Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,124
- 39,265
- Kwa siku kadhaa sasa Rais Magufuli amekuwa akitoa kauli za kuishauri na kuishinikiza mifuko ya Hifadhi ya jamii(Pension Fund) kuanza kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda na kuacha kabisa uwekezaji wa ujenzi wa majengo makubwa.
- Kwanza kabisa, ni kosa kubwa sana kwa wanasiasa(Viongozi wa kiserikali) kuingilia mifumo ya uendeshaji wa mifuko hiyo hususani eneo la uwekezaji. Ni hatari sana. Kwa sababu siku zote wanasiasa wanawaza mambo kwa jicho la kisiasa(kufurahisha wananchi), na uwekezaji wa mitaji ya kifedha ni suala la kibiashara(Kuzalisha Faida).
Upande wa pili, uwekezaji wa viwanda vikubwa, unatoa Faida kubwa, unaleta faida haraka haraka sana lakini una hatari kubwa sana kuzaa Hasara kubwa. Ni uwekezaji usioweza kutabirika kibiashara.
Mpaka sasa hapa Tanzania uwekezaji wa viwanda unaosimamiwa na mamlaka ya umma au serikali haujawahi kufanikiwa kabisa. Viwanda na makampuni karibu yote yaliyowahi kuanzishwa na serikali(Umma) yaliishia Kufilisika, Kufa, kuuzwa kwa hasara nk.
Hata machache yaliyopo sasa(ATCL, TRL, TTCL, TAZARA, TANESCO nk) yote yanaendeshwa na serikali kwa hasara kubwa sana.
Kujenga Kiwanda ni jambo moja(Tena kiuwekezaji ni jambo rahisi sana) ila kuendesha kiwanda ni jambo lingine kabisa(Kiuwekezaji ni jambo gumu sana).
Jambo moja lililowazi kabisa ni kwamba, Tanzania bado sana kufikia uchumi wa viwanda, kuna mambo mengi sana yanahitaji kufanyiwa marekebisho katika mifumo yetu ili kuhimili uwepo wa uchumi wa viwanda. Mengi yanayosemwa sasa kuhusu ujenzi wa viwanda ni nadharia fupi fupi sana, tena zinasemwa na wanasiasa, huwezi kuzikisia kamwe zikisemwa na wafanyabiashara wakubwa hapa Tanzania.
Katika hili naomba sana mifuko ya hifadhi ya jamii isikurupuke kabisa, wachumi elekezi wapewe nafasi ya kushauri na kuonya wazi wazi ili kuepusha pesa za dhamana za wafanyakazi zilizowekwa kwenye mifuko hiyo zikaangamia.