Ni Hatari Sana "Mnyonge" Anapochoka "Kunyongwa"

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
250
Ndugu wa JF,

Msemo wa Kiswahili, MNYONGE MNYONGENI ILA HAKI YAKE MPENI, ni dhahiri na kweli. Kwanza nianze kwa kutoa msimamo wangu binafsi kuhusu kuuwawa kwa Ndugu Mabina; ni kweli raia walikasirishwa na matendo ya Mabina; lakini hata hivyo si haki kwa raia kujichukulia sheria mikononi. Hali hii ikiendelea kwa kweli Nchi haita tawalika. Naomba tuache ushabiki wa kiasiasa katika hili jambo; ni lazima vitendo hivi vikemewe katika jamii.

Kwa upande mwingine; nitoe lawama kwa mfumo wa haki (Mahakama) na vyombo vingine na usalama. Ni hatari pale ambapo raia wataamini kwamba hawawezi pata haki yao katika vyombo hivi. NI HATARI SANA MNYONGE ANAPOCHOKA KUNYONGWA!! Tusipokuwa makini tutajikuta tunaibomoa nchi yetu kwa sababu ya wachache wasiotaka kutenda haki kwa jamii.

Rai yangu kwa walio madarakani na nafasi za maamuzi ni kwamba tukumbuke msimamo wa Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere; "CHEO NI DHAMANA; SITATUMIA CHEO CHANGU KWA MANUFAA YANGU BINAFSI AU KUGANDAMIZA WANYONGE."

Asanteni.
 
Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
673
195
Ukiua kwa upanga nawe utauawa upanga

Ndugu yangu lemikaoforo watu waache kupotosha wale wananchi hawakuchukua sheria mkononi bali walikuwa wakijilinda wao na mali zao dhidi ya mtu aliyejichukulia sheria Mkononi.Hila jambo linapotoshwa sana aliyechukua sheria mkononi ni Mabina walichofanya wanachi ni kutekeleza haki yao ya kisheria na kikatiba ya kujillinda wao na mali zao tena wametumia reasonable force katika ku retaliate (mawe na fimbo) kwani kama ni uwingi wa watu hata huyo marehemu alikuwa na kundi la mabaunsa.

Hata huo ukamataji unaofanywa na Polisi ukishindwa kuliangalia hili ,utakuwa ni muendelezo wa udhaifu wa jeshi hili ambalo sikuhizi linatumia mitulinga zaidi kuliko akili na ueledi.
 
piper

JF-Expert Member
Jan 17, 2012
3,253
1,195
Yaani kiukweli kuna hatari kubwa inatunyemelea hali hii ikiachwa iendelee.
 
Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,206
2,000
Ndugu yangu lemikaoforo watu waache kupotosha wale wananchi hawakuchukua sheria mkononi bali walikuwa wakijilinda wao na mali zao dhidi ya mtu aliyejichukulia sheria Mkononi.Hila jambo linapotoshwa sana aliyechukua sheria mkononi ni Mabina walichofanya wanachi ni kutekeleza haki yao ya kisheria na kikatiba ya kujillinda wao na mali zao tena wametumia reasonable force katika ku retaliate (mawe na fimbo) kwani kama ni uwingi wa watu hata huyo marehemu alikuwa na kundi la mabaunsa.

Hata huo ukamataji unaofanywa na Polisi ukishindwa kuliangalia hili ,utakuwa ni muendelezo wa udhaifu wa jeshi hili ambalo sikuhizi linatumia mitulinga zaidi kuliko akili na ueledi.

!
!
hahahahahahahaha we ni nouma hahahahahaha mambo ya binaadamu hayo
 
Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
May 16, 2013
1,337
0
Ndugu wa JF,

Msemo wa Kiswahili, MNYONGE MNYONGENI ILA HAKI YAKE MPENI, ni dhahiri na kweli. Kwanza nianze kwa kutoa msimamo wangu binafsi kuhusu kuuwawa kwa Ndugu Mabina; ni kweli raia walikasirishwa na matendo ya Mabina; lakini hata hivyo si haki kwa raia kujichukulia sheria mikononi. Hali hii ikiendelea kwa kweli Nchi haita tawalika. Naomba tuache ushabiki wa kiasiasa katika hili jambo; ni lazima vitendo hivi vikemewe katika jamii.

