Ni Halali Watoto wa Nje ya Ndoa Kuwaita WANAHARAMU???

Tuseme kwa faith ya wale waaminio mtoto wa kando, ni waharamu itabaki kua hivyo katika slogany but nijuavyo mie Baba still atakua responsible ku'provide frm A-Z juu ya huyo mtoto wa kando ecxept urithi ndiyo hatorithi, na hapo ndiyo source ya uharamu ilipoanzia.
Yaani mtoto wa kando kupata mirathi ya Baba ni haramu lakini kumridhi mama yake sio haramu.
Na Baba kumlea mtoto wa kando si haramu na niwajibu wake.
Nadhani watu mnajichanganya sana, mtoto wa kando ndio mtoto gani huyo? ebu nipe tafsiri, mimi sijao na nina mtoto mmoja ili jina la mtoto wa kando wewe unalitowa wapi?
 
Ni wapi nilipokutangazia kwamba mimi nimekubuhu kwa uzinifu? usinilazimishe mimi kuishi kwa imani unayoifuata wewe, ok, mimi ni muumini wa dini yangu ya kale ya mababu zangu, dini zetu za ukristo na uislamu usidhani kila mtu anaendeshawa na hizo imani zenu mlizoletewa wakati wa biashara ya utumwa.
Hao waliowaletea dini zao sidhani kama wanamjuwa mungu, maana haingii akilini kuleta dini sambamba na biashara ya utumwa. Heshima ni kitu cha bure.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza ndugu! Nimenukuu pale uliposema kuwa:mimi sina ndowa na nina mtoto.

pia mimi sijakulazimisha kuwa ufuate kile ninachokiamini mimi. Kwani imani yangu inaniambia hivi:

Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo. Qur'an 23:12

Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Qur'an 23:13

Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyoganda, na tukaumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi mungu mbora wa waumbaji. Qur'an 23:14

Huyo ndiye aliyeniletea dini na si kama unavyodai wewe. Sasa sijui hizo dini za kale za mababu zako sijui wameumba nini! Narudia tena samahani kama nitakuwa nimekukwaza kwani haikuwa kusudio langu.
 
Nimetoa angalizo mapema kwamba hapa sitaki nimkwaze mtu kwa imani yake, lakini wewe unataka kuniondowa kunipeleka kwenye imani yako bila mimi kupenda.
Ni hivi kama dini yako inakuongoza uwe na mahakama ya kadhi kwa ajili ya mirathi hiyo ni juu yako na mungu wako, mimi imaani yangu inaniongoza kumuwezesha mtoto mapema, na kurithi mali zangu mimi naweza kulithisha charity yoyote ile na familia yangu isipate chochote..
Kwahiyo uelewe mimi sio muumini wa Mirathi.

Hapana mkuu hujanikwaza! Na wala sikulazimishi kukuvutia kwenye imani yangu bila ridhaa yako. Huo ni uwamuzi wako.

(1) Umeuliza:Hivi mtu unakaa chumba kimoja cha kupanga utaacha urithi gani dnia hii? Nami nikaeleza hivi, kurithi ni haki ya mtoto.si lazima uwe umeacha magari,nyumba na vinginevyo chochote utakachokiacha hata kama ni kijiko atakirithi.

(2) Ukasema tena: na kwa nini ifikiriwe kwamba watoto kazi yao ni kurithi tu na sio wao kumiliki mali na wazazi wao ndio waje kurithi kama mtoto ataanza kufariki.

Kwanza nikueleze tu ya kuwa kurithi sio kazi. Kurithi ni haki ya mtu. Hata kama warithi walishajitafutia mali zao,lakini bado wao wana haki ya kurithi mali zilizoachwa na wazazi wao,au wazazi kwa watoto wao au ndugu wengine pia. Na urithi unakuja baada ya mrithiwa kuaga dunia. Si kweli kuwa mrithi hawezi akajishughulisha katika kujitafutia mali yake au mzazi akamuwekea misingi mtoto wake eti 7bu tu atakuja kurithi mali za wazazi wake hapana!

(3) Hizi dini msizifuate kama misukule, changanyeni na akili zenu.

Ufahamu tu kuwa dini ni mfumo wa maisha ambao binadamu anatakiwa awenao katika kila siku ya maisha yake hadi mwisho wa uhai wake. Sasa kwa vile wewe ni mpagani,huwezi kulielewa somo hili kutokana na kile unachoamini!
 
