#COVID19 Ni Furaha kuu, Corona kama Ugonjwa na yatokanayo yakielekea ukingoni

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,810
35,802
Leo ni siku ya furaha kuwa chanjo ya Corona inazinduliwa. Hatimaye pana Nuru tena katika maisha yetu.

Baada ya uzinduzi huu na kutupa maelekezo ya wapi kila yeyote alipo anaweza kwenda kuchanjwa kwa raha zake, tutakuwa tunaifunga rasmi sehemu kubwa ya mijadala kuhusiana na ugonjwa na yote yatokanayo. Corona itakuwa siyo issue tena.

Kipengele pekee kitakacho bakia itakuwa ni kuwajibishana kuhusiana na yaliyotusibu. Kuna watu wamekufa kwa uzembe tu. Kama tutaamua kusameheana, hilo litakuwa ni suala jingine.

Kupokelewa kwa chanjo kwa mtu kutamaanisha kuhitimishwa rasmi kwa Corona, kwake. Corona itakuwa imekuwa ni jambo lililopita na si hatari tena.

Hureee!

Wapi inapatikana Johnson Johnson nikapate jab yangu na wapendwa wangu tuufunge ukurasa huu?

Wenye dhamana, maelekezo tafadhali.
 
FB_IMG_16274482234571742.jpg
 
Hii nayo vpiii
JamiiForums-2093755274.jpg
 
Hizo label zisikupe taabu mkuu. Hata viwandani hapa kwetu, kuna vinavyozalishwa viko labeled "for export" kwa maana njema tu.

Kukurejea kwenye tashwishi yako ni kuwa:

"Label hiyo ilikuwa na maana ya kuwa dawa zilizo na ruzuku zisiishie kwa wasio hitaji ruzuku."

Dawa na vifaa tokea MSD huwa na alama ili zisiishie kwenye maduka binafsi bali katika hospitali za serikali.

Magari na products zote duniani zina soko lengwa.

Kwamba udhani kuwa label hiyo ni tatizo? Au wewe alipenda uletewe kwa label ipi ili wakuwekee hiyo?

Tatizo mvinyo? Au chupa au label ya chupa ya mvinyo huo?

Tuna nini sisi mpaka beberu atulenge kupitia chanjo hii na hii tu wala si kwenye smartphone, magari, ndege, au madawa au chanjo nyingine yoyote kutoka kwao?

Mwendazake alitupotosha sana. Acha apumzike huko huko.
 
Zombie hawana muda wa kufikiri hii kauli,Kama chanjo ni salama kwanini ujitoe kuwa responsible kwa madhara yatakayotokea?

Kwani chanjo zingine Kama polio,surua, tetanus, huwa hakuna kujaza consent form?

Tiba ipi wewe usiye zombie ambayo serikali huwajibika nayo lolote likitokea?

Jiwe hakuwajibika hata kwa tetemeko la ardhi ambalo lilikuwa ni janga. Ije kuwa umepata madhara ya dawa ukiwa na ugonjwa wako?

Tunasubiri maelekezo tunachanjwa wapi kina yakhe, tuufunge ukurasa huu wa Corona na yatokanayo.

Sana sana ibakie kwenye kuwajibishana na vifo vilivyotokana na ufyongo na porojo za awamu ile.
 
We
Tiba ipi wewe usiye zombie ambayo serikali huwajibika nayo lolote likitokea?

Jiwe hakuwajibika hata kwa tetemeko ardhi ambalo kulikuwa janga, ije kuwa umepata madhara ya dawa ukiwa na ugonjwa wako?

Tunasubiri maelekezo tunachanjwa wapi kina yakhe, tuufunge ukurasa huu wa Corona na yatokanayo.

Sana sana ibakie kwenye kuwajibishana na vifo vitokanavyo na ufyongo na porojo z
🤔🤔🤔🤔
 
Mm nimwuliza makupuku wenzangu (wenye vyeti vya utaalamu wa afya) hapa Mwannyamala hosp wakaniambia eti ni kwasabb hizo nchi zina uwezo. Na hizi dawa ni za msaada kwa nchi masikini.

Kwamba washindwe kuandika cha maana wanachotaka ili tusiweze kuona? Mbona watakuwa wajinga mno 😂😂😂 ?
 
Hizo label zisikupe taabu mkuu. Hata viwandani hapa kwetu, kuna vinavyozalishwa viko labeled "for export" kwa maana njema tu.

Kukurejea kwenye tashwishi yako ni kuwa:

"Label hiyo ilikuwa na maana ya kuwa dawa zilizo na ruzuku zisiishie kwa wasio hitaji ruzuku."

Dawa na vifaa tokea MSD huwa na alama ili zisiishie kwenye maduka binafsi bali katika hospitali za serikali.

Magari na products zote duniani zina soko lengwa.

Kwamba udhani kuwa label hiyo ni tatizo? Au wewe alipenda uletewe kwa label ipi ili wakuwekee hiyo?

Tatizo mvinyo, chupa au label ya chupa ya mvinyo?

