Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Hii ni shida ya Afrika. Business partners wanakuangusha. Kuna mifano mingi sana hapa nimeisoma na ni partner amemuangusha partner au ndugu.

Wazungu wao kwa asilimia kubwa hawana ujinga huo. Makampuni yote makubwa duniani ilikuwa ni partnership. Bill gates na paul allen (microsoft), steve jobs na wozniacki (Apple), Mark zuckerberg na Saverin (Facebook), Larry Page na Sergey (Google), Jeff Bezos na wazazi wake (Amazon). Tanzania unakuta hata baba na mtoto wanaibiana kwa partnership hadi mambo yanaharibika. Ndugu ndio usiseme kama mimi niliyopitia. Na hii ni sababu kubww ya watu ku-feli sababu tunarudishana nyuma. Very sad. Na umoja ndio unaunda makampuni makubwa kama hayo niliyoyataja hapo. Manake Africa tutaendelea kuwa na kampuni ndogo na hata ikiwa kubwa, bado haijafilia potential ambayo ingefikia na umoja wa partnership.
Partinership kwetu ni mtihani mkubwa .

Ngoja ninyamaze tuu asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tupe mbinu huwa unafankiwaje kuinuka tena from zero. Assume ulikuwa na 20m ukaingia kwny bussness flan ikapotea hela yoote na kumbka kaz iliyokupa hyo hela ushaachana nayo miaka mitatu nyuma. yaan unaingia kwny vibarua au unafanyaje fanyaje kupata shilingi mia yako ya kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Analyse pita hapa tafadhali umtag jamaa kwenye uzi wako atapata kitu.
 
Asante kwa kuchangia mada. Sijui sana kumhusu Dadii labda ungeniambia kwa undani kidogo ni kwa nini umemtaja Dadii. Lakini kwa lolote analopitia ajue mambo yanabadilika mtu ukiapambana lakini la zaidi ni KUJIFUNZA KUPITIA MAKOSA. Naona mfano kuna watu wanawapatia hela ndugu wasimamie kilimo kama ndg aliyelima ekari 30 za pamba. Kisa chake na changu vinafanana sababu wote tumelizwa na ndugu. Pia kuna wengine walioajiri watu kwenye miradi kama mmoja alipoteza million 8.7 nk. Watu ni kujifunza katika biashara. Unapoanza, usiangalie faida kwanza. Mimi tours mwaka wa pili ndio faida ilianza kuingia.

Pia mtu inabidi ujifunze kitu ili watu wasikuibie. Kama ni pamba, basi jua hicho kilimo kinafwanywaje hata angalao basic knowledge kwanza. Basic knowledge ni kujua mambo fulani muhimu sana kwanza. Kama inahudumiwaje, inapandwajwe. Unafanyaje kuhakiki ukipanda zinaota. Pia fanya testing kwanza hata ya nusu ekari kwanza. HASA KAMA MTU UNAWEKEZA HELA NYINGI HIVYO.

Bahati nzuri kwangu bado niliweza kupata pesa nyingine nzuri tu baada ya kupoteza hio 45 million. Ilichukua muda sana kuweza kuanza miradi tz, ila niliweza.

Pia Tanzania kama hauwezi kusimamia kitu mwenyewe, basi TAFUTA WATU WAAMINIFU TU ndio wakisimamie.

Kwa hio kwa swala la ajira kwa Dadii, atambue kufanya kazi kwa watu kama mimi lazima uwe mwaminifu sana. Na ninatoa mitihani fulani ninayoijua mwenyewe kwa wafanyakazi wote. Pia nafuatilia historia yake alikokuwa. Pia NAWALIPA VIZURI HELA YA KUTOSHA MAHITAJI YAO. Ili isiwe kisingizio cha kuiba.

Wanatambua uaminifu wangu ni one ot top requirements. Watu wasanii tz wapo wengi zaidi sababu kuna watu wanaamini bila wizi hawatoboi. Ila pia waaminifu wapo. Ukiwatafuta, unawapata.
@dadii mtafute huyu mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mkuu. Sema ulizingua mwanzo kinoma dah!!!
PLOT1:

