Ni fedhea kwa jeshi la polisi kulaghaiwa na misaada ya wafanyabiashara

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Nimesikia taarifa za Mkuu wa Mkoa wa DSM kuwaambia Askari kwamba amezungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda waweze kusaidia katika unafuu wa Bei yakiwemo mabati...kwa mtu asuyeeelewa Nini kazi ya jeshi la polisi atashangilia kama Askari hao walivyoshangilia lakini kwa anayeelewa majukumu ya jeshi la polisi atakemea kwa nguvu zote kauli kama hizi kwa sababu zifuatazo:

1.Jeshi la polisi lina jukumu la ulinzi wa nchi yetu bila kuwa na ubaguzi, je huyo anayetoa msaada au punguzo akikosea atawajibishwa na nani? Kama Leo nakupa bati kesho lazima uniheshimu na utoweza kutenda haki.

2.Uzalishaji wa viwanda unaendana na kulipa kodi kulingana na uzalishaji unaofanywa, je ni nani atakayeratibu ulipaji kodi kwa bidhaa zinazotolewa kwa bei punguzo kwa Askari?

3.Ili atoe unafuu wa bei lazima apate uthibitisho kuwa huyo anayepewa ni Askari wa jeshi la polisi, je ni sahihi kwa wamiliki wa viwanda kuwatambua Askari wetu kwa sababu tu tunataka kuwapunguzia Kodi?

4.Endapo Askari atatumia bidhaa hizo kwenda kuuza kwa raia wa kawaida kwa kutengeneza faida nani atawajibishwa na kwa sheria gani?

5.Serikali imeshindwa kuwahudumia Askari wake?

6.Huu ubaguzi ndani ya utumishi wa umma unalenga nn?

7.Je, huu utaratibu umepitishwa na taasisi nyingine wadau wa suala ili kama ofisi ya Rais na Wizara ya Fedha?

8.Nani alianzisha Jeshi la polisi la Dar es salaam badala ya jeshi la polisi la Tanzania?Bora Askari wabaki bila saruji na mabati lakini wabaki wamoja kuliko bati na vifaa vya ujenzi kuwabagua Askari wetu kwa vituo vyao.

Kwa maswali hayo na mengine ningependa kutaadharisha serikali kuepuka mpango huu kama walivyoepuka project nyingine za ulaghai wa wananchi ambazo hazitekelezeki. Tufike mahali tufanye kazi tuachane na Siasa hata katika mambo nyeti kama haya ya ulinzi wa Taifa letu.

Ni mtazamo wangu.
 
naunga mkono mkuu. mh. waziri wa mambo ya ndani awe makini sana. jeshi la polis. laweza ingia kwenye mtego. hao. wafanyabiashara wachunguzwe kwanza nyendo zao.
 
Badala amuombe mzee wake awaboreshee mazingira eti anaenda kuomba wafanyabiashara...

Hawa hawa mnaotaka waishi kama mashetani?
 
Ina maana hao wafanyabiashara hawalipi kodi au wao wana msamaha wa kulipa kodi. Mbona mkuu anahitaji vitu vya urahisi rahisi HV.Hili la container halijapoa anakoka moto mwingine; ama kweli LA kuvunda halina ubani
 
Na kwanini msaada huo uwe wa polisi wa dar peke yao? Polisi waliopo mikoani watanufaikaje na ofa hii ya wafanyabiashara wenye huruma wa dar?
Kwangu mimi kuvilaghai vyombo vya dola kwa misaada binafsi ni uhaini kwani mshawishi hana nia njema na yafaa achunguzwe kwani ipo siku atajimilikisha jeshi hilo na kuliamuru lifanye atakavyo yeye! Na haya ni matumizi mabaya ya madaraka yafaa ashtakiwe.
 
Hivi na walimu wanasafiri bure au ndio imeshindikana
Waalimu hawana input katika mkoa wa Dar es salaam kama ilivyo kwa polisi! Waalimu hawana uwezo wa kuzuia maandamo wala kuua kwa risasi inapobidi na wala hawana uwezo wa kuiba na kulinda kura!
 
Back
Top Bottom