Ni haki kuifananisha serikali ya JK na ya Hitler! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni haki kuifananisha serikali ya JK na ya Hitler!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Feb 8, 2012.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Japo sijafikia hatua ya kumfananisha Kikwete na Hitler kwa kukosa huruma dhidi ya binadamu, kama walipofikia baadhi ya watanzania kutokana na alipowafikisha watanzania, najiuliza na pengine hao wasiomtofautisha na diktena na katili huyo wa karne, nao wamejiuliza!:

  Hivi kweli Rais, wetu, Waziri mkuu wetu, Spika wa bunge na viongozi wngine wakuu wa serikali ‘na chama’ wana huruma na ndugu zao watanzania wanaoteseka kwa maradhi na kufa kwa mamia kutokana na kukosa huduma za matibabu!

  Kama walao wanayo chembe ya huruma, wanawezaje kuendelea na shughuli zao kama kawaida, huku wakitunishiana msuli na madaktari, bila kuchukua hatua za maana, huku wakitumia ujanja wa zamani wa kununua vyombo vya habari, ili kuwaaminisha watanzania kwamba huduma katika mahospitali zinaendelea na wananchi wasiwe na wasiwasi!

  Kwa nini hawataki kutumia mabilioni ya fedha tunayoambiwa na kuporwa mchana kweupe na makampuni na marafiki wa viongozi, ili kuboresha maslahi ya watumishi wa kada muhimu kama vile madaktari ili kuwafanya waendelee kuokoa maisha ya watanzania.

  Hata kama Kikwete hajamfikia Hitler kwa ukatili kama mmoja wa wachagiaji wa kipindi kinachoendeshwa na kituo cha haki za binadamu Channel ten, utoto unaofanywa na viongozi wetu, siku moja utawafikisha pabaya. na hiyo siku haiko mbali, yaweza kuwa wiki hii, mwezi huu au mwaka huu, kama hawatakubali kwamba leo siyo kama jana.
   
Loading...