Ni halali Mbunge mteule kila kiapo cha Uwaziri kabla ya kile cha ubunge?

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Tumeshuhudia wabunge wanoteuliwa na rais wakila viapo vya uwaziri na unaibu kabla ya viapo vya ubunge
swali langu ni kuwa je kwa sasa hawa mawaziri ambao ni wabunge wa kuteuliwa wanakidhi matakwa ya kisheria yanayotaka waziri kuwa mbunge?
 
Very good question. .......!! Ila inaelekea kwa Magufuli kila kitu kinawezekana!!!
 
Sijui ni kwa nini hawa washauri wa Rais hawamkumbushi na kumshauri vitu vidogo vidogo kama hivi ambavyo kisheria naamini ni kuvunjwa kwa katiba kumwapisha mtu kuwa waziri wakati hajaapishwa kuwa mbunge sifa inayomwezesha kuwa waziri.

Hii ni sawa kuruhusiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita bila kwanza kuwa umefanya mtihani wa kidato cha nne unaokupa sifa ya kufanya wa kidato cha sita.
 
Mbunge ni mbunge toka anapochaguliwa au kuteuliwa.
Anaweza kufanya kazi zote za ubunge isipokuwa ndani ya bunge mpaka aapishwe kwanza.

Hata waziri anaweza kuwa waziri ili mradi achaguliwe au kuteuliwa kwanza kuwa mbunge.

Ila hawezi kwenda kujibu bungeni maswali mpaka aapishwe kwanza.
Hakuna sheria iliyokiukwa hapo.
 
sheria inatambuwa mamlaka ya uteuzi yaani kama mbunge akichaguliwa na wananchi basi anakua na hadhi hiyo ya ubunge...hatua ya kula kiapo bungeni ni kula nadhiri ya kulitumikia bunge kama mhimili na utiifu kwa spika...kwahiyo walichofanya wale wabunge wateule ni kula kiapo cha utiifu kwa raisi...wakienda bungeni watakula kiapo cha utiifu kwa bunge na spika...kwahiyo hakuna utata hapo kilichofanyika ni halali kisheria
 
Wewe na mimi tukubali tu.kama kuna manufaa sheria ya nini....?????Sheria ngapi zimevunjwa na zinaendelea kuvunjwa.....????1:sheria ya madini ilipitishwa na wabunge wangapi 2:sheria ya kumpata Mayor wa Kinondoni na Ilala..3:Sheria ya rushwa ktk uchaguzi nk.Tuweke sheria pembeni twendeni tu
 
Sijui ni kwa nini hawa washauri wa Rais hawamkumbushi na kumshauri vitu vidogo vidogo kama hivi ambavyo kisheria naamini ni kuvunjwa kwa katiba kumwapisha mtu kuwa waziri wakati hajaapishwa kuwa mbunge sifa inayomwezesha kuwa waziri.

Hii ni sawa kuruhusiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita bila kwanza kuwa umefanya mtihani wa kidato cha nne unaokupa sifa ya kufanya wa kidato cha sita.

usilolijua ni usiku w giza...rudisha shule mkuu ama tafuta maarifa kuliko kufanya hitimisho katika mambo usiyoyajua
 
Mbunge ni mbunge toka anapochaguliwa au kuteuliwa.
Anaweza kufanya kazi zote za ubunge isipokuwa ndani ya bunge mpaka aapishwe kwanza.

Hata waziri anaweza kuwa waziri ili mradi achaguliwe au kuteuliwa kwanza kuwa mbunge.

Ila hawezi kwenda kujibu bungeni maswali mpaka aapishwe kwanza.
Hakuna sheria iliyokiukwa hapo.

Great Thinker Ahsante
 
Kuna utata hapo tena utata mkubwa sana. Unapoteuliwa/kuchaguliwa kuwa mbunge unakuwa ni MBUNGE MTEULE, na huwezi kuitumikia hiyo nafasi kisheria mpaka kwanza uapishwe na Spika ndani ya Bunge. Vivyo hivyo kwa Rais anapochaguliwa, anakuwa hana mamlaka ya kisheria mpaka kwanza aapishwe, hata unapoteuliwa kuwa Waziri unakuwa ni Waziri mteuliwe mpaka utakapoapishwa.

