Ni gazeti la Uhuru pekee ndiyo lasema Bajeti ni ya ahueni

Nimeshangazwa sana kati ya Magazeti yote ya hapa nchini yalizungumzia Bajeti ya 2016/2017 ni ngumu lakini Gazeti la UHURU pekee limesema ni Bajeti Ahueni.Nashauri tuache siasa kwenye mambo ya msingi tuache ushabiki wa kisiasa .

Gazeti la Uhuru ni la CCM hivi unafuu wa Bajeti upo kwenye nini? Bajeti nzima in kodi kodi mpaka kwenye soda Na sigara miaka yote.Wakati umefika Kwa CCM kuacha kushabikia vitu visivyo Na tija .
 
Nimeshasema mara nyingi kwamba Baba Jesca asitarajie kusifiwa tena. Sasa hivi ndiyo ukweli unabainika kwamba hana huruma na hao maskini anaowarubuni kwamba walimchagua na kamwe hatawaangusha. Yaani serikali yake imedhamiria kukusanya bila kuangalia athari ambazo zitawakumba wananchi walio wengi ambao ni maskini. Baba Jesca haaminiki tena.
 
1465447319056.jpg

Sijajua hiyo haueni ni kwa kina nani?
 
Nimeshasema mara nyingi kwamba Baba Jesca asitarajie kusifiwa tena. Sasa hivi ndiyo ukweli unabainika kwamba hana huruma na hao maskini anaowarubuni kwamba walimchagua na kamwe hatawaangusha. Yaani serikali yake imedhamiria kukusanya bila kuangalia athari ambazo zitawakumba wananchi walio wengi ambao ni maskini. Baba Jesca haaminiki tena.
Wewe ni jipu tu , nchi lazima ijitegemee , JPM anakusanya kodi lazima awakamue kila mtu afanye kazi , andamana mkumbane Na washawasha hakuna cha bure hapo ni kutumbua majipu mpk mkae level, mtachukia sana lkn mnaye miaka 20 ijayo kama hutaki jitundikeee!
 
Nimeshasema mara nyingi kwamba Baba Jesca asitarajie kusifiwa tena. Sasa hivi ndiyo ukweli unabainika kwamba hana huruma na hao maskini anaowarubuni kwamba walimchagua na kamwe hatawaangusha. Yaani serikali yake imedhamiria kukusanya bila kuangalia athari ambazo zitawakumba wananchi walio wengi ambao ni maskini. Baba Jesca haaminiki tena.
Pamoja na hayo yote ile ndoto ya kukusanya 1.3 b naona itakuwa ngumu sana kwake
 
Back
Top Bottom