Ni halali SUA kuwa na TV au kiwanda cha maziwa?

wadau Hiki kitu nimekuwa nacho moyoni nadhani huu ni mwaka watatu sasa, Kwa tulio wengi tunajua Malengo ya kuanzishwa kwa SOKOINE UNIVERSTY - MOROGORO ni nchi iwe na wataalamu wakutosha wakilimo, ni wazo jema kabisa, ila kilichonishangaza ni hao wasomi wa chuo hicho kuanzisha televison( SUA TV) nadhani ni Tv ya kwanza kumilikiwa na chuo kikuu hapa Tanzania, moyoni najiuliza ni kwa nini wasingeanzisha kiwanda cha maziwa na nyama?????naamini pesa mlizotumia kuanzishia hiyo TV zingetosha sana tu kwa hilo lengo, mtajitetea na kusema ni pesa za wafadhili na jiuliza mlishindwaje kuwa na hilo wazo kama mlitaka kuonekana SEREKALI si ina TV yake ambayo mgeingia nao mkataba wawe wanaonyesha mambo mliyokuwa mnataka jamii iyaone??? Hamkuona kiwanda cha maziwa hata bna baadae cha nyama kingekuwa na manufaa zaidi kiliko hiyo TV??naamini nyie ndo mlikuwa watu wa kwanza kuwa na mashamba ya mfano na hicho kiwanda ambacho naamini hakingewagarimu pesa nyingi kihivyo kuliko hiyo TV.Mbona wakenya wameweza? Chuo kikuu cha Egerton ni chuo cha kilimo kama nyie wameweza kuanzisha shamba la ngome na wana kiwanda cha maziwa ambacho kinatumika kama sehemu ya wanafunzi kujifunzia na maziwa yao wanayauza miji mbalimbali kya kenya kwa kupitia mawakala.

Wananzuoni wa SUA badilikeni,hata hiyo TV yenu haionekani maeneo yote ya morogoro mgekuwa mnatuzalishia maziwa naamini yangesambaa karibu TZ yote na kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza

Wadau nawakilisha??????

Katika pitapita zangu leo nimekutana na hii mada ya miaka mingi hapa jukwaani
Ni majuzi wazizri wa viwanda alikuwa Morogoro na alitamka SUA ni sleeping GIANT...na ndugu waziri hakukosea kabisa
Sijui tatizo ni nini SUA wanamashamba yao kila ukienda ulizia mbegu za Ngombe... Mbuzi.....kuku...kondoo..kupata ni shida saana......niligundua wanampaka kampuni inayomanage hayo Mashamba lakini ukilinganisha na wenzao Kenya au Uganda Wao kwa asilimia kubwa wamelala kabisa....sasa hivi Tanzania kuna mwamko mkubwa wa vijana kujikita kwenye sector ya kilimo.....hii ilikuwa ni fursa kwa wataalam wa sua kuwasaidia...watu wanahangaika wapape wapi Mbegu mfano za kuku.,Ngombe......Nilitamani hata SUA TV wangekuwa wanatengeneza vipindi wawe wanaviweka online au WAWE WANAUNGANA NA TBC kumbe wapi.... pesa za uendeshaji wa hiyo TV sibora wangekuwa wananunua airtime TBC Tanzania nzima ikaelimika...wao wamebaki kufundisha ....job seekers.....badala ya job creators.......
 
Wadau,

Hiki kitu nimekuwa nacho moyoni nadhani huu ni mwaka watatu sasa,

Kwa tuliowengi tunajua Malengo ya kuanzishwa kwa SOKOINE UNIVERSTY - MOROGORO ni nchi iwe na wataalamu wakutosha wa kilimo, ni wazo jema kabisa, ila kilichonishangaza ni hao wasomi wa chuo hicho kuanzisha televison( SUA TV) nadhani ni Tv ya kwanza kumilikiwa na chuo kikuu hapa Tanzania, moyoni najiuliza ni kwanini wasingeanzisha kiwanda cha maziwa na nyama?

Naamini pesa mlizotumia kuanzishia hiyo TV zingetosha sana tu kwa hilo lengo, mtajitetea na kusema ni pesa za wafadhili na jiuliza mlishindwaje kuwa na hilo wazo kama mlitaka kuonekana SEREKALI si ina TV yake ambayo mgeingia nao mkataba wawe wanaonyesha mambo mliyokuwa mnataka jamii iyaone?

Hamkuona kiwanda cha maziwa hata baadae cha nyama kingekuwa na manufaa zaidi kiliko hiyo TV naamini nyie ndo mlikuwa watu wa kwanza kuwa na mashamba ya mfano na hicho kiwanda ambacho naamini hakingewagharimu pesa nyingi kihivyo kuliko hiyo TV. Mbona wakenya wameweza? Chuo kikuu cha Egerton ni chuo cha kilimo kama nyie wameweza kuanzisha shamba la ngome na wana kiwanda cha maziwa ambacho kinatumika kama sehemu ya wanafunzi kujifunzia na maziwa yao wanayauza miji mbalimbali kya kenya kwa kupitia mawakala.

Wananzuoni wa SUA badilikeni, hata hiyo TV yenu haionekani maeneo yote ya morogoro mngekuwa mnatuzalishia maziwa naamini yangesambaa karibu TZ yote na kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza.

Wadau nawakilisha?
Kwanza nikuambie tu...SUA wanakiwanda cha maziwa! Japo ni kidogo ila kina supply maziwa campus nzima! Ukienda sua pita pale nyuma ya department ya engineering utayakuta!!

Nadhani ungesema wakikuze kiwe kikubwa zaidi!!
 
Back
Top Bottom