ni halali birthday kupita kimyakimya nami nna mpenzi

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,696
1,062
habari za wikend wanajamvi,
jamani miaka kadhaa huko cku ya leo nilifanikiwa kuja duniani, sasa tangu niamke asubuhi naskilizia licha ya kupewa zawadi hata wishes za mdomo sijazickia kutoka kwa mpenzi, jamani roho yaumia kuna kupendwa kweli hapa au nazugwa, na mimi nnavyopenda someone apay attention kwangu mshkaji kama hana kalenda vile, nimkumbushee au nimchunie niendelee kuila kimyakimya
 
ni vyema umkumbushe. Kusahau kupo. Au pengne ameplan kukufanyia bo bo booonge la sapuraizi.
 
Hakuna uhusiano wowote wa mapenzi na birthday. Ni siku kama siku nyingine tu.

Kama mwenyewe sikumbuki birthday yangu we ni nani nilazimike kukumbuka yako?

Mambo ya wazungu yanawavurugeni sana vijana wa dot com
 
subiri saa tano na dakika 59 ndiyo umkumbushe ya mwakani hatasahau tena
 
Hakuna uhusiano wowote wa mapenzi na birthday. Ni siku kama siku nyingine tu.

Kama mwenyewe sikumbuki birthday yangu we ni nani nilazimike kukumbuka yako?

Mambo ya wazungu yanawavurugeni sana vijana wa dot com

mmh bora hujawa mpenzi wangu ungenipasua kichwa kwa kukataa uzungu
 
Pole sana! Happy birthday!

Kwani ukimkumbusha ni tatizo?
 
mmh bora hujawa mpenzi wangu ungenipasua kichwa kwa kukataa uzungu

Una umri gani bibie? Uzungu utawalostisha. Mapenzi ya kitamthilia ni full uzushi.

Haya hebu mambie kwanini umemsakama mpenzi wako na wala si mama yako aliyekuzaa kwa uchungu, au baba yako aliyemmimbisha mama yako, au kaka na dada zako mliozaliwa tumbo moja?

Kwanini lawama ziende kwa mpenzi na wala si kwa wengine? Kumbuka mpenzi si nduguyo na wakati wowote mnaeza achana.

Tafakari, chukua hatua.
 
Happy birthday!

Pamoja na kuwa tuna miaka zaidi ya 7 pamoja, hadi leo sijawahi kukumbuka b'date ya mpenzi wangu
 
hahahaaaaaaaaaaa hata mimi mwenyewe huwa sikumbuki birthday yangu, kuna vitu vya msingi sana ambavyo mpenzi asipokukumbuka utaumia: let say unauma afu asikujulie khali, lakini birthday loh mie nawaza anifanyie tofauti sana, sijawahi kumwambia happy birthday wala yeye hajawahi maisha yanasonga, ila kwenye uso wa kitabu kwenye wall utapata nyingi sana.
 
Hiyo BD ya ngapi tangu uwe naye? kama ndo ya kwanza mkumbushe!!! but wewe unaabudu BD? kwn kwako ulitaka ufanye nini? au mjamaa unataka ku-do-tu, kwanza hata hukuandaa kitu maana mandalizi lazima ungemshirikisha... acha umwambie kisha aseme kaenda kwa rafiki yake na mtaonana kesho, mbona hukusema mapema d, kesho, bye!!! halafu ulie peke yako sisi ngoja tuangize nyingine hapa
 
Una umri gani bibie? Uzungu utawalostisha. Mapenzi ya kitamthilia ni full uzushi.

Haya hebu mambie kwanini umemsakama mpenzi wako na wala si mama yako aliyekuzaa kwa uchungu, au baba yako aliyemmimbisha mama yako, au kaka na dada zako mliozaliwa tumbo moja?

Kwanini lawama ziende kwa mpenzi na wala si kwa wengine? Kumbuka mpenzi si nduguyo na wakati wowote mnaeza achana.

Tafakari, chukua hatua.

...hahahhaaaaaaa hubby umeua hahhah......
 
punguza presha,kwa watu wengine kama mimi bday ni minor issue sijawahi kukumbuka birthday yangu,most of the time friends ndo huwa wananikumbusha,sasa ya mtu mwingine ndo basi tena
 
Back
Top Bottom