Tuna nini sisi mpaka beberu atulenge sisi kupitia chanjo hii na hii tu wala si kwenye smartphone, magari, ndege, au madawa yoyote kutoka kwao?

Mwendazake alitupotosha sana. Acha apumzike huko huko.
Sisi tuna rasmali nyingi ambazo mabeberu wamezikalia kodo na ndizo zilizowatajirisha, beberu hapendi Afrika,yupo kwa ajili ya mali zetu na ulinzi wa vitega uchumi vyake, kwa ajili ya usalama wake,siku hizi ana mhara mchina.
 
Mkuu hapo unajaribu kuelewesha taahira la Corona. Reasoning capacity yake ni VERY LOW. Nadhani kazaliwa hivyo ndo maana nyuzi zake nyingi hazifiki mbali na alivyopunguwani hashtuki kwamba watu wameshamshtukia utaahira wake wa kuwaza Corona masaa yote.
 
Sisi tuna rasmali nyingi ambazo mabeberu wamezikalia kodo na ndizo zilizowatajirisha, beberu hapendi Afrika,yupo kwa ajili ya mali zetu na ulinzi wa vitega uchumi vyake, kwa ajili ya usalama wake,siku hizi ana mhara mchina.

Huko ni kujidanganya na kujilisha upepo jombi. Uchumi wa Afrika haufiki hata 4% ya uchumi wa dunia. Hata Africa ikifutika yote haitakuwa na impact yoyote ya kusema kwenye uchumi wa dunia.

IMG_20210728_125243_097.jpg

Ngoja tuchanjwe kwanza tuache kufa. Mama kathibitisha watu wanakufa kwa kiwango cha kutisha.

Haujawafika wanaokejeli.

Hata hivyo hiyo si issue tena. Kwetu sasa tunasubiri wapi pa kwenda kupata chanjo kwa raha zetu. Ya nani alifanya nini ikawa nini hayo baadaye.

Kwa sasa nyie bakini msichanjwe kulinda raslimali 😂😂😂😂😂!

Mzee baba baki huko huko. Kwa kweli usirudi. Tutakutana huko huko kwenye neutral ground.
 
Kama Serikali haitahusika je nani atahusika??----- serikali ndio imeleta hiyo chanjo kwa ajili ya watu wake sasa kwanini isihusike kwenye matokeo mabaya na mazuri ya hiyo chanjo??. Kwani kama hiyo chanjo itakuwa nzuri serikaki haitopata sifa???

Ni sawa na Baba alete chakula nyumbani halafu awaambie watoto kwamba mtoto anayo hiyari ya kula chakula au laa na Baba hatohusika na matokeo mabaya ya hicho chakula.🤣🤣🤣🤣

Is it conceivable ???!
 
Katika orodha ya magonjwa yote na tiba zote zilizopo ndani na nje ya Tanzania, ni tiba ipi au ugonjwa upi ambao serikali inawajibika kwa lolote ikitokea litakwenda fyongo?

Wenye maelekezo wapi chanjo zinapatikana tufahamishane jamani.

Kuipata chanjo day 1 ingependeza zaidi. -- Dr. Shika.
 
Hetero ni chanjo inayotengezwa 🇮India, asili yake ni sputnik ya Russia, sasa unategemea watu wa US, Canada, EU watatumia chanjo hiyo?
Acheni kudanganya watu

Waswahili wanasema, akutukunaye hakuchagulii tusi. Mkataa chanjo anatafuta kila sababu hata kama ni.ya kuokoteza.

IMG_20210720_094159_438.jpg

Uzuri ni kuwa umuhimu wa chanjo unaishia sasa mtu ukishachanjwa. Pana haja tena hata ya kurushiana maneno?

Asiyetaka na abakie na m@vi yake. -- mzee baba.
 
Katika orodha ya magonjwa yote na tiba zote zilizopo ndani na nje ya Tanzania, ni tiba ipi au ugonjwa upi ambao serikali inawajibika kwa lolote ikitokea litakwenda fyongo?

Wenye maelekezo wapi chanjo zinapatikana tufahamishane jamani.

Kuipata chanjo day 1 ingependeza zaidi. -- Dr. Shika.

Hapa kinachozungumziwa ni:- "CHANJO ILIYOLETWA NA SERIKALI KWA AJILI YA WATU WAKE."-----kumbuka hiyo chanjo inawezekana imeagizwa na serikali kutokana na kodi za hao wananchi.

Serikali kamwe haiwezi kukwepa Consequences za hiyo chanjo kwa wananchi, ni hivi kama chanjo itakuwa na matokeo chanya je serikali haitapongezwa???, bila shaka katika hilo itastahili pongezi kwa kutekeleza vyema wajibu wake, sasa kwanini isipokee lawama kama chanjo itakuwa na matokeo hasi???!!---- serikali
makini inatakiwa iwe makini katika uchaguzi wa vitu inavyopeleka kwa raia wake, huwezi kucheza kamari katika maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom