Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Mwaka 2016 nilimpa rafiki yangu M.5 kwa ajili ya biashara ya mahindi. Yeye alikuwa na nafasi bila hela, mm nilikuwa na M.5 bila nafasi.

Kweli tukaanza biashara lengo likiwa tufikishe M.20 tuanzishe kiwanda cha sembe na dona, maana eneo nilikuwa nalo. Lakini fedha ilivyofika M 8.7 jamaa yangu hakupatikana tena hadi leo.

Nilibaki mweupe mpka siku moja naenda bank kutoa elfu 10 nikaambiwa haiwezi kutoka, nilikuw na akiba ya elfu 6,300. Nilikonda kila nguo ikawa kubwa kwangu.

Hadi leo sijawahi kunenepa tena.
Rafiki yangu I.M kama uko humu, nilishakusamehe lkn hukufanya vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mwaka 2017 baada ya kumaliza chuo baba yang mdogo aliniunganisha mgodini nkawa napga kazi mshahara ulkuw mdogo kama Laki tatu lakin nilijibana sana ndani ya mwaka nilifikisha M 2.6 ili nifungue duka la dawa sikukaa sawa hata lengo langu halijatimiia mkataba ukasitishwa.
Tulikaa na bamdogo tukashauriana cha kufanya nikaona niende kwanza home huku nkfikiria cha kufanya, eee bwana eee sinikapanda gar mpak home. Ukwel mm nimelelewa na bibi na babu alafu familia mob kinoma huwez amin M 2.1 iliteketea kwa matumiz ya nyumbani na visa vya wazee mara babu atishie kukupa laana kisa hutoi hela na anasema mm ninapesa ila sitoi home na wakat natoa na matumizi nanunua kila mara na pia wakati huo wakati nafanya kazi nilikuwa nawatumia kila mwezi before mkataba haujaisha.
Sikukata tamaa baada ya hayo kutokea nkasema nkampgia sim mamdogo wangu akanitumia kama laki 3.5 nkafungua biashara ya kuuza chipsi, kiukweli niliipenda kazi yangu naondoka asubuh narud usiku, nakumbuka babu yangu ananiambia maneno ya ajabu kuhusu hyo biashara duh! Eeee bwana ee haikuchukua round ilikufa nkawa sina hata 100 nkabak mweupeee.
Nashukuru baada ya miez kadhaa nkaajiliwa serikalini lakin kila mipango ninayo ipanga shetan anaingilia kati saiv ninaandika haya nipo home nilipatwa na ajar ya pikipiki hvyo ndio najipanga kurud kazin ni miez miwili nipo home

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao kina Babu zako,hawabebeki,achana nao,japo kwa mda
 
Nilimuanu jamaa angu kwa kuwa alikuwa msabato tena mzuri Tukaanzisha biashara ya vitabu mimi nilitoa sh 100000 na yeye alitoa sh 40000 kwa kuwa alikua mzoefu wa hiyo biashara na kwa imani yake ya dini nlkamuachia majukumu yote kwa makubaliano ya kila wiki ataniletea sh 10000 kama faida ya kazi na akanambia faida ya wiki si chini ya sh 50000 nikamwambia wewe yako utachukua 40000 mpaka leo ni mwaka na nusu sijaona faida wa mtaji laki yangu imefiapo nikimuuliza napigwa story tu juzi kaniletea kadi ya mchango wa harusi yake machoni niko kawaida ila moyo umejaa sumu naumia sana

COVID-19
 
Pole sana ndugu pamoja na wadau wote wanao pitia changa moto za kimaisha,yatupasa kushukuru Mungu kwa kila jambo,pia yatupasa kuwa makini sana hasa katika suala la kuamini watu ama ndugu wa karibu.
Binadamu ni wachache sana wenye uaminifu,wengi ni wabaya na wanatamaa na hawapendi maendeleo ya wengine,Tusikate tamaa tuendelee kupambana na ninaamini asilimia kubwa wadau wote waliomu humu ni wapambanaji hivyo tukaze buti na tusitizame changamoto kama vitu vya kutuzuia kusonga mbele ila ni vitu vitupavyo uelewa zaidi na kutambua undani wa watu wetu walio karibu jinsi walivyo.kama ni wema au wabaya katika hali zote.

Kingine ni mzazi pekee anaeweza kuona uchungu wa mtoto pale anapo anguka au kufeli katika jambo fulani,hawa dada,kaka,shangazi ,mjomba sijui rafiki,nk ni wachache sana wenye upendo wa dhati,ni kuwa nao makini sana.Walio wengi ni wabaya sana na hawapendi kuona fulani anasonga mbelel.
Kumbuka usidhulumu,kutapeli au kuiba mali au kitu cha mtu yeyote,hii dhambi huwa inadumu na huendelea kuzaa riba,utakuja kupoteza vingi zaidi tena wakati usio taraji na kupoteza baraka ya kufanikiwa kwa mambo yako.kumbuka wema ni akiba,tenda wema kadri unavyoweza,pia samehe kwa walio kukosea na sahau.

Jifunze kupoteza,

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa mwisho umegongea msumali vizuri..
Dhuruma yoyote ila unayoifanya utailipia bila hata kujua na malipo yanakuja kipindi ambacho ni cha muhimu zaidi hata ya kipindi unatenda dhuruma..

Ndio labda waweza ufanye dhuruma na usiilipe kwa njia ya hasara, lakini jua tuu una deni na kwa namna yoyote ila linahitaji malipo.

Lakini pia Sio wote wanaopata mapigo basi ni sababu ya dhuruma..

Pia inaonesha wengi humu wamelizwa na walio waamini,
Poleni wote, tumai siku moja utarejesha ulichokipoteza kwa njia ambayo huijui.
 
Nilimuanu jamaa angu kwa kuwa alikuwa msabato tena mzuri Tukaanzisha biashara ya vitabu mimi nilitoa sh 100000 na yeye alitoa sh 40000 kwa kuwa alikua mzoefu wa hiyo biashara na kwa imani yake ya dini nlkamuachia majukumu yote kwa makubaliano ya kila wiki ataniletea sh 10000 kama faida ya kazi na akanambia faida ya wiki si chini ya sh 50000 nikamwambia wewe yako utachukua 40000 mpaka leo ni mwaka na nusu sijaona faida wa mtaji laki yangu imefiapo nikimuuliza napigwa story tu juzi kaniletea kadi ya mchango wa harusi yake machoni niko kawaida ila moyo umejaa sumu naumia sana

COVID-19
Mkuu Pole..
Moyo wa mtu haupimwi kwa dini au dhehebu lake, ule ni mwemvulitu tuu wa Tigo ila biashara ni M-pesa.
 
NliFungua biashara nikaangukia pua, sikuchoka nikafungua nyingine napo nikaanguka tena,, hadi leo nimekuwa na moyo mzito wa kufanya biashara,

Kuna mwamba ananishauri nianze biashara ya mchele napo roho inasita,

Mwangine ananiambia nunua bodaboda
emoji23.png
,

Biashara ya nguo nliwai ifanya ila sasa wanawake ni adui sana ktk hii biashara,,

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh had forex umefanya?? Unamoyo!!..hahaa pole....udalali unapigwaje?..yes kuna my friend uliwah msaidia kupata mjengo hum😍😍!
 
kwenye udalali kuna mwenye tajiri wa hela na kuna mwenye tajiri wa bidhaa,
sasa naweza kuwa na mteja nikamdirect kwa mwenzangu,yule mwenzangu anapokea chake anakwambia tajiri hajatoa pesa kumbe anachonga na tajiri ili abaki na mgao peke yake,
au unapewa 10,000 kumbe mgao ni 100,000

Kwa sasa nyumba labda kuuza/kununua na viwanja za kupangisha nyumba moja INA chain ya watu saba na bado wanakuzunguka
 
VIBAKA.

hii siku sitakaa nisahau. ilikuwa siku Moja nimetoka ukweni kutoa posa na kulipa mahali, ile bembeleza bembeleza ili tupunguziwe mahali tukajikuta kidogo tunatofautiana na wakwe zetu,baada ya kumaliza na kuagana na washenga wangu mida ya saa tatu usiku hivi naingia home nikiwa nimechoka Kama chizi na mawazo juu ya kupata aibu ukweni, huku bila kujua kuwa Kuna vibaka wamenilia timingi yangu mchana maana nilitoka na pamba Kali. Sasa nafika home hata kuoga sikukumbuka navua nguo na viatu naweka kwenye kochi ili nijilaze kidogo usingizi hkanichukua Moja kwa moja, kuamka saa kumi na moja nakuta dirisha liko wazi pande mbili wamekata nyavu huku nguo zooote za kwenye kochi hazipo, nilizokuwa nimetundika mlangoni hazipo, simu mbili hakuna, pochi hakuna,viatu pair Saba hakuna, vyombo vodogo vodogo hakuna, tv walijaribu kuichomoa kwa kutumia gundi ikawashinda nilikuta Alama kibao wakiwa wanajaribu, redio nilikuta chini maana ilidondoka wakati wanajaribu kuinyanyua kwa gundi. aiseee nikaja kujua daadae kuwa walinipulizia dawa za usingizi ndo maana sikusikia mshindo wowote.

