Ni haki kwa binti kumtia adabu mama wa bf wake?

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,223
2,902
Habari zenu wadau,mwenzenu hili limenipa utata kidogo,kuna kaka fulan amepanga nyumba ya jiran na ninapoishi huyu jamaa ni mtoto pekee kwa baba na mama yake ila baba alishafariki,mama yake nae anaishi mtaa wa jirani na anapoishi mwanae, huyu mama siku zote alishapanga mwanae akitaka kuoa basi aone binti wa kitanga ila kwa bahati mbaya yule kaka hakuwahi kubahatika kuwa na mpnz wa kutoka tanga,ikawa mama yake anamfatilia kwa kila mpnz anayekuwa nae na akigundua sio wa tanga anaanzisha visa vya ajabu mpaka msichana anaamua kutosa jamaa,visa vyake ni pamoja na kuibuka kwa mwanae alifajiri na akikuta jamaa kalala na binti panachimbika amtukana huyo binti na kumfukuza na kumkanya kumona na mwanae, sasa tabia hiyo ikamkera sana jamaa akaamua kuwashirikisha ndugu wengine wa mkanye mama yake tabia hiyo, ila huyo mama hakuacha na akaendelea na upuuzi wake,sasa jamaa akapata binti wa kichaga na kabla hajaanza kwenda nae kwake alimpa story nzima kuhuhsu tabia ya mama yake, yule dada akubali na kumwomba jamaa amruhusu kukomesha tabia mbaya ya mama yake, jamaa kutokana na kero za mama na amempenda yule dada na ana mapango wakumuoa akaubali.

Sasa juzi kati mama akagundua mwanae ana mpnz na huwa anakuja kulala mara kwa mara, kama kawa siku hiyo kaibuka kwa mwanae saa kumi na moja alfajiri akagonga yule dada ndio akaenda kumfungulia, alipoingia tu akaanza kumhoji yule binti anafanya nn pale na maswali kibao mpaka kabila binti akamwambia ni mchaga, mama akaanza kubwata katukana sana mda wote jamaa yuko chumban anasikilizia,yule binti akafunga malango wa kutoke nje na akamuuliza yule mama sababu za kutukanwa na kutakiwa aondoke pale mda ule ni nn,yule mama hakujibu akamkata kibao yule binti, wandugu dada alitembeza kibano cha ukweli kwa bi mkubwa mpaka akawa naomba msaada jamaa hakutoka chumbani,binti akamwambia bi mkubwa apige magoti na amwombe msamaha na aahidi kuacha tabia yake chafu, ili kuepuka kipigo zaidi bi mkubwa akakubali na wakayamaliza na mama akaondoka kimya kimya bila hata kuuliza aliko mwanae,je hata kama mama mkwe ni mcharuko ni haki kwa binti kumtia adabu?wadau mnalionaje hili nawakilisha.
 
AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Hii story bana imenimaliza... kwamba kwa mama mshari hivo kakubali na kua mpole baada ya kupigwa kichapo!! Hata hivo sijaelewa hao wahusika... Ogopa saana mwanaume ambae hamueshimu mamake (no matter ana madhaifu gani hata kama ni CD) to the extent anakuruhusu wewe mwanamke uwe Mke let alone galfriend akuruhusu upitishe kipondo kwa mamake na akaridhia kabisa katulia.... Oh! My dear such a MAN... To me is not man at all... Moja ya vigezo vya mimi kutambua a GOOD MAN ni the way he treats and respects his Mother and sisters regardles huyo Mkwe na dadake wananifanyia nini..... For yeye kuwaheshimu No matter what!! Is a guarantee to me hata tukija gombana na kuachana DAIMA ataniheshimu hivo hivo.....

Naomba hata hivo pitia hii Link (Ladies Understand your Mamamke) yaweza kua msaada thou sio kwako but to the lady in question....
 
Kwanza habari ya ww dada mkubwa,kwakweli hata mie hili limenipa ukakasi kidogo ndio maana nikaamua kulileta hapa nione wadau wao wanalionaje na watasemaje, asante dada ngoja nicheki hii link!
 
BornTown

JF-Expert Member
May 7, 2008
1,716
478
mmh! inasikitisha kwa kweli ila huyo mama nadhani atakoma hatosahau katika maisha yake
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534
Haa hii naona kama binti alishapewa kibali cha go ahead na kijana maana kutokutoka kwka jamaa kumsaidia mamake ni wazi kuwa aliridhia kichapo kitembezwe. Ingawa si ustaarabu lakini mwe na sie wamama nasi tumezidi. KAma humtaki huyu binti huna haki ya kumtukana wala kumpiga, kuwa mstaarabu nawe uheshimiwe. Tusilas=zimisha kufanya maovu kwa kuwa tu tu watu wazima na tunaowafanyia wanatakiwa kutuheshimu ili waonekane wana heshima. Kumbuka kuwa ma yule binti ni binadamu, kuna ile ya kushindwa kujizuia ati........hata mie kuna mambo huwa nayafanya out of hacra then najikuta nalazimika kuomba msamaha baadae lakini ujumbe unakuwa umefika.
 
Kijana aliruhusu mama arekebishwe ila hakujua ni kwa njia ipi,wewe unadhani bint alikuwa na haki ya kumpiga huyo mama?
 
Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,223
2,902
Hakuwa na haki ya kumpiga. Na jamaa kama anataka usalama wa maisha yake, asimuoe huyo demu la sivyo atajuta.
Kama ni mpango wa mungu wao kuoana wanaweza fika huko,unafikiri binti kakosea wapi kama alipewa ruhusa ya kumrekebisha mama mkwe bila kupewa mipaka ya njia atakazotumia?
 
daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,277
738
No matter what the case could have been,wote kijana na binti ni washenzi na hawana adabu hata kidogo. Hivi huyo binti kweli anapata wapi ujasiri wa kuinia mkono na kumpiga mama wa kijana anayedai anampenda? na huyo kijana anapata wapi ujasiri wa kumruhu huyu girlfriend ampige mamake?
sidhani kama hao wawili watakaa waoane unless kwanza walitambue kosa watubu mbele ya Mungu wao,mama yao,jamii na mioyo yao ndo watafanikiwa.
Mama ni mama tu jamani hata kama anamapungufu gani.
 
daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,277
738
Kwanini? Kwani huyo mama ye ana haki ya kumtukana binti wa watu? Kwa misingi ipi na kwa kosa gani alilolifanya huyo binti? Embu tueleze, we ungeweza kwenda kumtukana huyo binti wa watu? Na ungekung'untwa ungelaumu?

Kwa hiyo huyo binti ana haki ya kumpiga mama wa bf wake?
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
No matter what the case could have been,wote kijana na binti ni washenzi na hawana adabu hata kidogo. Hivi huyo binti kweli anapata wapi ujasiri wa kuinia mkono na kumpiga mama wa kijana anayedai anampenda? na huyo kijana anapata wapi ujasiri wa kumruhu huyu girlfriend ampige mamake?
sidhani kama hao wawili watakaa waoane unless kwanza walitambue kosa watubu mbele ya Mungu wao,mama yao,jamii na mioyo yao ndo watafanikiwa.
Mama ni mama tu jamani hata kama anamapungufu gani.

binti hapa kwa kweli hii story ina uwalakini lakini tuichukulie kama ilivyo..
huyo binti na bf wake wote ni swashenzi na huyo kijana hana malezi sahihi , hivi kweli wewe na akili yako ukubali mama yako mzazi apigwe na gf wako unategemea huyo mtu mkioana atakuwa na heshima na mama mkwe wake???
hata kama mama ana makosa kulikuwa na njia mbadala ya kumrekebisha lakini siamini kweli mama apigwe wewe umekaa chumbani huo ni ubabe au ujinga
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,531
2,523
He makubwa haya, ukistaajabu ya Musa (mama mtu) utaona ya Firauni (mkwe mtarajiwa).

Tukiwa wakweli wote wawili ni wakosa. Huyo mama mzee mwenzangu ni mkosa kwa kulazimisha mwanawe aoe mwanamke anayempenda yeye. Hayo yamepitwa na wakati. Na hata watu wengine wanaweza kumaanisha kwamba huyo mama alikuwa anamtaka mwanawe ndiyo maana anaweka vikwazo visivyokuwa na msingi.

Huyo mwana naye ana makosa kwa kufanya mipango na huyo gf wake ampige mama yake. Ijapokuwa yeye hakunyanyua mkono lakini hivyo alivyofanya ni sawa na kumpiga tu.

Wanatakiwa yeye na gf wake watafute wazee wamwombe radhi mama, na yeye mama aahidi kuwacha hiyo tabia.
 
mkongwe umesema sahihi kabisa maana hii imezidi sijui tuite ujunga au upuuzi au sijui tuwaweke wapi hawa vijana maana huwezi kumdhalilisha mzazi wako hata kama ni chizi
 
fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,828
1,660
duh,hiyo kali!kweli kuwa uyaone,me sithani kama ni sawa sana kwani mama ni mama
 
Ave Ave Maria

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,735
5,613
Kama ni mpango wa mungu wao kuoana wanaweza fika huko,unafikiri binti kakosea wapi kama alipewa ruhusa ya kumrekebisha mama mkwe bila kupewa mipaka ya njia atakazotumia?

Mambo mengine bana ni ya kujitakia, we unaenda kudeal na mpendwaji ye ana kosa gani? Kuna watu wamepinda si masihara eti! Lol! For this case, huyo binti ana haki kabisa ya kutembeza kichapo kama ambavo angetembeza kwa mtu mwingine yeyote yule hata bila ruhusa! Lakini pia unaweza ukawa na haki ya kufanya jambo fulani na bado ukajikuta unakosea kwa upande mwingine, and this happens where the right ur trying to exercise, is of negative consequences to you! Na ndicho alichokifanya huyo binti! Amemnyuka mama wa b.friend wake only for the reason that atakomesha hiyo tabia mbaya ya mama mtu pasipo kuangalia uhusiano wake wa mbele na mamamkwe utakuwaje?? Angetumia staha tu kutompiga huyo mama na badala yake kutumia nguvu nyingi kumfanya yule mama mtu amuamini hata kama si kwa siku hiyo! To me, she is so careless kwa kukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia na kuweza kuwasafishia wenzie umande unless huyo mama akubali kosa lake na aamue kusamehe!
 
wengine hufikiria kwa kutumia masaburi .... huyu dada hakuwa anaelewa anachofanya angeelewa kwamba anajifungia milango ya riziki asingekuwa na uthubutu
 
Binti Magufuli

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
7,480
5,109
wengine hufikiria kwa kutumia masaburi .... huyu dada hakuwa anaelewa anachofanya angeelewa kwamba anajifungia milango ya riziki asingekuwa na uthubutu

Yani kama mimi ndo angenipiga, haki ya Mungu huyo binti asahau ndoa......katu asingeolewa na mwanangu,ningeitisha vikao hadi vya ngazi ya taifa kuhakikisha huyo binti haingii kwenye mji wangu. Hata kama nina madhaifu hapaswi kunipiga......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom