX-110 NA ZINAFANYA KAZI KAMA KAWA (SIPINGANI NA ANDIKO LAKO LAKINI)
Tatizo lipo kwa mafundi wetu hawa wa uswahilini kila kitu wanafanya kwa magumashi ilimradi wapate cha juu kama wire basi watakufungia fake ndio maana zikipata moto zinasababisha shoti
 
Mkuu ukibadilisha waya inayopeleka current kwenye bulb hapo Si inakuwa naamanisha waya upitishe moto sawa na Watt zinazoenda kuwasha
 
hata mimi nimefanya mabadiliko, ila nilikua makini sana kwenye upande wa technical specifications bila kusahau kuhakiki taa mpya haigusi lile jumba ikafanya liungue.

ushauri mzuri sanaa.
 
Mkuu kwema? Gari yangu inasumbua sana, ina miss nimesha badirisha plug na pump za mafuta lakini hola, nimeambia n tatizo la power supply kwenye umeme, naomba msaada wako
 
Mkuu kwema? Gari yangu inasumbua sana, ina miss nimesha badirisha plug na pump za mafuta lakini hola, nimeambia n tatizo la power supply kwenye umeme, naomba msaada wako
Jaribu kuangalia distributor ya gari yako.
wakati mwingine ile contact pointer inayozunguka kugusa wire zinazopeleka umeme kwenye plugs inaungua hivyo haigusi ipasavyo na kupelekea kutopeleka moto wa kutosha kwenye plugs.Hapo utabadilisha plugs zote,pump na ntatizo liko pale pale.
 
W = V×A
Nb;
W = watts ( load capacity eg, light)
V = Volts (source of power eg 12V from battery)
A = Ampere (fuse capacity to pass the current in the wire eg, 10A, 20A in the fuse box)
While, wire should have specific gauge (ga) to pass the current within eg, 6ga or 4ga.

Ukija ktk kesi ya mleta mada kwa mafundi wote bila ya kuliathili hill gari ktk saketi husika kinachotakiwa ni kujua hizo hesab za kubalance saketi isiungue

Mfano;
Watts = 1,000w
Volts = 12V
Ampere to use huijui course umeshabadili watts hapo juu kutoka ktk taa ya awali.

So, you doing this to find Ampere.
From, W = V×A
1,000 = 12 × A
1,000÷12 = A
Amperage = 83.3A
So, tafuta fuse ya uwezo huo au iliyo na makadilio hayo
Then ingia ktk Google ktk dawat la technical issue za masuala ya umeme Wa DC watakwambia, kutokana na Ampere rate hiyo utumie wire gauge size ipi.
Ukishafanikiwa basi hyo saketi yako itakua sehem salama bila ya short.

Mafundi weng wa mitaan hawalijui hili wao wanajua kufunga tu.
 
konki....
 
Mafundi wengi vilaza wa mtaani!ukiona anapoteza muda kuingia google ujue basi hapo anaangalia porn
 
Back
Top Bottom