sikuwa na jinsi Bali kuripoti kwa MWENYEKITI wa mtaa hatimae nikaenda polisi japo nilijua hawawezi kunisaidia kwa lolote.

nikapiga ghalama nikaona nimepigwa Kama milioni Moja na nusu kamili na kipindi hicho ndo nilikuwa naanza maisha. nashukuru hawakuwa na uwezo wa kuingia ndani nadhani hata Mimi wangenidhuru.

Aiseeee mtu anakuzunguka
 
nkikumbuka huwa naumia sn, sikutapeliwa na yeyote ila nliwahi pata changamoto ya kiafya dah iliharibu maisha yangu yote nkapoteza kila kitu mpk ndg jamaa marafiki na mwshowe mpenzi, nkajiunga jamii forum ikawa rafiki yangu mkubwa sn, baadae changamoto ikapita ila ndio hvyo nkaanza maisha upya kila kitu kipya hadi marafiki nnao wapya
 
kwenye udalali kuna mwenye tajiri wa hela na kuna mwenye tajiri wa bidhaa,
sasa naweza kuwa na mteja nikamdirect kwa mwenzangu,yule mwenzangu anapokea chake anakwambia tajiri hajatoa pesa kumbe anachonga na tajiri ili abaki na mgao peke yake,
au unapewa 10,000 kumbe mgao ni 100,000

Kwa sasa nyumba labda kuuza/kununua na viwanja za kupangisha nyumba moja INA chain ya watu saba na bado wanakuzunguka

Duh nimeelewa
 
Hati mmechukua asije kukopea tena?
Baada ya mama kufariki tuliachiwa nyumba Mimi na kaka mwangalizi alikua mama mkubwa,kaka aliposimama kimaisha akaomba kupokea kijiti coz nyumba ilikua inaingiza pesa nzuri,mama mkubwa alipoona hivyo akawahi benki fasta akachkulia mkopo m5 afu akachuna no kurudisha marejesho,tunakuja kushtuka mpangaji anapiga simu barua ya kuuza nyumba imekuja deni ni 8.5,..nlikua na miezi 2 ndo nmeanza kazi ikabidi wote na bro tukope ye akatoa3 mi 2 afu zilizobaki tukawa tunalipa kila mwezi,maisha yangu yalikua magumu mwaka ule sitasahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mwaka 2017 baada ya kumaliza chuo baba yang mdogo aliniunganisha mgodini nkawa napga kazi mshahara ulkuw mdogo kama Laki tatu lakin nilijibana sana ndani ya mwaka nilifikisha M 2.6 ili nifungue duka la dawa sikukaa sawa hata lengo langu halijatimiia mkataba ukasitishwa.
Tulikaa na bamdogo tukashauriana cha kufanya nikaona niende kwanza home huku nkfikiria cha kufanya, eee bwana eee sinikapanda gar mpak home. Ukwel mm nimelelewa na bibi na babu alafu familia mob kinoma huwez amin M 2.1 iliteketea kwa matumiz ya nyumbani na visa vya wazee mara babu atishie kukupa laana kisa hutoi hela na anasema mm ninapesa ila sitoi home na wakat natoa na matumizi nanunua kila mara na pia wakati huo wakati nafanya kazi nilikuwa nawatumia kila mwezi before mkataba haujaisha.
Sikukata tamaa baada ya hayo kutokea nkasema nkampgia sim mamdogo wangu akanitumia kama laki 3.5 nkafungua biashara ya kuuza chipsi, kiukweli niliipenda kazi yangu naondoka asubuh narud usiku, nakumbuka babu yangu ananiambia maneno ya ajabu kuhusu hyo biashara duh! Eeee bwana ee haikuchukua round ilikufa nkawa sina hata 100 nkabak mweupeee.
Nashukuru baada ya miez kadhaa nkaajiliwa serikalini lakin kila mipango ninayo ipanga shetan anaingilia kati saiv ninaandika haya nipo home nilipatwa na ajar ya pikipiki hvyo ndio najipanga kurud kazin ni miez miwili nipo home

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu
 
Wakati niko sekondari, nilinunua mkate wa kula juma zima. Siku ya kwanza tu naanza kuula, roommate akaingia na marafiki zake. Kama mnavyojua, utamaduni wetu wa kiafrika, unakaribisha watu. Nikawakaribisha kwa kuzuga. Si wakaja. Wakavamia mkate mzima ukaisha. Tulikuwa tumekaribia mitihani. Ili-disturb matayarisho yangu mpaka nikafeli mtihani. Kwa kweli ilikuwa hasara kubwa sana.
 