Kwa upande mwingine; nitoe lawama kwa mfumo wa haki (Mahakama) na vyombo vingine na usalama. Ni hatari pale ambapo raia wataamini kwamba hawawezi pata haki yao katika vyombo hivi. NI HATARI SANA MNYONGE ANAPOCHOKA KUNYONGWA!! Tusipokuwa makini tutajikuta tunaibomoa nchi yetu kwa sababu ya wachache wasiotaka kutenda haki kwa jamii.

Rai yangu kwa walio madarakani na nafasi za maamuzi ni kwamba tukumbuke msimamo wa Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere; "CHEO NI DHAMANA; SITATUMIA CHEO CHANGU KWA MANUFAA YANGU BINAFSI AU KUGANDAMIZA WANYONGE."

Asanteni.

Nani amkemee nani. Umesikia suala la Kapuya? Wamefikia wapi? Mbona yule mtoto aliyefanyiziwa na Prof Kapuya anateseka mbele ya macho ya Umma, Kwa mujibu wa nukuu za gazeti la Tanzania Daima Kapuya anadai hawatamfanyia lolote maana nchi ni yao hii, watoto wao wanauza unga hakuna anaye wagusa, ndugu yangu hata kama kusoma hujui hata picha huoni? Uliyasikia ya Ditopile Mzuzuri wakati anamuua yule dereveva wa daladala? Huyasikii ya Meno ya Tembo na madawa ya Kulenya?Kama wenye dola na chama tawala ndo wenye kuchukua maamuzi hayo, unategemea nini? Wanyonge kokote Duniani wanategemea nguvu ya Umma. Nani amwamshe nani katika hili?
 
Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,870
2,000
Walichokifanya raia wa eneo hilo Mwanza wako sahihi kabisa,hakukuwa na njia mbadala unless tungekuwa chini ya uongozi wenye kusimamia haki za kibinadamu. Tz mwenye pesa na cheo ndiyo wenye haki tu.
 
Ndugu yangu, nakubaliana na wewe kwamba kwa namna moja au nyingine wapo viongozi wengi wanaotumia vibaya nafasi zao kupindisha au kunyima haki kwa wanyonge. Lakini kama tusipokemea hili la kuua watu kinyama nchi inaweza elekea pabaya sana. Tutoe changamoto kwa serikali na viongozi kutumia ofisi na madaraka kwa manufaa ya umma. Hii ya kuua watu haina tija kwa mstakabali wa Taifa.
 
Inasikitisha, lakini ukweli unabaki palepale, tunahitaji utawala wa sheria ndugu Ndikwega. Mob Justice itatufikisha pabaya.
 
Jiwejeusi

JF-Expert Member
May 3, 2011
753

unachosema ni sawa japo kilishasemwa sana lakini serikali na vyombo vyake haikuchukua hatua, kwa kuwa wanaominya haki za raia wamo serikalini. sasa baada ya juhudi zote hizo unawataka raia wafanye nini? wadhulumiwe bila ya kuchukua hatua?
 
Jiwejeusi; unayosema ni kweli, lakini Je, unaamini kwa wananchi kuwashugulikia viongozi kwa staili ya alivyofanyiwa Mabina Jijini Mwanza itasaidia? Huoni kwamba hii inaweza pelekea vurugu na watu wengine kuonewa??
 
Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,870
2,000
Inasikitisha, lakini ukweli unabaki palepale, tunahitaji utawala wa sheria ndugu Ndikwega. Mob Justice itatufikisha pabaya.

MKUU UTAWALA WA SHERIA UKO WAPI KWA TZ? Wanyonge tunaonewa,tunadhurumiwa ukipeleka kesi Mahakani huko ndiyo unakuwa umejitakia maumivu sana maana rushwa ndiyo kiongozi wao huko, hivyo hawachelewi hata kukufunga mwenyewe au kukupiga fine. Hii nchi tunakoelekea ndiyo huko, nguvu ya umma ndiyo utakuwa msaada wetu. Haki ikikosekana kinachofuata ni machafuko ndugu yangu. Ukweli ndiyo huo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom