Ni haki wanajeshi kutoa kichapo kwa raia wasio na hatia ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni haki wanajeshi kutoa kichapo kwa raia wasio na hatia ?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by GHIBUU, Mar 17, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Na A.Salum,
  Wanajeshi wa JWTZ wametembeza kipigo kwa kila mtu katika maeneo ya Jangonmbe….na kuendelea: eti madam wa mmoja wa wanajeshi hao ameibiwa kipochi.
  Sasa tujiulize: kwanza tuna uhakika gani kama kipochi kimeibiwa (kipochi cha mke wa mfalme, mfalme wa Tanganyika anayeitawala Zanzibar).


  Je, wanajeshi wanatakiwa kuchukua sheria mikononi mwao? na Isiwe chochote….
  Je, ni watu wangapi wanaoibiwa vipochi, simu, pesa nk hapo Zanzibar; na hatujaona watu kupigwa au angalau kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria…kwa sababu wanaoiba ni wenzao, na wanawaibia wazanzibari (haki yao kupata shida).


  Mimi yote hayo hayakunishangaza, ni mambo ninayoyategemea sana kutukuta sisi wazanzibari- naweza kusema kutokana na udhaifuwetu tulionao.Pili, waziri wa ulinzi tuliyenaye, yeye pia kwa zanzibar ni mfalme, anafanya na kusema anavyotaka – anathubutu kuisema kuwa ‘hajiuzulu ngo’ kwa sababu hakuripua yeye mabomu! ya mbagala wala ngongo la mboto. yeye like father/like son — wote mafia baba yake ni mafia wa kusali na kusalisha.


  Lakini, je, ingalikuwa tukio hili aliyepigwa ni mtoto wa waziri au mheshimiwa yeyote (lakini anayetoka katika nasaba ya kifalme, tanganyika, ingalikuwaje). Mheshimiwa mzanzibari si chochote, si lolote kwa kuruta mmoja tu wa Tanganyika.
  Ilivyo hasa, wanajeshi hawa watiwe adabu kw amujibu wa sheria zao ‘court marshall’. Lakini watapewa vyeo, maana wamepiga na hata kuuwa mzanzibari ni sawa.


  Amiri jehsoi wetu Mkuu — bwana JK…yeye ni ‘check bob’ tu: asafiri kwenda ivory coast na kurudi, na kutaka kujidai kusulusha kila kwenye tatizo wakati nyumba yake inanuka kama mzoga kw akila aina ya uchafu. Ah…! vizuri sana Tanzania dunia imewapa uso bado.
  Mimi ingalikuwa ni Dgabo au Mugabe au yeyote nisengeliwez akukubali kusulishwa na JK.


  Haya, nisije kuambiwa nina-mix mambo na mada. Mada yetu ni JWTZ kupiga watu/raia wasiokuwa na hati..kwa sababu mke wa mfalme ameibiwa kipochi. Unajua wanajeshi hawa moja ya kitu cha kwanza wanachofundishwa ni chuki dhidi ya zanzibar na wazanzibari. hakuna chengine.
  Inashangaza sana na sisi wazanzibari hatujangamua chochote au namna ya kujitayarisha. tumefunikwa na mambo yasiyokuw ana maana tu kama ‘mabadiliko ya katiba, au GNU au Zanzibar Mpya — hizi ni fantasy tu. haziwezi kutufikisha pahala, zaidi zinatupozea malengo na fikra.


  Hivi kweli TZ au Zanzibar inahitaji katiba mpya? Yaani kwa zanzibar, kwa sasa, kama utapinga katiba mpya — wewe ni adui tu, kama ulivyokuwa unaohoji GNU/SUK au kuipiga CUF au CCM. Tunakwama kwa sababu hatuna ‘national agenda’.


  Iwe iwavyo, JWTZ hawakufanya haki. Na Bado waziri wa ulinzi Dr.Hussein Mwinyi atasema hahusiki wala hajiuzulu. Baadaye anakuja mtu anasema TZ inaongoza kwa marks za utawala bora duniani? Dr.Hussein Mwinyi endelea kukalia kiti, na Mzee Mwinyi pia– like father/like son – wote mafia waliobobea.
   
 2. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu umeandika mambo mengi na yanayo sikitisha. Kiujumla hakuna mtu aliye juu ya sheria yaani hata amiri jeshi mkuu.isipokuwa umejadiili kwa kuonyesha kaama vile wamefanyiwa hivyo kwa kuwa ni wazanzibari .wakati hata bara yanatokea
   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Ila zanzbar ndio imezidi mambo haya,,,,lazima waseme sana,,,,
   
 4. M

  Meck Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashauri wanapoenda kwenye mafunzo yao ya awali ktk mitaala yao wawekewe somo la HUMAN RIGHTS inawezekana labda huwa hawafundishwi,no one is above the law bwana.
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wote wana makosa mwizi anakosa na aliyechukua sheria mkononi anakosa pia, kila mtu ana hitajika kufikishwa mahakamani kujibu shtaka lake.

  Hata hivyo kwa sisi waislaam mwizi ukatwa mikono! labda hiyo adhabu ya kipigo ni mbadala maana mi ninge kuwa mwizi, bora kichapo cha Jeshi kuliko kukatwa Mikono; kinachonishangaza ni kwanini walipiga watu wengi, maana maelezo yako yanaonyesha kibaka aliyepora ni mtu mmoja au hilo eneo lote ni la vibaka?!
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu Arafat.
  Wewe ni muislamu uliyepo nchi ipi?
  Tanzania sijawahi kusikia waislamu wakikatana mikono? Au hapo unapoishi kuna islamic court? Tanzania hakuna hata kadhi courts!

  Tanzania kuna mahakama ya mtaani ambayo wananchi wenye hasira ,mara nyingi kibaka huhukumiwa adhabu ya kifo, kibaka hupigwa chochote na wengine hufa.

  mahakama nyengine ni ya serikali, huko kibaka akitoa rushwa huachiwa akafanye ukibaka wake mitaani.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ni vema na haki. maana nchi hii imejaa raia wavivu wasiotambua hata haki zao kiasi kwamba hata wanajeshi wanatushangaa.
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapa nilipo kuna Kadhi Courts, Mzee mwizi Mkono unaondoka na Mzinzi mawe hadi kufa, ila ebu niweke sawasawa Zanzibar hamna Kadhi kweli!, mbona kama na kumbuka ipo, labda kama wanaogopa sharia wanakimbilia Sheria za dola, ebu futilia unisaidie hapa kwa PM tafadhali?!
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Kulia kushoto kulia kushoto kulia. There is no best for ef double o el than to let him pass.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Usidanganye watu, hakuna nchi inayojitapa kuwa wanafata Sheriah kama Saudi Arabia na huko watu hawakatwi mikono kwa petty thefts kama hizo za simu.
  Halafu Mzee wangu sielewi wewe ni Muislamu gani usiejuwa kuwa Kadhi kazi yake sio kuhukumu makosa ya jinai. Wacha Bwana, usijivike kanzu kwa lengo la kuleta kejeli kwa dini za wenzako!
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wanakata Mikono kwa wizi upi Mkuu? we tatizo lako unataka kule ligi za dini na utoto hapa, Mi ni Muislaam tena kuliko wewe bendera tu, hujui lolote katika hili kwa taarifa yako mi nimeishi Saudi Arabia (Kingdom of Saudi Arabia) unataka kuleta ubishi wa kitoto hapa, hujui maana ya Mahakama au neno Kadhi Court ndi linakuchanganya? kuamua kesi gani mtu akatwe mkono siyo hoja hapa, hoja ni kuwa Sharia inasemaje kuhusu mwizi! si kila anayefikishwa mahakamani anafungwa au anashindwa keshi au lazima akatwe mkono, hilo ni jambo lingine Mkuu, inategemea mahakama itaperuzi vipi ushahidi ulifikishwa mbele yake, ila ujue wapo wanaokatwa kama hujui na wamekatwa mikono wengi tu.

  Kinachotuponza sisi Waislamu wa nchni maskini wengi wetu wamegoma kufikiri na kuelimika. Ndio maana hakuna mtoto wa Kiarabu hata mmoja anaye vaa bomu kujilipua tunavaa sisi maskini, maskini ata akili yake inakuwa maskini, Mzee mwili mlimpiga wanini hapo Dar kama siyo ufinyu wa elimu tena ya Dini. Kama unashida na elimu ya Dini nitafute acha kuchakachuliwa akili yako na Wazee wenye njaa hapo Tanzania, Mzee Gorogosi mlimuuwa wa nini?
   
 12. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Katika hilo tukio walipigwa ni watoto wadogo tena wanafunzi,,,,inasikitisha,,,wamewapiga vibaya sana wamewajeruhiii,,,,ndio maana tunauchukia muungano sisi wazanzibari...
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hivi JWTZ haina wazanzibari? Munachukia muungano lakini hamjitahidi vya kutosha kujiondoa!
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu Arafat.
  Kama wewe ni mwislamu na mtanzania ulipaswa kujua zaidi hili la Kadhi courts hapa TZ kuliko mimi.

  Lakini la msingi kwa vile uko huko na zipo Kadhi courts ujikinge na wizi na uzinzi. bado tunahitaji michango yako hapa JF.
  Nimefuatilia kuhusu Mahakama ya kadhi Tanzania.
  Findings.
  Tanzania bara uko mjadala au malumbano ya uanzishaji wa kadhi courts.

  Zanzibar ipo kadhi court lakini inajishughulisha na mambo ya ndoa za kiislamu na mirathi ya kiislamu haihukumu makosa ya jinai. kwa hiyo hakuna mtu aliyewahi kukatwa mikono,kichwa au miguu huko kwa hukumu ya mahakama hii.

  Bonus...Kenya pia wanayo kadhi courts ambayo inashughulika na ndoa za kiislamu na mirathi ya kiislamu na mahakama kuu ya Kenya inaweza kutengua hukumu ya mahakama hii kama rufani itapelekwa dhidi ya hukumu ya kadhi courts. Pia huko hakuna mtu aliyewahi kukatwa mkono, kichwa, kidole ,sikio au mguu kutokana na hukumu ya kadhi courts.

  Nilichojifunza hapa ni kuwa Kadhi courts za huko uliko ni tofauti na kadhi courts za Kenya na Zanzibar. Za huko uliko wanatumia islamic laws kama penal code ya mfumo wa mahakama, tofauti na Tanzania, Tanzania bara(Tanganyika) au Zanzibar ambazo zinatumia common laws.

  Mkuu Arafat kula kitabu vizuri ukirudi uwasaidie waislamu wenzako katika kujiendeleza kielimu. nimekusoma hapo juu ya watoto wa mabomu na umasikini na elimu. Umelijua tatizo ,uwasaidie kulitatua.
   
Loading...