Ni halali wizara zetu kutuwekea aina ya mavazi (dressing code) ilikupata huduma?

NOD

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
848
682
Mwaka jana nilikwenda katika wizara moja nikiwa na shida ya kuwaona wahusika. Ajabu sana nilizuiwa kuingia eti kwa sababu nilivaa jeans na tshirt nikiwa nadhifu kabisa.

Kijana aliyenipokea alijaribu sana kunielewesha kuhusu huo utaratibu. Nilimuuliza nini mantiki ya hiyo amri? Alikuwa mkweli kuwa kuna sababu za maana na pia mitazamo ya wakubwa kidini!

Iliniuma sana baada ya huyo kijana kuonyesha pia kukelwa na utaratibu huo huku akionyesha tangazo lenye hayo mavazi yanayotakiwa. Alisema yeye ni msandawi hivyo kwa jinsi anavyoyafahamu mavazi yao haitakuwa rahisi kwa watu wa kijijini kwao kuhudumiwa hapo wizarani.

Nafikiri hawa mawaziri walioanzisha utaratibu huu walilewa madaraka na kusahau kuwa kazi yao ni kutoa huduma kwa hao waliowaweka hapo (wananchi) katika hali yoyote nitakayokuja nayo na sio kuangalia mavazi wala matakwa ya imani zao.

Yule kijana alinitajia wizara nyingine ambazo wanaendesha utaratibu huo bila kujali maana ya huduma kwa umma. Watanzania wana tamaduni na imani tofauti hivyo sio haki waziri kujiamlia kuwa anataka nivae vipi tukiachilia mbali uvaaji wa kihuni uliopitiliza.

Kuwawekea dress code wananchi wako, tena kwa msingi ya utamaduni au imani yako, ni dharau isiyo kifani na inatakiwa ifutwe mara moja. Kumnyima huduma mtanzania na hata mgeni eti kwa sababu hajavaa unavyotaka ni uzembe na aibu kubwa kwa hao tuliowapa dhamana.

Kama inatakiwa kukidhi matakwa yako ya kilimanjaro nanda kafanye kazi kanisani au msikitini kinyume Cha hapo toa huduma kwa wananchi bila masharti ya Siyo na kichwa wala miguu.

Hili ni jipu na linafaa kutumbuliwa!!
 
umenikumbusha pale UTUMISHI wana "kijibango" chao cha mavazi nao na mlinzi nje.....lolhaha..
 
Unaenda wizarani na kata k?
Kapombe nimetanabaisha kuwa sio mavazi ya kihuni na yasiyo na heshima kwa jamii. Nachouliza ni vipi mtanzania anyimwe huduma kwa vazi kama jeans au mgolole?
 
ni sahihi kabisa wanavyoweka dressing code kwani kuna watu hawajui kuwa ni mahali gani wanatakiwa kuvaa mavazi gani mtu anavaa vazi la beach kwenda ofisini jeans ni vazi la kazi ila huku ndio tunafanya vazi la kutokea
 
Ha ha ha! Pole sana ndugu. Ila lingeingia kundi la wafadhili wa kizungu wakiwa utupu ungeshangaa jinsi maofisa wakuu wanavyohangaika kuwapokea na kuwakaribisha kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza kujadili ajenda muhimu za kitaifa na kimataifa. The world is not fair.
 
Rodrick kuna dress code ya wafanyakazi na vazi la heshima la mtu anayehitaji huduma. Labda tujadili kwa kutilia maanani Hilo. Official dress code ya mfanyakazi hilo ni swala la kisheria kwa mfanyakazi na nitofauti na uvaaji wa heshima (vigumu kuuelezea) wa mtu baki anaekuja kuhudumiwa.
 
Mwaka jana nilikwenda katika wizara moja nikiwa na shida ya kuwaona wahusika. Ajabu sana nilizuiwa kuingia eti kwa sababu nilivaa jeans na tshirt nikiwa nadhifu kabisa.

Kijana aliyenipokea alijaribu sana kunielewesha kuhusu huo utaratibu. Nilimuuliza nini mantiki ya hiyo amri? Alikuwa mkweli kuwa kuna sababu za maana na pia mitazamo ya wakubwa kidini!

Iliniuma sana baada ya huyo kijana kuonyesha pia kukelwa na utaratibu huo huku akionyesha tangazo lenye hayo mavazi yanayotakiwa. Alisema yeye ni msandawi hivyo kwa jinsi anavyoyafahamu mavazi yao haitakuwa rahisi kwa watu wa kijijini kwao kuhudumiwa hapo wizarani.

Nafikiri hawa mawaziri walioanzisha utaratibu huu walilewa madaraka na kusahau kuwa kazi yao ni kutoa huduma kwa hao waliowaweka hapo (wananchi) katika hali yoyote nitakayokuja nayo na sio kuangalia mavazi wala matakwa ya imani zao.

Yule kijana alinitajia wizara nyingine ambazo wanaendesha utaratibu huo bila kujali maana ya huduma kwa umma. Watanzania wana tamaduni na imani tofauti hivyo sio haki waziri kujiamlia kuwa anataka nivae vipi tukiachilia mbali uvaaji wa kihuni uliopitiliza.

Kuwawekea dress code wananchi wako, tena kwa msingi ya utamaduni au imani yako, ni dharau isiyo kifani na inatakiwa ifutwe mara moja. Kumnyima huduma mtanzania na hata mgeni eti kwa sababu hajavaa unavyotaka ni uzembe na aibu kubwa kwa hao tuliowapa dhamana.

