Ni hatari Kutangaza dawa za kulevya zinazotengenezwa kienyeji

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,579
Ni kweli dawa za kulevya hutengenezwa na kemikali ambazo kwa matumizi mengine ni salama kwa binadamu ila kwa Upande wa pili zinaweza kutumika kama dawa za kulevya hivyo SI salama.

Kuna dawa ambazo ni salam kwa matumizi ya binadamu na hupatikana kirahisi hospitalini au Pharmacy mitaani ila ukichanganya na dawa nyingine au kemikali nyingine zinakua ni dawa za kulevya, habari kama hizo tukiziandika ni hatari. Kuendelea kutangaza kua watu fulani wanatumia dawa flani kama dawa ya kulevya ni Sawa kuuza formula ya kutengeneza BOMU kwa jamii kitu ambacho kinaipa kampeni ya kupambana na dawa za kulevya kuwa =0

Ni vyema tukazuia hizo habari zisiwafikie vijana maana ndo waathirika zaidi maana hizo dawa au kemikali tunaishi nazo mitaani miaka nenda rudi ila hazikujulikana kama zinaweza kutumika kama dawa za kuevya..
 
Ni hatari sana maana dawa nyingi zinalevya ni vile tuu watu hawajui
 
Back
Top Bottom