Kipindi nipo Mlimani mwaka wa pili nilifanikiwa kuweka akiba ya 1M kwa ajili ya biashara nikirudi likizo mkoani.Ilipofika kipindi cha field niliweza kuanzisha biashara ya play station ambayo nilikua na experience nayo kiasi maana kipindi nasoma nimecheza sana na nimewahi fanya kipindi nipo A level huko huko shuleni.Kweli niliweza pata frem mkaoni kwa bei rafiki na vifaa nilichukua toka Dsm k.v ps2 na flat inch 32.Pesa nyingine ilitumika kwenye miundombinu ikiwemo kodi na umeme.Baishara ilianza vizuri kwa mwezi nilikua sikosi 150k.Hadi nafika 3rd year nilikua napokea per day ya 5k uhakika.Kuna kipindi dogo niliye muweka alizingua basi ofisi ikafa na vifaa vyote niliuza.Nilipokua chuo niliwaza sana ile pesa niliyokua napata kila siku (5k).Maisha yalinipiga haswaa yani kwa waliopitia Mlimani wanaelewa na nilikua nimepanga mtaani toka 1st year.Mwaka wa 3 nilichelewa kupata boom(cause of results)na nikaja pata quarter zote 3 kwa pamoja na kufika 1.7M na yote nikaipeleka tena kwenye biashara ile ile iliyokua inaniweka mjini,yani nikaanza upya na nikapanua zaidi yani tv zikawa 2 na mashine 2.nikawa sikosi 10k per day nikaona life nimelipatia.Kipindi hicho nakaribia kumaliza chuo.Balaa likaja kuna mdogo angu alianza chuo ada yake ya chuo ilikua inalipwa kwa muhula.Basi mzee akawa anaiwekea kwenye akaunti yangu na kufika 1.5M ili nikalipe chuoni kwa mdogo wangu.Ile pesa nilikua nainyofoa mdogo mdogo kwa kuamini nitaifidia kwenye biashara yangu muda ukikaribia.Ikiwa imebaki wiki moja dogo apige pepa,pesa ya ada inahitajika mtu mzima sina hata senti na hela ya biashara nilikua nakula.Nilidata nusu niugue kichaa na biashara iliyumba kwa sababu ya electricity cut-off kule mkoani nikawa napata hadi buku kwa siku.Basi ikanilazimu kuuza tena vifaa vyangu vyote around 1.5M ili nilipe ada ya dogo apige pepa na ukizingatia miezi miwili mbele naingia mtaani rasmi.Nilifanikiwa kulipa ada na mimi nikaanza kupambana na khali yangu nikamaliza chuo nikiwa sina mbele wala nyuma yani hata mia mbovu sina uwezo wa kuipata.Nikawa nimetulia geto sina mbele wala nyuma,hata pesa ya kula nilikua nategemea kwa maza anitumie buku 2 tatu akikosa napiga pasi ndefu.Bahati nzuri kuna ndugu ake maza mmoja yupo kwenye system na yupo stable mfukoni ananielewa sana toka nasoma O level,so ikabidi niwe karibu naye.Nikamcheki akaniuliza unajishughulisha na nini nikasema kwa sasa nipo tu ila niliwahi fanya biashara fulani ikaanguka.Basi mze akanipa ahadi atanisapoti mambo mawili,ajira na hiyo biashara ila ataanza na biashara atanipa mtaji wa 2M.Zilipita kama wiki 3 nikapewa hilo salio na sikufanya ajizi yote nikaitumbukiza kwenye biashara ya play station.Nashukuru Mungu huu mwezi wa 3 toka nianze upya nimeingiza around 1.2M..Naendelea kupambana na nimeweka malengo mengi zaidi katika kujiajiri kuliko kuajiriwa.Tusikate tamaa katika kupambana na maisha hata kama ukiangua usichoke siku yako ipo utafanikiwa tu.

Mkuu naomba msaada kwenye hii biashara,nikitaka kufungua minimum capital ni kiasi gani? Location inatakiwa iweje kwa experience yako mkuu?
 
Hello Dadii,
Kuna mambo nimependa sana nilivyosoma posts zako.
Kwanza umesema kukata tamaa ni dhambi. Uko sahihi kabisa. Chukulia tu kila changamoto kama somo. Lakini la muhimu zaidi tafakari sana na jiulize hapa nimejifunza hiki na hiki, na sitarudia tena kosa. Mimi mafundi siwalipi hadi wamalize kazi. WAKITAKA ADVANCE NAWAULIZA YA NINI? Kama ni material, nanunua au watu wangu wa katibu wananunua zinaenda site. FUNDI HELA ANALIPWA KWA ALIYOFANYIA KAZI.

Pili nimependa uliposema tufanye kazi kwa uaminifu. Nimekuona wewe ni mwaminifu. Endelea hivyo hivyo. Malipo ya uaminifu ni mafanikio ya kudumu. Na waliopata utajiri kwa wizi ndio kama Mbunge Suleiman Nchambi sasa anahaha kortini.

Tatu nimependa nimeona ulivyofaulu vizuri masomo ya science. Nimeona kweli wewe ni mtu mwenye akili ya kujifunza mambo vizuri.

Tanzania najua biashara kwa wengi inawasumbua sababu mtaji wanapata mara moja na ukiisha ndio basi. Mimi nilibarikiwa kuwa na hela kwa muda mrefu kwa hio hata mambo yakikataa, bado hela ipo ya kuendelea kupambana hadi mambo yanakubali.

Pia Tanzania gharama za elimu ziko juu. Wazazi wengi wanajua ili mtoto afanye vizuri inabidi ende private na English medium. Na huo ni ukweli halisi. Shule nyingi za primary za public zina deficits nyingi. Ila gharama ziko juu kwa private na ndio mtu anapambana lakini ndio hapo naona madeni na kuuza vitu nk.

Kwa sasa sijui nitakupatia ushauri gani. Labda nikuulize kwamba una skills (ujuzi) gani?

Mkuu ningependa ushauri zaidi hapo kwenye ku deal na mafundi haswa ukiwa mbali. Mimi niko Scandinavia na kwa kweli naogopa hata kutuma hela ya kununulia kiwanja achilia mbali kujenga kwa sababu nishasikia hizi habari za ndugu/ marafiki kutokuwa waaminifu. Hili limenipa wakati mgum maana nakuwa nabaki na hela mkononi tu na likizo zenyewe ni siku 25 kwa mwaka kiasi ambacho huwezi kwenda bongo na kufanya la maaana
 
Investment gani?
Mimi nilipotewa kiasi kama hicho kwenye Forex... Mambo ya Autotrading.. Trading Robot!!! Kumamae
Mmh,japo tunashauriwa kuwa risk takers ili tufanikiwe but this was too much of you🤔..pole hata hivyo maana hilo tusi hapo mwisho umelitoa kwa uchungu sana😅
 
Back
Top Bottom