Ni faida gani wanayopata wenye followers wengi Instagram na viewers wengi YouTube?

tommyy

Senior Member
Mar 7, 2013
178
85
Wadau naomba kuuliza maswali mawili mwenye kujua anielekeze.

1. Wale wenye followers wengi Instagram hadi wanakuwa na tick ya blue hivi wanapata hela au inakuaje, yaanikiufupi wanapata faida gani na ile tick ya blue?

2. Wasanii wakiwa wametoa nyimbo wakiiweka kwenye YouTube wakipata views wengi nao vipi wanapata faida gani kiuchumi?

Kwa anayejua anielekeze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa hizo mkuu.

Christiano anaingiza pesa ndefu punda habebi kwa kila post moja huko huko mitandaoni bro.
 
Naam!

Faida zinazopatikana kutoka kwa watumiaji wenye subscribers, views au followers wengi kupitia mitandao ya YouTube na Instagram ni kama ifuatavyo:-

• Kupitia YouTube kuna fedha au pesa anazipata muhusika mwenyewe subscribers wengi na views nyingi. Pesa hizi hutokana na matangazo yanayopitishwa na kampuni baba Google kupitia channels za wahusika wenye vigezo hivyo, hii tuitafsiri kama "Indirect Revenue". Njia nyingine tuipe tanzu "Direct Revenue" ambayo inaruhusu muhusika kupokea fedha za matangazo direct kabla ya uchakataji katika channel yake.

Kwa mfano; Millard Ayo utaweza kuona kuna matangazo ya Vodacom Tanzania, GSM na mengineyo.

• Kupitia Instagram faida zinazopatikana kutoka kwa watumiaji wenye Blue Tick (Verified) na Followers wengi moja ni kuaminiwa, baada ya kuaminiwa huanza kutengeneza fedha kutokana na mambo yafuatayo:-
- Kuuza bidhaa kupitia kurasa husika
- Kutangaza biashara za wengine kupitia kurasa husika na kuingiza fedha.

Kwa Mfano; Kupitia Instagram page ya Diamond Platnumz, Masoud Kipanya au Carry Mastory utaona wafanyabiashara, makampuni na watu binafsi wakitangaza biashara au huduma zao kupitia wao.

Faida nyingine ni uanzishaji wa Merchs hii tutaizungumzia kutokana na maswali nitakayopokea.

Shukrani Taslim
 
Instagram video ikiangalia na watu 100,000 faida Ni $ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Instagram video ikiangalia na watu 100,000 faida Ni $ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina hakika Instagram kulipa same kwa Facebook ambayo ni kampuni baba wao ni kuchukua pesa zako wewe.

Labda Facebook ni wachache sana yani 2.3% ya watumiaji wote ndio waliofanya Monetization kupitia wakala wa Video & Sound Aggregator, wengi wao wakiwa ni wanamuziki, wanafilamu na kampuni zenye mlengo wa kidigitali.
 
Back
Top Bottom