Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Nakumbuka mwaka 2017 baada ya kumaliza chuo baba yang mdogo aliniunganisha mgodini nkawa napga kazi mshahara ulkuw mdogo kama Laki tatu lakin nilijibana sana ndani ya mwaka nilifikisha M 2.6 ili nifungue duka la dawa sikukaa sawa hata lengo langu halijatimiia mkataba ukasitishwa.
Tulikaa na bamdogo tukashauriana cha kufanya nikaona niende kwanza home huku nkfikiria cha kufanya, eee bwana eee sinikapanda gar mpak home. Ukwel mm nimelelewa na bibi na babu alafu familia mob kinoma huwez amin M 2.1 iliteketea kwa matumiz ya nyumbani na visa vya wazee mara babu atishie kukupa laana kisa hutoi hela na anasema mm ninapesa ila sitoi home na wakat natoa na matumizi nanunua kila mara na pia wakati huo wakati nafanya kazi nilikuwa nawatumia kila mwezi before mkataba haujaisha.
Sikukata tamaa baada ya hayo kutokea nkasema nkampgia sim mamdogo wangu akanitumia kama laki 3.5 nkafungua biashara ya kuuza chipsi, kiukweli niliipenda kazi yangu naondoka asubuh narud usiku, nakumbuka babu yangu ananiambia maneno ya ajabu kuhusu hyo biashara duh! Eeee bwana ee haikuchukua round ilikufa nkawa sina hata 100 nkabak mweupeee.
Nashukuru baada ya miez kadhaa nkaajiliwa serikalini lakin kila mipango ninayo ipanga shetan anaingilia kati saiv ninaandika haya nipo home nilipatwa na ajar ya pikipiki hvyo ndio najipanga kurud kazin ni miez miwili nipo home

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikulacho....!!
 
Ngoja namim nijarib kupunguza machungu yangu hapa kwenye jamvi, mwaka 2014 nipo chuo mwaka wa 2 nilikuwa napiga harakat zangu nikafanikiwa kuweka akiba sh 1.2M nikaenda kununua pikpik used ikaanza kazi baad ya miez 6 nikaongeza zikawa 2 ila nilihama eneo nilikuwa naishi na kwnda sehem nyingne nikakutana na rafik yangu wa utoton alikuw amemalza shule ila hakufanikiwa kufaulu akaniomba nimsaidie km naweza kumpa kazi, nikaona nimpe kazi ya kusimamia zile pik pik sabab m nipo busy na chuo akatafta madereva mwnyw m nikawa namlipa, alileta hesab ndani ya mwez mmoja tu akakata mawasliano miez 6 kuja kumfatlia anasema pik pik zimekufa nikamwomba nizione, nakuta ameziacha kwa fundi pik pik zipo hoi haztamaniki moja iligeuzwa ya kutoa spea za fundi, tukagombana sanaaaa bila mafanikio nikachukua pikpik zangu.

Nikatengeneza moja ambayo ilikuwa na afadhal ilinicost almost 200k kukaa sawa nikatafta dreva wa hesab akaja ndug yang anakaa makongo akaleta rafik ake n dereva hana pikpik ya kuendesha nikampa kaenda nayo akawa anatuma hela baad ya mwez napgiwa simu na dreva anasema pikpik imekamatwa ipo kituon UBUNGO kwa makosa ya wizi baada ya kufatlia sana ikashindkana kuitoa maana dereva alikuw anabadlisha plate number ili kufanya uhalifu.... iliniuma sana sitosahau.
Dah noma sana. Tunaangushwa na tunaowanyanyua.
 
Aisee
Aliniambia Tutafute kijiji Kilichokuwa mbali na maeneo ya mjini Ili tupige kazi Sisi tulikuwa wawili na yeye jumla wa tatu. Basi jamaa alikuwa na kimashine chake cha kuchakata hizo pesa Kule kijjin tulikaa siku mbili.Baadae akasema wino na mafuta ya taa vimeisha akaomba aende mjini akavichukue. Yule jamaa hakurudi tena alituacha pale masaa mengi adi asubuh nikampigia simu lakin hakupatikana nikajua nishapigwa kuangalia kwenye lile begi tuliloweka pesa kuna makaratasi tu yamepakwa malangi ya blue mpaka leo hii Sijampata na kile kimashine chake alikiacha tukalipot polisi yule jamaa hajapatikana.

