Ni haki kwa aliyesoma shule za kata kupewa mkopo kiasi hiki?

Mr Pixel3a

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
5,053
7,263
Hebu fikiria vijana kama Hawa wengine hawana Wazazi, wamesoma shule za kata since primary na bado Ada ni 1.3milion mpaka 2.5milioni lakini bodi inampa asilimia 49 tu kwa mwaka mtoto akafie mbele, je wadau wa elimu wako wapi, viongoz wako wapi?
Screenshot_20221101-165407~2.png
 
Hebu fikiria vijana kama Hawa wengine hawana Wazazi, wamesoma shule za kata since primary na bado Ada ni 1.3milion mpaka 2.5milioni lakini bodi inampa asilimia 49 tu kwa mwaka mtoto akafie mbele, je wadau wa elimu wako wapi, viongoz wako wapi? View attachment 2404152
Nchi hii ngumu wanaoharibu lengo la kuanzishwa hii board na viongozi.
Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna mdogo wangu alikuwa anasoma shule moja inamilikiwa na waziri fulani mstaafu ambapo karo yake si chini ya milion 3 kipindi hicho.
Aliwaahidi wazazi kuwa kila mtoto anayesoma pale atapata mkopo na kweli ndivyo ilikuwa. Na kuna hata mmoja yeye hakuomba kwa sababu baba yake alimwambia hataki achukue mkopo ila akashangaa kufika chuo kapewa mkopo tena asilimia kubwa sana kitu ambacho kinaonyesha kuwa majina ya wahitimu wa pale yalishapelekwa bodi na kupita moja kwa moja.
 
Hebu fikiria vijana kama Hawa wengine hawana Wazazi, wamesoma shule za kata since primary na bado Ada ni 1.3milion mpaka 2.5milioni lakini bodi inampa asilimia 49 tu kwa mwaka mtoto akafie mbele, je wadau wa elimu wako wapi, viongoz wako wapi? View attachment 2404152
Afadhali huyu amepata nyingi, kuna kijana ni yatima amepewa ada shilingi 800,000 tu ilhali chuo anachosoma MD ada ni 5,000,000 plus, na amesoma St Kayumba kuanzia chekechea hadi kidato cha tano
 
Mimi nimesoma shule zote za serikali na sikupata licha ya kila mwaka kuomba lakini wapi, mdogo wangu ambae ni mwaka wa kwanza kwa sasa nae amesoma shule zote za kata tena kijijini huko, na amechukua mambo ya sayansi na amekosa pia. Ni hatari sana
 
Back
Top Bottom