Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Mimi nadhani nimeshakuwa sugu,nimepoteza mno kiasi kwamba imeshakuwa naona ni kawaida,siumii wala sishtuki ila wanaonizunguja wanaumia Hadi nawaonea huruma,,,mwezi wa tano pekee nimepoteza Mali ya zaidi ya million Saba,mwaka Jana sio chini ya million 70,komesha ni 2016...Duka la zaidi ya million 120 lilitafunwa na dogo niliyemuokota na kumfanya mdog o wangu,niliingizwa mjini na mtu was karibu million 70,nilipata hasara ya mifugo kufa zaidi ya 56m, nilibaki na madeni ambayo Hadi leo yananinyima Raha,2000 nilitapeliwa na mtu wa karibu 8m...mikasa ni mingi mno,ila namshukuru Mungu bado napigana,leo hii Niko naanza upya naamini sijachelewa bado....
Una umri gani mkuu ..ili nikupe namba ya kufanya usipoteze tena.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Nilipoteza 1.5M nikiwa na miaka 20 niliingiza pesa hiyo kwenye biashara ambayo sikuifanyia utafiti wowote wala kuomba ushauri kwa mtu yoyote kwakua nilishawishiwa na mtu nilie muamin Sana lakin sikirudisha hata senti 1 ya pesa ile baada ya kuitoa
.. naamin lile lilikua funzo tosha kwenye maisha yangu, ni story ambayo sikuwahi kumsimulia mtu yoyote kwakua niliamin kutokumsimulia mtu yoyote ndo njia rahisi ya kulisahau lile tukio.
Hahaha ka 1.5M tu hahaha mbona hizo ni chenchi tu mzee

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Dahh ..umenihuzunisha San ila pia mm nimepta hasra jaman mwak 2018 nilipoteza ajira yangu ktk kampuninya sola bas nilikuwa nasave sana ktk mshahra wangu hvyo nilishi kwa perdiem tu bila kugusa msharaha mm nilikuwa cpend mademu wa ghla bas niliweza kusave Kama milioni 14 hv pmj na kulipwa malilimbikozo na pesa za kurudishwa nyumbn bas .bas bhna nikaenda kununua bajaja mpy uwez amuni ile mabajaj ajamaliza ata mwaka nikauza milion nne na nusu ..mkp sas cjajenga Wala nn nimetulia tu na maisha yamekuwa magumu mno na Kaz cna Wala kuoa Bado Ni hasara Sana
Ulinunua bajaji mbovu nini ..mbona watu wanaingiza faida kupitia bajaji hadi 50k per day..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Aisee, huu wizi uliingia sana... tena jamaa waliokuwa wanafanya hizi mambo... walikuwa wanajifanya wakongo...
Watu wengi sana wameharibiwa maisha yao kutokana na huu utapelii... maana jamaa wakikuingia hawakupigi padogoo... yan ukija kupikicha macho hivi... 50M ishakatikaaa.
Yaani ilibaki kidogo tu nijiue ila ndio changamoto za biashara. Mimi nilikuwa naagiza simu Nyingi sana Yaani Itachukua muda ku recover sahizi biashara hakuna kabisa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu, lkn najiuliza hapa unawezaje kumwamini mtu ukampatia 19M eti akutengenezee zingine? Au kuna ushirikina hua unatumika vp?
Aliniambia Tutafute kijiji Kilichokuwa mbali na maeneo ya mjini Ili tupige kazi Sisi tulikuwa wawili na yeye jumla wa tatu. Basi jamaa alikuwa na kimashine chake cha kuchakata hizo pesa Kule kijjini tulikaa siku mbili. Baadae akasema wino na mafuta ya taa vimeisha akaomba aende mjini akavichukue. Yule jamaa hakurudi tena alituacha pale masaa mengi adi asubuh nikampigia simu lakin hakupatikana nikajua nishapigwa kuangalia kwenye lile begi tuliloweka pesa kuna makaratasi tu yamepakwa malangi ya blue mpaka leo hii Sijampata na kile kimashine chake alikiacha tukalipot polisi yule jamaa hajapatikana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kupata Mwanaume MVuta bangi..Hii ndo hasara kubwa niliyowai ipata...YAAANI KUNA watu ukikutana nao maishani UMEKWISHA...hapa nilipo Leo Ni matokeo ya yule kuwa na yule mtu....

Hasara ilioji
Huyo mvuta bangi amekufikisha vipi hapo ulipo?..alifanya nini?
 
Jambo linalokuhusu wewe hasa la kimafanikio usijaribu kumwambia mtu akufanyie bila usimamizi wa wewe mwenyewe
Pole sana mkuu!

Kisa chako sehemu ya pili kinakaribiana kufanana na cha kwangu.

Mimi nililima mpunga hivyo hivyo sehemu 2 tofauti, sehemu ya kwanza nilikuwa namtumia rafiki yangu hela aweke vibarua lakini mwisho wa siku sikuvuna hata kilo moja. Sehemu hii nililima hekari 4 na ilinigharimu kama 1M. Niliamua kumpotezea tu ila hadi leo hatuna mawasiliano naye.

Sehemu ya pili niliyolima walikuwa wanasimamia dada yangu na shemeji yangu. Huku nililima hekari 20 na ilinigharimu kama 4.6M kuanzia kukodi eneo hadi kipindi cha kuvuna. Na nilipokuwa natuma hela ya kulimia pia nilikuwa nawapa na hela ya matumizi yao nikiassume kuwa wasihangaike. Kumbe kwanza eneo walilokodi zilikuwa ni ekari 15 tu na hela ya kulimia niliyowapa hawakuweka vibarua wa kulima badala yake walikuwa wanabangaiza kutafuta watu wanaalika wanalima kama sehemu ya shamba la familia lao hivyo hela ya kulimia wakala na walilima kwa kuchelewa sana japokuwa hela niliituma kwa wakati. Kwenye kuhupalilia tena walipalilia sehemu ndogo tu sehemu nyingine hawakupalilia wakala hela na pia dawa ya kupulizia hawakununua walikula pesa. Ila cha ajabu ni kwamba walikuwa wananitumainisha sana kuwa mazao yako vizuri na nitatajirika mwaka huo nitakapokuja kuvuna but nilichoambulia sikuamini aisee.

Kutokana na kuwa busy na majukumu sikuweza kufika kipindi chote cha kulima. Sasa ilipofika kwenye kuvuna ikabidi nimwambie mdogo wangu aende maana ilikuwa ni likizo alikuwepo home. Alichoenda kukutana nacho aliishia kusema bro hapa umepigwa hakuna shamba la thamani ya pesa uliyoitumia.
Nikamwambia avune tu kiasi kilichopo na auze angalau apate tu hata nauli na hela ya kumhudumia mwenyewe akiwa anarudi shule. Alivuna akauza na kupata kiasi cha 700000.

Ila kuanzia hapo nimeshasema kuhusu shemeji na dada tutasaidiana kwa mambo mengine lakini sio kifedha tena hata wakiwa na shida kiasi gani otherwise labda iwe kwenye kuokoa uhai tu ndio tutasaidiana kifedha itakapolazimu vinginevyo walishajilipa tayari kwa kile walichokula.

Kwa hiyo nikawa nimepata hasara mbili kwa rafiki yangu na kwa sister.
 
kinachonipa ugumu kwenda ni lile lifestyle la kule na lile barid a ule mkoa. just imagne makaz n zle nyumba zlizojengwa miaka ya 60 na yaan kanyumba kama pagale......lakn kubwa zaid kule mzunguko wa pesa n mdogo mana kuna jamaa kasema ndoo ya parachichi unapata kwa 1500 saasa kweli ukienda eneo kama hlo kuna kutoka kimaisha kweli au ndo naenda kudidimia zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
ndio ya parachichi buku jero

Huko unaenda kudedi



Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Aliniambia Tutafute kijiji Kilichokuwa mbali na maeneo ya mjini Ili tupige kazi Sisi tulikuwa wawili na yeye jumla wa tatu. Basi jamaa alikuwa na kimashine chake cha kuchakata hizo pesa Kule kijjin tulikaa siku mbili.Baadae akasema wino na mafuta ya taa vimeisha akaomba aende mjini akavichukue. Yule jamaa hakurudi tena alituacha pale masaa mengi adi asubuh nikampigia simu lakin hakupatikana nikajua nishapigwa kuangalia kwenye lile begi tuliloweka pesa kuna makaratasi tu yamepakwa malangi ya blue mpaka leo hii Sijampata na kile kimashine chake alikiacha tukalipot polisi yule jamaa hajapatikana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Ila wee jamaa mbona ulipigwaa kifalaa hivii yani...

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Ni wazi Katika harakati za maisha kuna pingamizi nyingi sana, kuna muda unapambana sana kutafuta kile unachokihitaji, unabahatika unakipata lakini kinapotea na kubakiza kama ambaye hajafanya chochote,

Yaweza iwe kwa kuibiwa, kutapeliwa, kudhulumiwa, kupoteza, kuharibika n.k n.k

Kwa kweli huwa inauma sana, tena sanaaa,
Sizungumzii kitu kikubwa, hapana nazungumzia kitu chochote ambacho ulikipambania kukipata lakini kikatoweka haraka/kirahisi.

Binafsi Wakati nipo chuo mwaka wa kwanza nilikua nahifadhi pesa yangu kwa kujibana sana, zaidi ya nusu ya hela yangu ya Boom(nilikua napata 100%) nilikua naitunza inisaidie nikishamaliza au popote nitakapo pata nafasi ya kuianzishia biashara,

Hela yangu yote ya kujikimu, field, special faculty na za vikazi kazi kipindi cha likizo nikawa nimefikisha 2.6M mpaka namaliza,

Wazo kubwa nililokuwa nalo baada ya kumaliza ni kufungua stationary Morogoro, kulikuwa na uhaba sana wa stationary, nikaona hii ni fursa na bahati nzuri nikapata eneo zuri kabisaa.

Basi ile nimehitimu tuu sikutaka kukaa kabisa nyumbani, nilienda tuu kuwasalimia wazee nikawaomba kuondoka baada ya week moja nikatafute maisha,

Kiukweli hawakukubali mwanzo, waliomba hata wakae na mimi kidogo maana kiukweli sijawahi kukaa nao kwa muda mrefu tangu nianze darasa la kwanza, ila baadae wakalazimika sababu ya kuwashawishi, sikuwaambia chochote kuhusu ile pesa na mpango mzima.

Nikiwa nimeandika mahitaji yangu yote, nikaenda mjini kwenye duka flani hivi pale mtaa wa uhuru, nikanunua kila kitu kihusianacho na stationary(niliuza simu yangu nikajazia na kwingne ile hela ikafika 3.0M) na baadhi ya accessories za simu nikafungasha mzigo wangu ile jioni nikaupeleka Kwenye haya malori ya Mizigo yanayoleta mizigo Dar na kurudi mikoani Usiku, mimi nikarudi zangu home.

Lengo mzigo usafiri ule usiku, kuna rafiki yangu aupokee asubuhi mimi niukute huko mchana, ile ndio ikawa kwa heri 3.0M yangu.

Kiufupi mpaka leo hii sijajua ule mzigo ulipotelea wapi, Dereva na konda wanadai waliufikisha kwa mpokeaji na akapokea, Mpokeaji(rafiki yangu) nikimuuliza anadai amesubiri ila hakupata mzigo.

Mpaka dakika za mwisho naongea na konda anasema mpokeaji huyu hapa ongea naye, nikaongea na Mshkaji kweli akasema anashushiwa mzigo, Baadae nampigia sasa yeye kwa simu yake akasema hajapokea mzigo wala hajaongea na mimi kupitia simu ile...

Hiyo ilikua asubuhi niko pale Ubungo na mimi ndio nataka nitoke,

Sitosahau ile siku....nilikaachini bila kujijuaa,
Maumivu yale sitokuja kuyasahau, nilikaa pale chini kama nusu saa hivi,

Mdada mmoja msafiri aliona ile hali yangu ndio akaja kunisaidia,

Yule dada Alichelewesha safari yake kwa kunisaidia kunivusha barabara na kuhakikisha mpaka napanda daladala akaniomba namba, akamwambia konda huyu anashukia sehemu flani ni mgeni hapajui, ndio akaondoka, sidhani kama ile siku ningepita salama pale mataa,

Network ilipotea kabisa, kufika kituoni ndio konda akanishtua "shuka dogo ndio hapa" pasipo kujua nimekulia hapo ila pamegeuka pageni kwangu, narudi nyumbani wanashangaa, kila wanachouliza nipo kimya, sio kama sitaki kujibu ila hata kinywa hakifunguki, macho yanaonesha kbsa nazuia machozi, walielewa ile hali, wakaniambia nenda kalale,

Nilianza kwa kuwaomba sana msamaha wazee, nikawaelezea kisa changu, nikawaonesha risiti za manunuzi na za kusafirishia mzigo, waliumia sana Mwishowe wakanipa support...

Hasara zipo nyingi, lakini je ni ipi ilikuumiza zaidi na kuona kama imekurudisha sana nyuma na ni ngumu kurudi kwenye Hali ya kawaida.

Sio lazima iwe pesa,
Yaweza kua ulipoteza mda kwa kitu flani, Nguvu, Matuaini/Mtarajio makubwa yakabuma n.k n.k
SHARE
...Kuna Makosa makubwa mawili ninayoona ulifanya hapa:

1. Kuwaamini watu na mtaji wako wa kwanza kabisa maishani upelekwe na kufikishwa unapotaka na watu baki wakati Wewe unarudi nyumbani kulala kwa Amani kabisa. Kosa Kubwa.
Huu ilikuwa ni mtaji wako wa kwanza kabisa ambayo ulitakiwa kwenda nao sambamba ili kujua hali inavyokuwa kuhusu.

2. Ulipaniki kwa maongezi ya simu tu wakati MTU anaweza kukuambia chochote kwenye simu ili akutoe tu njiani!

Ulipaswa baada ya kusikia tu maelezo ya Dereva kisha rafiki yako mpokea mzigo, upande gari kama ulivyokuwa umepanga ili ukayajulie huko huko ana kwa ana na waliohusika na mzigo!

Hulaumiwi sana hata hivyo. Ilikuwa ndio unaanza. Ninaamini kuwa kwa Uzoefu huu mambo yaliendelea vyema baadaye ukiwa umeishajifunza! Pole.
 
Mimi nilijibana hela ya boom nilipomaliza chuo nikawa na vihela bahati nzuri nilivyomaliza tu nikapata sehemu ya kujitolea nalipwa kidogo,basi bwana nikaanza tubiashara cha nguo za ndani za wadada nilianza na mtaji wa elfu 70 sikutaka kuwekeza hela zaidi mtaji hadi ukafika laki 3.

Mara paap sister angu alikopa mkopo bank akashindwa kurudisha kwa wakati nyumba yake ikataka kuuzwa na bank ikabidi tukae kikao kama familia tumuokoe ndugu yetu nikatoa pesa yoote baasi na biashara ikaishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
...Vipi, biashara ya nguo za ndani ya amina mama ni Mzuri? Ilikuendea vyema? Kuna dogo wangu mmoja amemaliza form four anazagaa zagaa tu hapa nyumbani anataka kujaribu.....
 
Back
Top Bottom