Dini zenu zote zinaeleza wazi wazi kwamba mnatakiwa mtoe 10% ya kipato chenu kila mwaka kama dhaka, mbona kipengele hiki kimekuwa kigumu sana kwenu kama mnafuata huo mfumo wa maisha?
 
hahaha mkuu Amavubi....umenikumbushakipindi cha kampeni za kura za maoni Yusuph Makamba alipomuita Nape Mtoto haramu
 
mtoto hana kosa kabisa.ila aliyemzaa nje ya ndoa ndo haramia mkubwa.wanaume wengi wanazaa watoto, kwa kuheshimu status yake kijamii ana mpotezea nje.matokeo yake mama mtoto anakosa matunzo mtoto anakuwa wa mtaa.alafu wanakutana mtoto akiwa baa medi baba anajichukulia kimwana.BE RESPONSIBLE FOR THE CONSEQUENCES OF YOUR SEXUAL INTERCOURSE
 
mtoto ni mtoto...inawezekana wa njee ndo akakusaidia kuliko mitoto yako ya ndoa,ni afadhali uwalee na uwape maisha boraa,na elimu bora kama wa ndani tu,cse wote ni damu yako...ila kunamijitu inauzi sanaa,haina chochote still bado inazalisha wanawake ovyoo njee?
 
Navyo fahamu mtoto akizaliwa nje ya ndoa anaitwa wadi al haramu au bent al haram sababu-amezaliwa aje ya ndoa...sababu ya kuitwa vile ni wazazi wao walikubali kufanya kitu kilicho katazwa na mungu-na watoto wao kuitwa haramu si kosa sababu wazazi wao walisha kosea na anaye kosea lazima ayajutie makosa yake.

Logic hakuna mtu anakubali mtoto wake aitwe haramu-sasa kama yeye hakubali mtoto wake kuitwa haramu-kwanini alifanya hayo.

Mototo kuitwa haramu si vizuri lakini kazaliwa kiharamu-kwa kuwa kazaliw akiharamu basi muiteni mtoto wa haramu tu.
 
Hayo maneno niliyoyakazia ni ya lugha ya kiarabu kwa kiswahili tungesema kijana nje ya ndoa au binti nje ya ndoa. Kwa lugha ya kiarabu yanaweza kuwa yanatamkika bila kukwaza mtu lakini kiswahili hayatamkiki kwa stara ndio maana tunasema '..nje ya ndoa'

Ni kosa kuwaita hivyo kwa mantiki ya lugha na stara. Kama wazazi walikosea yeye hakuwepo uharam wake unatoka wapi? Kama tutakubaliana kuwa ni haram basi huyo hafai kuwa na dini (nikimaanisha muislam kwa maudhui ya neno na nilivyokunukuu). Sasa nionyeshe wapi mtoto nje ya ndoa imeandikwa katika Quran au hadithi kuwa hapaswi kuwa muumini( Naomba unielimishe)
Nasema hivyo kwasababu kilicho haram ni kile kilichokatazwa na mola, sasa kama yeye ni haram tayari, uhalali wake upo wapi katika uumini. Je unataka kusema huyu hafai kuwa muumini! kama sivyo je aombe msamaha kwa mola wake kwa kosa lipi alilotenda?

Kama wazazi walikosea na mtoto alikuwa hayupo na wala hakushiriki kuanzia 'kusomeshana hadi mipango na utimilifu wake' yeye anakuwa amekosea nini?

Kula chakula mchana wakati wa mfungo ni haram, hiyo haimfanyi aliyekosea kula awe haram hata kidogo sasa kwanini hili la mtoto liwe tofauti.

Haram ni tendo lililokatazwa

Angalizo: Tafsiri za lugha zinatofautiana na lugha ni chombo kinachobeba utamaduni. Kunatakiwa umakini wakati wa matumizi yake.
Mfano, ni rahisi sana kusikia katika TV na Radio za nchi kama za magharibi neno 'vagina' tena katika mijadala ya hadharani.
Hebu jaribu kulitumia neno hilo kama lilivyo katika lugha ya kiswahili uone kama jamii haiatakuachi radhi na laana kama utasalimika kisago!!
 
Kunasehemu nime highlighted in red hapo unafurahisha....Sasa hata sisi binadamu tunamakosa gani kukosa pepo alio ipata Adam na Hawa kabla hawajafukuzwa kule na Mungu....Wakati Adam na Hawa ndo waliokosea....huoni hapo kama baba na mama wamefanya makosa na mtoto lazima ale adhabu.

Sasa ndo vile vile kama mtoto kazaliwa nje ya ndoa, kiarabu au kiswahili anatiwa mtoto wa haramu pia.
 
Imeelezwa katika aya gani ya Koran takufu au hadithi ipi kuwa mtoto anayezaliwa nje ya ndoa atahukumiwa kwa kosa hilo
 
Back
Top Bottom