Ni halali SUA kuwa na TV au kiwanda cha maziwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni halali SUA kuwa na TV au kiwanda cha maziwa?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Prodigal Son, Dec 21, 2009.

 1. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Wadau,

  Hiki kitu nimekuwa nacho moyoni nadhani huu ni mwaka watatu sasa,

  Kwa tuliowengi tunajua Malengo ya kuanzishwa kwa SOKOINE UNIVERSTY - MOROGORO ni nchi iwe na wataalamu wakutosha wa kilimo, ni wazo jema kabisa, ila kilichonishangaza ni hao wasomi wa chuo hicho kuanzisha televison( SUA TV) nadhani ni Tv ya kwanza kumilikiwa na chuo kikuu hapa Tanzania, moyoni najiuliza ni kwanini wasingeanzisha kiwanda cha maziwa na nyama?

  Naamini pesa mlizotumia kuanzishia hiyo TV zingetosha sana tu kwa hilo lengo, mtajitetea na kusema ni pesa za wafadhili na jiuliza mlishindwaje kuwa na hilo wazo kama mlitaka kuonekana SEREKALI si ina TV yake ambayo mgeingia nao mkataba wawe wanaonyesha mambo mliyokuwa mnataka jamii iyaone?

  Hamkuona kiwanda cha maziwa hata baadae cha nyama kingekuwa na manufaa zaidi kiliko hiyo TV naamini nyie ndo mlikuwa watu wa kwanza kuwa na mashamba ya mfano na hicho kiwanda ambacho naamini hakingewagharimu pesa nyingi kihivyo kuliko hiyo TV. Mbona wakenya wameweza? Chuo kikuu cha Egerton ni chuo cha kilimo kama nyie wameweza kuanzisha shamba la ngome na wana kiwanda cha maziwa ambacho kinatumika kama sehemu ya wanafunzi kujifunzia na maziwa yao wanayauza miji mbalimbali kya kenya kwa kupitia mawakala.

  Wananzuoni wa SUA badilikeni, hata hiyo TV yenu haionekani maeneo yote ya morogoro mngekuwa mnatuzalishia maziwa naamini yangesambaa karibu TZ yote na kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza.

  Wadau nawakilisha?
   
 2. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145

  duuuu kaka nakupa senks,una mawazo ya mbali sana,
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  asante kaka, hawa wataalamu wa SUA wanaturudisha nyuma kabisa, tunatakiwa tuwaambie kwani wengi wamesomeshwa kwa kodi za wazee wetu, mambo yanayohusu kilimo hatuwasikii hata kidogo, wangekuwa na kitu kama hicho ingekuwa chachu kwa wanafunzi pindi wanapomaliza wangeweza kuwa na mawazo chanya na kufikiria hata kufungua viwanda vidogo vya maziwa kwenye maeneo yao naamini wanaweza pata mkopo hata SIDO kama bank itakuwa ngumu

  Watanzania hususani wasomi tunatakiwa tuamke
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tusiwalaumu sana wanazuoni wa hapo SUA, hii ni system ambayo imeharibika kuanzia kwa viongozi wa juu!
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hayo ni mawazo mgando...! Sometimes tuache ushamba.....hata website ungetaka vyuo vyote vya umma visiwe nazo kwa vile wizara mama ina website...! Lol..!
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  The two are not mutual exclusive!
   
 7. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kama wanauwezo SUA wawe na vyote viwili TV na kiwanda cha maziwa au zaidi. Vyote ni muhimu
   
 8. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nafikiri aliyeandika hiii thread hafahamu nini maana ya chuo kikuu. kazi ya chuo kikuu ni kufundisha, kutafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu, chuo hakiwezi kuanzisha kiwanda ila kama unasema demonstration unit sawa. Nafikiri na mazumuni ya kuanzisha TV ni kuweza kuiwasilisha elimu hiyo kwa wananchi kupitia program mbalimbali wanazozitegemea. Nafikiri unajua tatizo la usambazaji wa technology kwenda kwa wananchi ulivyo mgumu na unahitaji pesa nyingi kwa hiyo kwa kutumia hivyo vipindi wanaweza kuelimika sana na kutumia hiyo elimu kwa maendeleo yao.
   
 9. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  sidhani kama upo sawa kwani kwa kutumia vyombo vya habari vya serekali, hiyo elimu unayosema ingewafikia watanzania wote, TV yao hata morogoro yote haionekani, cha msingi hapa vyuo vingine vya kilimo kama SUA vina miradi ambayo inaendana na elimu wanayotoa, nimetoa mfano wa Egerton,UDSM ni sawa wawe na TV na radio kwani inatumika na wanafunzi kama sehemu ya kufanyia practicals, ila kwa SUA ni upotezaji wa rasilimali na kukosa mwelekeo kwa upande wa chuo.wanaweza wakaingia mkataba na private inividuals au company na kuwa na shamba la mifugo pamoja na kiwand akidogo cha maziwa lengo wanafunzi wapate pakujifunzia kwa vitendo
   
 10. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  Lyangalo sijakurupuka nilipoandika, na ninauelewa mzuri saana wa maana ya chuo kikuu, UDS wana TV. Radio na Gazeti, ambayo vyote vinatumika kama sehemu ya wanafunzi kujifunzia kwa vitendo na biashara ili viweze kujiendesha,Chuo Kikuu cha Egerto kenya wanachamba kubwa la ngombe na kiwanda cha kuprocess maziwa, Kiwanda cha maziwa hakihitaji technologia kubwa saana na wala mtaji wake sio mkubwa kama wa kuanzisha TV,Vyuo vikuu vinanvyofundisha masomo ya Tourism na Hospitality wana Hotel ambazo zinaendeshwa kibiashara na zinatumika kama sehemu ya wanafunzi ya kujifunzia sasa nini cha ajabu SUA kuwa na kiwand acha mzaziwa??????
   
 11. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  sio SUA pekee yenye tv, kwani hujasikia mlimani TV
   
 12. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  soma vizuri post yangu, naamini utanielewa
   
 13. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #13
  Dec 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi 100%, ndo maana watanzania wengi tunafeli mambo mengi,Vitu tunavyosoma atuvi-implement kwenye maisha yetu,tunaviacha kwenye vitunzia kumbukumbu tu, tungekua na timu ya ma-thinker kama nyie, nchi hii ingekua mbali sana
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  agree!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Mi sidhani kama ni vibaya kwa SUA kuwa na televisheni yake...inatumika kueneza ujuzi mpya wa kilimo kwa hao hao wachache inaowafikia.

  Na sidhani kama ni sahihi kwa SUA kuwa na kiwanda cha maziwa. Ninavyojua pale wanafuga Ng'ombe wa mfano kwa ajili ya maziwa (naamini na mbuzi na kondoo pia wapo) na ni kazi ya watanzania wengine kuanzisha hivyo viwanda vya maziwa na mashamba ya mfano kwa kutumia utaalam wa pale SUA!
   
 16. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kaizer, kwa wanafunzi wakitanzania kinachotakiwa ni elimu ya vitendo,n dicho kitakachotuokoa na ushindani wa EAC, hilo halina ubishi kumbuka tuna TBC ambayo wangeweza kuitumia ikawafikia watanzania wote, mawazo yangu ni chuo kuwa na miradi ambayo inakuwa na manufaa mojakwamoja kwa wanafunzi na chuo kwa ujumla, kuwa na mashamba ya mifugo na kiwand aau viwand avya kutengeneza mazao yake ni jambo la msingi, hao watanzania wengine unaowazungumzia ni wakina nani cha na hiyo elimu wataipata wapi? Tatizo wanafunzi wanfundishwa kwa nadharia tu ulimwengu wa sasa kinachotakiwa ni vitendo, Mbona egerton wamefanikiwa wankiwanda na shamba kubwa la mifugo na wanaofanya kazi kubwa hapo kiwandani ni wanafunzi, wanapomaliza wengi wemeweza kurudi vijijini mwao wakiwa na ujuzi wa kutosha,
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi kabisa.

  Chuo kikuu cha Sokoine hakikuwa na haja ya kutumia mapesa yote yale ya umma kujenga TV ambayo haionekani nchi nzima. Kingeweza kabisa kuomba serikali ikipatie muda kwenye TV ya taifa kutolea matangazo yake kwa vile sidhani kama kweli chuo kile kina program za kurusha kwa masaa 24 kiasi cha kuhitaji kituo chao binafsi. Kwa kawaida vyuo vinavyomiliki vyombo vya habari huwa pia vinatoa mafunzo ya uandishi na usambazaji wa habari (mass communications); kwa hiyo vyombo vile vinakuwa ni sehemu ya kufundishia wanafunzi kwa vitendo. SUA hawana kozi yoyote ya namna hiyo, kwa hiyo kuanzisha TV ile ama wameajiri wanahabari kuindesha kwa gharama za chuo au inaendeshwa bila utaalamu. Na kama wameajiri wanahabari na wanaiendesha TV ile kibiashara, basi ni afadhali wangeendesha biashara inayoambatana na utaalamu utolewao na chuo hicho badala ya hiyo biashara ya matangazo. Na vile vile kama wanaiendesha bila utaalamu basi hayo ni matumizi mabaya ya pesa za umma.
   
 18. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Lete mada za maana mkubwa hivi kipi cha muhimu kuwa na kiwanda cha nyama na maziwa au TV inayosambaza matokeo ya tafiti na kutoa elimu kwa wakulima Chuo kikuu si sehemu ya kufanya biashara practical wanafunzi wanaweza kwenda kwenye viwanda husika ambavyo si lazima vimilikiwe na chuo na ndo maana kuna study tours. pia kwa taarifa ni kwamba mashine za kukamua na kusindika maziwa zipo hapo department of animal science nafikiri kusambaza elimu ya kilimo ni bora zaidi ya kufanya biashara
   
 19. chishango

  chishango JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  kaka elimu kwa vitendo si kwa wanafunzi wa kitanzania tu malengo ya kuanzishwa vyuo vikuu si kufanya biashara wazo lako la kwenda vijijini baada ya kumaliza masomo chuo kikuu kwa mfumo tulionao haliwezekani kila mhitimu atawaza kutafuta kazi ya kuajiriwa tatizo ni mfumo ambao hautoi fursa ya wahitimu wa fani mbalimbali kudhaminiwa mikopo na serikali toka katika taasisi za fedha ili wakaanzishe miradi usipotoke kaka kama kuna chuo ambacho wanafunzi wanamaliza wakiwa fit practically basi ni SUA jaribu kufanya utafiti katika soko la ajira tatizo si masomo kwa vitendo bali ni mfumo thats why utakuta mtu kamaliza BSc Agriculture General hapo SUA lakini yupo kaajiriwa Bank watu awana option bali ni kufanya kazi yoyote
   
 20. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  SUA TV kwa covarege ipi hata morogoro yote haionekani, its better if you can THINK BIG, ni tafiti zipi ambazo zimeshawahi tangazwa na hiyo TV, je mwananchi wa kigoma anaweza faidika vipi na hiyo TV, Unatakiwa uwe na mtazamo chanya kwani kama hizo mshine zipo department animal science are they utilized effectively??? watanzania tulio wengi tunapoambiwa ukweli huwaga tuankuwa wabishi kukubali na kuelewa, nayaongea haya ili wakenya na Waganda watakaporuhuiswa waje kwenye soko la ajira la TZ naamini waathirika wakwanza watakuwa na wanafunzi wa SUA hilo halina ubishi
   
Loading...