Ni haramu kuilipa kihalali kampuni haramu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni haramu kuilipa kihalali kampuni haramu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by asha ngedere, Jan 14, 2011.

 1. a

  asha ngedere Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, hebu mwenye data zaidi aweza kuzimwaga, maana nimekutana na hii taarifa, je, ina ukweli wowote wandugu?

  Ni haramu kuilipa kihalali kampuni haramu!

  • La Dowans ladhihirisha namna Tanzania inavyotiwa vidole machoni na matajiri
  • Mabilioni yanakwenda, lakini kampuni yenyewe haijulikani hata Costa Rica
  Na Daniel Mbega

  KAULI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kusema kwamba mjadala kuhusu suala la malipo ya fidia ya Dowans Tanzania Limited umefungwa imetushtua wengi kwa sababu imemaanisha kwamba serikali imesalimu amri na sasa itailipa kampuni hiyo mabilioni ya wavuja jasho.

  Ingawa niliwahi kulisema suala hili huko nyuma, lakini leo nimelazimika kulizungumzia tena nikijaribu kuangalia namna Watanzania tunavyochezewa kirahisi na wahusika, hasa wenye fedha.

  Nafahamu kabisa suala hili ni la kisheria, kwani ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans dola za Marekani milioni 185.

  Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari wiki tatu zilizopita alisema shirika lake lingeweza kutoa tamko kuhusu hatua za kuchukua kuhusu uamuzi wa ICC na kwamba walikuwa wakisubiri uamuzi huo kusajiliwa rasmi katika Mahakama Kuu nchini.

  Hata hivyo, kwa kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sasa ni rasmi kwamba hakutakuwa na hatua zozote za kisheria dhidi ya uamuzi wa ICC na badala yake Tanesco watatakiwa kujipanga kuwalipa Dowans mabilioni hayo ya shilingi kama walivyoamriwa.

  Hili ndilo linawafanya Watanzania waone kwamba suala hili, pamoja na kupitia katika mkondo wa sheria, lakini lina harufu na mazingira ya kifisadi, kwa sababu taarifa za ndani ya Tanesco zinasema kwamba tayari shirika hilo limeanza kuweka fedha kwa ajili ya malipo katika benki moja (jina tunalihifadhi kwa sasa) jijini Dar es Salaam.

  Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi wamebainisha kwamba hatua yoyote ya kulipa fidia ya shilingi bilioni 185/= kwa kampuni ya Dowans, ni kuhujumu uchumi wa nchi na kuna kila dalili za genge linalohujumu nchi kuandaa mpango wa kutafuta fedha kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.

  Nimepata kusema awali, na hata Watanzania watakubali hili, kwamba inawezekana kwa sababu ni genge hilo hilo lililoamua kukomba mabilioni ya fedha kutoka akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu mwaka 2005 na kuusimika utawala wa awamu ya nne, hivyo kama walifaulu kuvuka vikwazo vyote wakati ule kwa kuchota bilioni 90/=, si ajabu wakachota mara mbili zaidi ya zile za kwanza.

  Sababu sakata la Dowans halina tofauti hata kidogo na lile la Kagoda Agricultural Co. Ltd, kampuni iliyochota bilioni 40/= za EPA na kuzirudisha fedha kwa siri kwenye maboksi baada ya Rais Jakaya Kikwete ‘kuwahurumia’ kwamba wazirejeshe. Mpaka kesho mmiliki wake hajatajwa na hakuna anayethubutu kuinua ulimi wake kumtaja, hata kama anamjua.

  Pamoja na pekua pekua za wanahabari kumbaini mmoja wa watu wenye hisa nyingi ndani ya Dowans, Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, ambaye ni Brigedia Jenerali mstaafu wa Jeshi la Kifalme katika nchi ya Oman, lakini hakuna hata mahali ambako serikali imewahi kuthubutu kuwataja wamiliki wazawa wa kampuni hiyo.

  Dowans Tanzania Limited ilisajiliwa Desemba 2006 hapa nchini kwa msaada mkubwa wa wakili maarufu Dk. Ringo Tenga aliyejitambulisha kama Katibu wa kampuni. Tunaambiwa tu kwa ‘redio mbao’ kwamba wamiliki wa Dowans ni pamoja na mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Abdulrasul Aziz na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa, lakini hakuna aliyekanusha wala kuthibitisha hili.

  Kinachozidi kutia mashaka ni uhalali wa kampuni hiyo kusajiliwa haraka na hatimaye katika kipindi cha miezi mitatu ikapewa mkataba mkubwa wa mabilioni ya fedha, yaani mkataba uliokuwa wa Richmond.

  Ndiyo Dowans Tanzania Limited imetokana na Dowans Holdings S.A ya Costa Rica. Lakini hakuna aliyewahi kuthubutu kuifuatilia kwa makini hiyo kampuni ya Costa Rica na kubaini kama taarifa ilizozitoa zilikuwa sahihi ama la.

  Vyanzo binafsi vya habari za uchunguzi vinabainisha kwamba, Dowans Holdings S.A haipo Costa Rica na kama ilikuwa imeandikishwa huko, basi ilikuwa kampuni ya mkobani tu.

  Kutokana na kubweteka kwa watendaji kuhusu masuala ya kisheria na taratibu nyingine, inaonekana ilikuwa rahisi wakati huo nchini Costa Rica kwa wafanyabiashara wasio waaminifu kumweka “mwanasheria” ambaye angesimama badala yao kama ndiye wakala wa masuala yote.

  Vyanzo binafsi vilivyofanya uchunguzi wa suala hilo nchini Costa Rica vilitembelea ofisi za wanasheria mbalimbali na havikuweza kumpata mwanasheria aliyetajwa kuhusika na Dowans wala anuani yake au mahali ofisi ilipo. Mtu mmoja aliweza kuvieleza vyanzo hivyo kwa siri kwamba wakili huyo hayupo na hakuwahi kuwepo, isipokuwa alikuwa kwenye makaratasi tu.

  Kwenye fomu za Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), Dowans Tanzania Limited imeandikisha kampuni mbili kwamba ndio wanahisa wake wakubwa, mojawapo ikiwa Dowans Holdings S.A yenye aunuani yake AVENIDA DE LA ROSAS 3J
  CALLE BLANCOS, 1150 SAN JOSE, COSTA RICA, na nyingine ni kampuni kubwa ya Singapore na maarufu duniani kwa masuala ya Bandari; Portek Internation of 20 HARBOUR DRIVE #02-01 PSA VISTA, SINGAPORE 117 612 (Portek International Limited).

  Portek iliwaeleza wachunguzi hao huru kwamba haikuwa na hisa za aina yoyote na Dowans Tanzania Limited na kwamba haijihusishi na uzalishaji wa nishaji nchini Tanzania. Mradi pekee waliokuwa nao ni uuzaji wa vifaa mbalimbali kwa kampuni ya TICTIS.

  Aidha, Dowans Holdings S.A inaelezwa kwamba imewahi kuacha machungu katika sehemu kadhaa, na kwa mujibu wa wachunguzi hao huru inaonekana “hakuna kampuni nchini Costa Rica yenye jina la aina hiyo".

  “Kwa kutumia anuani iliyoandikishwa kwenye fomu za BRELA likaelekea kwenye eneo huru la biashara. Kampuni ambayo iko mahali hapo siyo hiyo iliyoandikishwa. Baada ya kupekua kwenye rekodi za umma na za binafsi zikiwemo Msajili wa Taifa (National Registry) wa Costa Rica, Shirika la Simu, Umeme, magari na vyanzo vingine sikuweza kuambua chochote. Si kuhusu “wakili” Bernal Zamora Alce wala kampuni yenyewe,” kinasema chanzo kimoja kilichofanya uchunguzi kwa uzalendo wa taifa la Tanzania.

  Kwa mujibu wa wachunguzi hao, inaonekana kuwa Dowans iliingia nchini Tanzania kwa hila, ikatoa taarifa za uongo na kwa maana nyingine ikawa imejiingiza kwenye ufisadi, na kwa maana nyingine, Dowans ilisajiliwa kimakosa nchini Tanzania na shughuli zake nchini haziko kisheria.

  Aidha, kwa maana nyingi basi, Dowans haina haki yoyote ya kisheria kusimama kwenye mahakama zetu kuomba kulipwa fidia kwa sababu ni kampuni haramu na inaendeshwa kiharamu pia!

  Hivyo basi, serikali ilistahili kutaifisha rasilimali zote za kampuni hiyo na kuwapeleka wahusika wote mahakamani kwa kuiwezesha kampuni hiyo kuingia nchini na kuingia mkataba na Tanesco, kwani walikuwa wanajua taarifa walizozitoa hazikuwa sahihi.

  Ikumbukwe kwamba haya ni maoni yangu, sihukumu wala siingilii uhuru wa mahakama, lakini binafsi naona siyo halali kutoa malipo halali kwa kampuni ambayo si halali, kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya sheria za nchi.

  Jamani, hizi ni fedha za Watanzania, na Tanzania inaongozwa na utawala wa sheria, sasa iweje watu wanavunja sheria kubwa kama hizi halafu wanaangaliwa? Hivi kitengo cha uchunguzi wa masuala ya fedha (Financial Intelligence Unit) kinafanya kazi gani?

  Nauliza pia, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kina majukumu yapi kama si pamoja na kuwachunguza wawekezaji wote wanaoingia nchini? Au kwa vile tunahitaji wawekezaji basi tunakuwa kama jalala linalopokea takataka za aina zote?

  Lazima ifike mahali tuone aibu na kutanguliza uzalendo wa Taifa letu badala ya kuwaonea haya matajiri wachache wanaoingia nchini mikono mitupu na kutoka wakiwa na maburungutu!

  Tuijenge, tuilinde nchi yetu kwa kudumisha amani na kulinda rasilimali za umma, vinginevyo Watanzania watakapochoka watakuja inuka na kunyang’anya mali hizi kwa waliochuma kihalali na kiharamu, kama ilivyokuwa mwaka 1967 wakati wa Azimio la Arusha.

  CHANZO: DIRA YA MTANZANIA JANUARI 3, 2011
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hapana tuwalipe mbona wapokeaji hizo hela siyo haramu kwa mf: Ra, el, karamagi, nimrod mbona wote siyio haramu mbele ya watanzania? Jamani tulipe tu
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwa sababu wewe ni mzambia hazikuumi naona tulipe tuu, mimi mwenyewe mmalawi!
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kama dowans ni haramu basi hata ccm na mwenyekiti wake (rais) ni haramu.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tutaficha mmiliki wake mpaka lini maana waTz wenyewe wameshamjua hata msipomtaja. Mnamkomoa nani?
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Wajilipe tu maana inanikumbusha kisa cha mwehu kutoka baru na nguo za mwenye akili timamu alipomkuta mtoni akioga...tumepiga sana kelele na suala hili la DOWANS na wanaonekana wamejiziba masikio,wafunge mjadala kwa upande wao..wakiishagawana hizo rasilimali pesa zetu halali kwa njia haramu mijadala tulokwisha ianza kabla ya wao mdogo wa kujilipa itaamua tuwafanyeji..nadhani ni Watanzania wachache sana wasiojua ukweli wa mambo...Ujumbe umefika!
   
Loading...