....mwisho walinieleza tu ukweli kwamba pesa nilizokua nawatumia wao walifungulia miradi yao shem alinunua pkpk mbili sista akafungua mgahawa wa kisasa wakaniomba radhi na kuniahidi kunilipa kdogokdogo maza nae akanisihi nisiwe na hasira...

hii michezo ipo sana Ifakara...
 
Pole sana ndugu pamoja na wadau wote wanao pitia changa moto za kimaisha,yatupasa kushukuru Mungu kwa kila jambo,pia yatupasa kuwa makini sana hasa katika suala la kuamini watu ama ndugu wa karibu.
Binadamu ni wachache sana wenye uaminifu,wengi ni wabaya na wanatamaa na hawapendi maendeleo ya wengine,Tusikate tamaa tuendelee kupambana na ninaamini asilimia kubwa wadau wote waliomu humu ni wapambanaji hivyo tukaze buti na tusitizame changamoto kama vitu vya kutuzuia kusonga mbele ila ni vitu vitupavyo uelewa zaidi na kutambua undani wa watu wetu walio karibu jinsi walivyo.kama ni wema au wabaya katika hali zote.

Kingine ni mzazi pekee anaeweza kuona uchungu wa mtoto pale anapo anguka au kufeli katika jambo fulani,hawa dada,kaka,shangazi ,mjomba sijui rafiki,nk ni wachache sana wenye upendo wa dhati,ni kuwa nao makini sana.Walio wengi ni wabaya sana na hawapendi kuona fulani anasonga mbelel.
Kumbuka usidhulumu,kutapeli au kuiba mali au kitu cha mtu yeyote,hii dhambi huwa inadumu na huendelea kuzaa riba,utakuja kupoteza vingi zaidi tena wakati usio taraji na kupoteza baraka ya kufanikiwa kwa mambo yako.kumbuka wema ni akiba,tenda wema kadri unavyoweza,pia samehe kwa walio kukosea na sahau.

Jifunze kupoteza,

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamàa unaongea kirahisi sana, tena sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VIBAKA.

hii siku sitakaa nisahau. ilikuwa siku Moja nimetoka ukweni kutoa posa na kulipa mahali, ile bembeleza bembeleza ili tupunguziwe mahali tukajikuta kidogo tunatofautiana na wakwe zetu,baada ya kumaliza na kuagana na washenga wangu mida ya saa tatu usiku hivi naingia home nikiwa nimechoka Kama chizi na mawazo juu ya kupata aibu ukweni, huku bila kujua kuwa Kuna vibaka wamenilia timingi yangu mchana maana nilitoka na pamba Kali. Sasa nafika home hata kuoga sikukumbuka navua nguo na viatu naweka kwenye kochi ili nijilaze kidogo usingizi hkanichukua Moja kwa moja, kuamka saa kumi na moja nakuta dirisha liko wazi pande mbili wamekata nyavu huku nguo zooote za kwenye kochi hazipo, nilizokuwa nimetundika mlangoni hazipo, simu mbili hakuna, pochi hakuna,viatu pair Saba hakuna, vyombo vodogo vodogo hakuna, tv walijaribu kuichomoa kwa kutumia gundi ikawashinda nilikuta Alama kibao wakiwa wanajaribu, redio nilikuta chini maana ilidondoka wakati wanajaribu kuinyanyua kwa gundi. aiseee nikaja kujua daadae kuwa walinipulizia dawa za usingizi ndo maana sikusikia mshindo wowote.

sikuwa na jinsi Bali kuripoti kwa MWENYEKITI wa mtaa hatimae nikaenda polisi japo nilijua hawawezi kunisaidia kwa lolote.

nikapiga ghalama nikaona nimepigwa Kama milioni Moja na nusu kamili na kipindi hicho ndo nilikuwa naanza maisha. nashukuru hawakuwa na uwezo wa kuingia ndani nadhani hata Mimi wangenidhuru.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pengine hata kukufanyia mchezo mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom