Ni halali wizara zetu kutuwekea aina ya mavazi (dressing code) ilikupata huduma?

NOD

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
848
682
Mwaka jana nilikwenda katika wizara moja nikiwa na shida ya kuwaona wahusika. Ajabu sana nilizuiwa kuingia eti kwa sababu nilivaa jeans na tshirt nikiwa nadhifu kabisa. Kijana aliyenipokea alijaribu sana kunielewesha kuhusu huo utaratibu. Nilimuuliza nini mantiki ya hiyo amri? Alikuwa mkweli kuwa kuna sababu za maana na pia mitazamo ya wakubwa kidini! Iliniuma sana baada ya huyo kijana kuonyesha pia kukelwa na utaratibu huo huku akionyesha tangazo lenye hayo mavazi yanayotakiwa. Alisema yeye ni msandawi hivyo kwa jinsi anavyoyafahamu mavazi yao haitakuwa rahisi kwa watu wa kijijini kwao kuhudumiwa hapo wizarani. Nafikiri hawa mawaziri walioanzisha utaratibu huu walilewa madaraka na kusahau kuwa kazi yao ni kutoa huduma kwa hao waliowaweka hapo (wananchi) katika hali yoyote nitakayokuja nayo na sio kuangalia mavazi wala matakwa ya imani zao. Yule kijana alinitajia wizara nyingine ambazo wanaendesha utaratibu huo bila kujali maana ya huduma kwa umma. Watanzania wana tamaduni na imani tofauti hivyo sio haki waziri kujiamlia kuwa anataka nivae vipi tukiachilia mbali uvaaji wa kihuni uliopitiliza. Kuwawekea dress code wananchi wako, tena kwa msingi ya utamaduni au imani yako, ni dharau isiyo kifani na inatakiwa ifutwe mara moja. Kumnyima huduma mtanzania na hata mgeni eti kwa sababu hajavaa unavyotaka ni uzembe na aibu kubwa kwa hao tuliowapa dhamana. Kama inatakiwa kukidhi matakwa yako ya kiimani nenda kafanye kazi kanisani au msikitini kinyume Cha hapo toa huduma kwa wananchi bila masharti yasiyo na kichwa wala miguu. Hili ni jipu na linafaa kutumbuliwa!!
 
Utaratibu huu ulishaanza siku nyingi. Mimi binafsi siupendi ila ninapoenda ofisi za serikali lazima ni dress "appropriately". Pengine inabidi wai review na wananchi wapate taarifa mapema. Ni embarrassing sana kurudisha getini.
 
Back
Top Bottom