Katika hili Magufuli ameteleza, maana sheria inatamka kuwa anapaswa kumteua Waziri kutokana na miongoni mwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano(Sio wabunge wateule) hivyo kimantiki wale wabunge alitanga kuwateua ili kuja kuwa Mawaziri, ilipaswa kwanza waende kuapa bungeni ili uteuzi wao wa kuwa mawaziri uwe na nguvu ya kisheria.

Huwezi kuvaa Soksi baada ya kuvaa viatu, Soksi kwanza then ndio viatu!!
 
Wewe na mimi tukubali tu.kama kuna manufaa sheria ya nini....?????Sheria ngapi zimevunjwa na zinaendelea kuvunjwa.....????1:sheria ya madini ilipitishwa na wabunge wangapi 2:sheria ya kumpata Mayor wa Kinondoni na Ilala..3:Sheria ya rushwa ktk uchaguzi nk.Tuweke sheria pembeni twendeni tu

ujinga umekuelemea hadi umepata mtando wa ubongo mahaba yanakufanya umwone magu kama anatosha kwa kila unalohitaj wewe
 
Hijja sikutegemea kupata jibu kama hilo toka kwa mtu mwenye jina la Ki ungwana kama lako.Hata hivyo kabla ya kunitusi ungesoma vizuri bandiko langu ungenielewa vizuri na wala usingenitusi.Kama wakuu wanafanya hivyo wewe na mimi tunakitugani cha kuweza kuzuia.Wewe kubali tu.
 
Mbunge ni mbunge toka anapochaguliwa au kuteuliwa.
Anaweza kufanya kazi zote za ubunge isipokuwa ndani ya bunge mpaka aapishwe kwanza.

Hata waziri anaweza kuwa waziri ili mradi achaguliwe au kuteuliwa kwanza kuwa mbunge.

Ila hawezi kwenda kujibu bungeni maswali mpaka aapishwe kwanza.
Hakuna sheria iliyokiukwa hapo.

Mbunge anakamilishwa na sifa zipi?
Na kuna maana gani ya kusema waziri lazima awe mbunge!
 
Hakuna mbunge mteule mbunge anakuwa mbunge soon baada ya kuchaguliwa ama kuteuliwa anaweza kufanya kaz zote kama mbunge
 
Kuna utata hapo tena utata mkubwa sana. Unapoteuliwa/kuchaguliwa kuwa mbunge unakuwa ni MBUNGE MTEULE, na huwezi kuitumikia hiyo nafasi kisheria mpaka kwanza uapishwe na Spika ndani ya Bunge. Vivyo hivyo kwa Rais anapochaguliwa, anakuwa hana mamlaka ya kisheria mpaka kwanza aapishwe, hata unapoteuliwa kuwa Waziri unakuwa ni Waziri mteuliwe mpaka utakapoapishwa.

Katika hili Magufuli ameteleza, maana sheria inatamka kuwa anapaswa kumteua Waziri kutokana na miongoni mwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano(Sio wabunge wateule) hivyo kimantiki wale wabunge alitanga kuwateua ili kuja kuwa Mawaziri, ilipaswa kwanza waende kuapa bungeni ili uteuzi wao wa kuwa mawaziri uwe na nguvu ya kisheria.

Huwezi kuvaa Soksi baada ya kuvaa viatu, Soksi kwanza then ndio viatu!!

Great-lakini wengine tuna mahaba yetu, tutahalalisha tu au tutafumba macho.
 
Ile hatua tulopiga katika kuikuza demokrasia na kufata mfumo wa kisheria ulowekwa na kikwete
naona awamu hii umeanza kuvurugwa km si kuufutilia mbali
mungu mkuu tuongoze
 
Hiki Kisanga Nakumbuka Hata Kipindi Cha Kwanza Cha Uwaziri Wa Muhongo 2014 Kilijadiliwa Humu.Kumbukumbu Zinaonesha JK Alimwapisha Huyu Jamaa Uwaziri Kabla Ya Ubunge Kuapa Na Maisha Yaliendelea.Kisheria Nadhani Haikatazi Japo Kimantiki Inaleta Walakini!!
 
Back
Top Bottom