Sent from my SM-A013G using Ja
Aisee! Mkuu huyo jamaa mlikua mnamjua vizuri?
 
Mwaka 2019 tu hapo nilishawishiwa na rafiki yangu ninunue hiace moja ilikuwa kazini kwao inauzwa, kumbe ile gari ni kimeo mbaya mbovu, engine haieleweki kabisa, ni zile hiace za NISSAN zenye tabia kama X-Trail ikianza kuharibika....jamaa nilikuwa namuamini sana so sikuwa na haja ya kukagua kivile, alinitumia picha tu nikaridhika nikijua ni marekebisho madogo madogo ya rangi e.t.c! Kitu ambacho sikujua ni kwamba jamaa yangu huyo alikuwa anapata commission kwa kuuza hiyo gari....dah nikazama CRDB nikapewa mkopo nikachukua gari langu nikiwa na matumaini itaingia road irudishe pesa!!! Mpaka navyoandika sasa hivi nimeamua kui-park tu, garage kila siku....mkopo bado natoboka kwenye mshahara wangu na gari haijarudisha hata robo ya pesa
 
Mkopo
Mkopo
Mkopo

Nimetaja kwa kukariri mara tatu... Nina hasara iendeleayo ila yote hiyo kwajili ya mkopo tu. Eti mimi ni wa kushindwa kutatua hata tatizo la elfu10 nyumbani kwetu!!!? Kisa eti nina mkopo unaosababisha nakatwa hela nyingi sana (kama siyo yote)

Kukitokea dharura ya kuhitaji pesa ya fasta eti mimi ni wa kushindwa kukopa hela kwingine maana1ya3 imeshagota kweli!!!? Kwahiyo mpaka nikope washkaji ambao wao wamekidhi vigezo vya kwenda kukopa

Kuna watu huwa hawaamini lakini watu tunapitia magumu sana hatuwezi kuyaandika wala kuyaanika. Halafu eti ndio kwanza nna mwaka wa pili (naingia wa tatu)kazini!

Hatahivyo, muda mwingine narudisha mkanda wa kumbukumbu nyuma basi sijilaumu sana kwani wengine tumeanza kazi tukiwa sisi kama sisi (hakuna mtu wa kutushauri maswala ya kikazi wala nini) kwahiyo maswala mengi (mengine) tunayajulia humuhumu kwwenye kazi

Nawashauri wenye uelewa juu ya mikopo kwa watumishi basi wawe wanawaasa na kuwasihi ndugu jamaa na marafiki zao namna ya kuyaingia haya mambo
 
Nyie ndo huwa mnakuwa na hasira sana kazini...kwasababu mmekopa mshahara Wote
 
Hahaha dah pole sana pia vumilia makato yakiisha usikurupuke tena.
 
Aliniambia Tutafute kijiji Kilichokuwa mbali na maeneo ya mjini Ili tupige kazi Sisi tulikuwa wawili na yeye jumla wa tatu. Basi jamaa alikuwa na kimashine chake cha kuchakata hizo pesa Kule kijjin tulikaa siku mbili.Baadae akasema wino na mafuta ya taa vimeisha akaomba aende mjini akavichukue. Yule jamaa hakurudi tena alituacha pale masaa mengi adi asubuh nikampigia simu lakin hakupatikana nikajua nishapigwa kuangalia kwenye lile begi tuliloweka pesa kuna makaratasi tu yamepakwa malangi ya blue mpaka leo hii Sijampata na kile kimashine chake alikiacha tukalipot polisi yule jamaa hajapatikana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Sasa polisi mlisemaje, maana hata nyie mlikuwa wahalifu kwa jamhuri
 
Mwaka 2019 tu hapo nilishawishiwa na rafiki yangu ninunue hiace moja ilikuwa kazini kwao inauzwa, kumbe ile gari ni kimeo mbaya mbovu, engine haieleweki kabisa, ni zile hiace za NISSAN zenye tabia kama X-Trail ikianza kuharibika....jamaa nilikuwa namuamini sana so sikuwa na haja ya kukagua kivile, alinitumia picha tu nikaridhika nikijua ni marekebisho madogo madogo ya rangi e.t.c! Kitu ambacho sikujua ni kwamba jamaa yangu huyo alikuwa anapata commission kwa kuuza hiyo gari....dah nikazama CRDB nikapewa mkopo nikachukua gari langu nikiwa na matumaini itaingia road irudishe pesa!!! Mpaka navyoandika sasa hivi nimeamua kui-park tu, garage kila siku....mkopo bado natoboka kwenye mshahara wangu na gari haijarudisha hata robo ya pesa
Ishu kama hii ndo imenipotezea mimi pesa zangu zooote. Ila anyway nitapata tu nyngine nyingi zaidi.
 
Huu uzi unatoa mafundisho mengi mazuri sana katika utafutaji.
Ninatamani MODS waupe heshima inayostahili ukae kama STICK THREAD kwenye jukwaa mojawapo kwa manufaa ya wengine sasa na baadae.
Ni mtizamo wangu tu lakini.
Nakazia hapa
 
Asante kwa kuchangia mada. Sijui sana kumhusu Dadii labda ungeniambia kwa undani kidogo ni kwa nini umemtaja Dadii. Lakini kwa lolote analopitia ajue mambo yanabadilika mtu ukiapambana lakini la zaidi ni KUJIFUNZA KUPITIA MAKOSA. Naona mfano kuna watu wanawapatia hela ndugu wasimamie kilimo kama ndg aliyelima ekari 30 za pamba. Kisa chake na changu vinafanana sababu wote tumelizwa na ndugu. Pia kuna wengine walioajiri watu kwenye miradi kama mmoja alipoteza million 8.7 nk. Watu ni kujifunza katika biashara. Unapoanza, usiangalie faida kwanza. Mimi tours mwaka wa pili ndio faida ilianza kuingia.

Pia mtu inabidi ujifunze kitu ili watu wasikuibie. Kama ni pamba, basi jua hicho kilimo kinafwanywaje hata angalao basic knowledge kwanza. Basic knowledge ni kujua mambo fulani muhimu sana kwanza. Kama inahudumiwaje, inapandwajwe. Unafanyaje kuhakiki ukipanda zinaota. Pia fanya testing kwanza hata ya nusu ekari kwanza. HASA KAMA MTU UNAWEKEZA HELA NYINGI HIVYO.

Bahati nzuri kwangu bado niliweza kupata pesa nyingine nzuri tu baada ya kupoteza hio 45 million. Ilichukua muda sana kuweza kuanza miradi tz, ila niliweza.

Pia Tanzania kama hauwezi kusimamia kitu mwenyewe, basi TAFUTA WATU WAAMINIFU TU ndio wakisimamie.

Kwa hio kwa swala la ajira kwa Dadii, atambue kufanya kazi kwa watu kama mimi lazima uwe mwaminifu sana. Na ninatoa mitihani fulani ninayoijua mwenyewe kwa wafanyakazi wote. Pia nafuatilia historia yake alikokuwa. Pia NAWALIPA VIZURI HELA YA KUTOSHA MAHITAJI YAO. Ili isiwe kisingizio cha kuiba.

Wanatambua uaminifu kwangu ni one ot top requirements. Watu wasanii tz wapo wengi zaidi sababu kuna watu wanaamini bila wizi hawatoboi. Ila pia waaminifu wapo. Ukiwatafuta, unawapata.
Safi mkuu
 
Jamaa Fulani. Walioana na mamaa kwa bashasha na nderemo, zawadi kubwa kubwa! Zawadi ya baba Mkwe: Aisee wanangu hamna haja ya kutafuta kiwanja. Mimi natoa sawadi yangu aisee ekari mbili na nusu !"
Mc: "Makofi kwa Baba mkweee!!" Pra, pra, pra.
Jamaa akajenga bonge nyumba. Ilipoisha tu, kila siku mamaa vituko. Siku moja akamlamba makofi ya uso!
Mama akazimia, akalazwa wiki moja (fake), alipotoka tu ni kudai talaka. Kugawana Mali, pasupasu. Mamaa akawahi nyumba. Baba mkwe: Aisee babangu nisikuone hapa aisee, yaaani unataka niulia mwanangu aisee! Tena kimbia haraka sana! We kadogoo ebu lete ile panga juu ya kabati, fanya harakaa!!
 
Back
Top Bottom