Ni gazeti gani sahihi kutangaza msimamizi wa mirathi?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,516
Habari wadau,

Ukiambiwa peleka tangazo la mirathi katika gazeti? Je, gazeti la kampuni yeyote ama gazeti maalumu.

Ni gazeti gani linakubalika na mahakama?

Ama umepoteza vyeti ukaambiwa katangaze gazetini? Gazeti gani linakubalika na mahakama?
 
Linaitwa hivyo hivyo gazeti la serikali. Nenda ofisini kwa mpiga chapa wa serikali shida yako itatatuliwa hapo
 
Angalia isije kua unataka kugushi Mirathi ya Watu huko!? Kuna jela nakukumbusha tu!!
 
Government Gazzette (Gazeti la serikali)
Simaanishi Daily News/Sunday News.
 
Linaitwa hivyo hivyo gazeti la serikali. Nenda ofisini kwa mpiga chapa wa serikali shida yako itatatuliwa hapo

Gazeti la serikali ni kitu kingine kabisa tofauti na magazeti yale ya 'chama' kina Uhuru/Daily News/Mzalendo (sijui kama bado lipo)...

Huyu bwana apeleke tangazo lake pale Lumumba kama yupo Dar, ndipo mara ya mwisho nakumbuka Uhuru walikuwepo pale...

Nadhani wale watu huwa wanahitaji picha na uthibitisho wa kisheria kuonesha yeye ni mtu halali kuweza jitangaza kama msimamizi
 
Ni gazeti lolote lililopo nchini. Siyo lazima liwe la serikali.
Hii ni sahihi?

Nina matukio mawili yalihitaji gazeti na unaambiwa kabisa ni gazeti la serikali linahitajika. Tukio la mirathi na kupoteza cheti
 
Angalia isije kua unataka kugushi Mirathi ya Watu huko!? Kuna jela nakukumbusha tu!!

Mirathi huwaga inagushiwa kiurahisi?.. na je huko gazetini mtangazaji huwa anaenda tu bila kibali cha hakimu na mahakama? Ofisi gani zinaendeshwa kienyeji hivyo
 
Back
Top Bottom