Kama inatakiwa kukidhi matakwa yako ya kilimanjaro nanda kafanye kazi kanisani au msikitini kinyume Cha hapo toa huduma kwa wananchi bila masharti ya Siyo na kichwa wala miguu.

Hili ni jipu na linafaa kutumbuliwa!!
T shirt na jeans nadhifu mbona msikitini poa tuu
 
Ha ha ha! Pole sana ndugu. Ila lingeingia kundi la wafadhili wa kizungu wakiwa utupu ungeshangaa jinsi maofisa wakuu wanavyohangaika kuwapokea na kuwakaribisha kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza kujadili ajenda muhimu za kitaifa na kimataifa. The world is not fair.
Hata kwa wazungu kuna dressing code, kuna sehemu niliwahi fanya kazi Ijumaa ndio angalau unaruhusiwa mavazi fulani ambayo ni simpl T-Shirt or so. Nami nadhani nia ni nzuri hiyo ya kusema dini fulani sina uhakika, ila kama ikiwekwa holela inaweza tomkea vituko. All in all ni suala la debate as wtu wengine km wanmasai wanaweza kosa huduma.
 
Mwaka jana nilikwenda katika wizara moja nikiwa na shida ya kuwaona wahusika. Ajabu sana nilizuiwa kuingia eti kwa sababu nilivaa jeans na tshirt nikiwa nadhifu kabisa.

Kijana aliyenipokea alijaribu sana kunielewesha kuhusu huo utaratibu. Nilimuuliza nini mantiki ya hiyo amri? Alikuwa mkweli kuwa kuna sababu za maana na pia mitazamo ya wakubwa kidini!

Iliniuma sana baada ya huyo kijana kuonyesha pia kukelwa na utaratibu huo huku akionyesha tangazo lenye hayo mavazi yanayotakiwa. Alisema yeye ni msandawi hivyo kwa jinsi anavyoyafahamu mavazi yao haitakuwa rahisi kwa watu wa kijijini kwao kuhudumiwa hapo wizarani.

Nafikiri hawa mawaziri walioanzisha utaratibu huu walilewa madaraka na kusahau kuwa kazi yao ni kutoa huduma kwa hao waliowaweka hapo (wananchi) katika hali yoyote nitakayokuja nayo na sio kuangalia mavazi wala matakwa ya imani zao.

Yule kijana alinitajia wizara nyingine ambazo wanaendesha utaratibu huo bila kujali maana ya huduma kwa umma. Watanzania wana tamaduni na imani tofauti hivyo sio haki waziri kujiamlia kuwa anataka nivae vipi tukiachilia mbali uvaaji wa kihuni uliopitiliza.

Kuwawekea dress code wananchi wako, tena kwa msingi ya utamaduni au imani yako, ni dharau isiyo kifani na inatakiwa ifutwe mara moja. Kumnyima huduma mtanzania na hata mgeni eti kwa sababu hajavaa unavyotaka ni uzembe na aibu kubwa kwa hao tuliowapa dhamana.

Kama inatakiwa kukidhi matakwa yako ya kilimanjaro nanda kafanye kazi kanisani au msikitini kinyume Cha hapo toa huduma kwa wananchi bila masharti ya Siyo na kichwa wala miguu.

Hili ni jipu na linafaa kutumbuliwa!!

Wenzetu nchi zilizoendelea wameshafanikiwa kuondosha mawazo kama hayo ya kuwabana raia wake kwa mavazi wanayovaa,ukweli Tanzania ni moja katika nchi zenye raia wenye akili mgando,mimi binafsi ziwezi kuamini kama serikali inakuja na sera kama hizo wakati kuna mambo mengi muhimu ya kuwafanyia raia wake.

Kuna kitu kinaitwa "Freedom of expression" yaani ni uhuru wa kumwachia binaadamua afanya anachofanya lakini havunji sheria za nchi,kuvaa ni uhuru wa kila binadamu,tukumbuke tu kuwa kuna binadamu hasa tuchukulie ndugu zetu wa kike,mama zetu ni watu walioumbwa kwa kuwa na umuhimu wa kujiona kapendeza,wengine wanapenda kuonyesha maumbo yao wengine hawapendi,binadamu hatuko sawa.

Sasa hawa dada zetu na ndugu zetu wa kike kuwanyima uhuru wao wa kuvaaa wanachotaka ni kuwanyima haki zao za ubinadamu,Serikali ya TANZANIA inasema haina dini watu ndio wenye DINI kwa muono wangu serikali isiwe na mawazo au sera kama hizo ni uvunyifu wa haki za binadamu....

Wawachie watu wajidai wawe na UHURU wakujiamulia hapo ndio serikali itawapata watanzania hamu ya kuipenda nchi yao...
 
sawa tu watuwekee sababu wengine mavazi yao yanafanya watu waache kazi wawe wanaangalia uumbaji wa aliye juu
 
kwa hiyo mavazi yetu ya kiasili hayaruhusiwi kwenye wizara zetu hizi?ngachookkaaaaa kapsaa!
 
Mtazamo wangu juu ya suala hili ni kua Serikali imekosea. Tena tamko linahitajika mara moja dhidi ya unyanyaswaji unaofanyika. Dressing code ni kwa wafanyakazi tu wa ofisi ndio wanhelazimishwa kuvaa nguo za staha. Mtu akifata huduma hata avaeje bado apewe huduma aondoke. Kwakua hakuna sare basi watumishi watoa huduma wavae kama walivyoelekezwa na si wageni wajao maofisini. Huduma haihitaji isivae jeans wakati wazungu wanafika maofisini na jeans zao wanaruhusiwa kuingi kwa uzungu wao.
 
Back
Top Bottom