Anthony Diallo alipata nini kwa kutumia Star Tv kupotosha jamii wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015?

Hawa wanaojiita wawekezaji wazawa kama Diallo wengi ni wababaishaji tu.Hawawalipi wafanyakazi wao mishahara,hawalipi kodi serikalini na wengi wamejificha kwenye usanii wa kwamba wao ni makada wa chama ili biashara zao zisiguswe.Kila siku huyu Diallo analia eti kuhama kwenda digital kulisababisha kuyumba kiuchumi na kushindwa kulipa kodi na kuwalipa wafanyakazi.Swali la kujiuliza ni kwa nini hiyo hasara aipate yeye tu mbona media nyingine kama ITV, channel ten nao walihamia digital lkn hatusikii wakishindwa kulipa kodi?Tatizo kubwa kwa Diallo ni management.Yeye ndo mhasibu,HR,mhariri,mhandisi wa ujenzi nk kwa maana hafuati ushauri wa watu wenye taaluma aliowaajiri.Aache kulialia awaachie wataalamu waendeshe media asubiri faida.
 
Huyu jamaa ni mwanaccm kama walivyo matajiri wengi wa nchi hii , anamiliki kituo cha TV kama alivyo mwanaccm mwenzake Reginald Mengi .

Sasa cha kushangaza huyu aliamua kukiuka maadili ya utangazaji , kwa kuamua kuwanyima coverage wagombea wengine na kuwapromote wagombea wa ccm tu , na nina hakika kama tungekuwa kwenye nchi zenye kufuata sheria , vyombo vyake vya habari vingekuwa historia.

Nimebaki najiuliza hivi kwa mtu mzima kama huyu kuamua kupotosha umma kwamba ni ccm pekee inayoweza kuleta maendeleo kwa nchi hii , HUKU AKIJUA KWAMBA SIYO KWELI ( maana uko ushahidi wa wazi kwamba wameshindwa kwa karibu miaka 60 , hivyo hawataweza kwa miaka mitano ) , ALILENGA KUPATA NINI ?

Ikumbukwe kwamba kwa watu wa kanda ya ziwa kuangalia STARTV ni kama ibada , hivyo kuitumia kwa malengo ya kupotosha ni hatari sana !
Kwa akili yako ndogo uliamini Lowassa ataishinda CCM ? Kuna chama gani zaidi y'a CCM kinachofaa kuongoza Nchi. Nchi haiwezi kuwekwa rehani kwa kuwapa wahuni waingie Ikulu !! NEVER !!
 
Kama kupotosha ndio kumkampenia magu dhidi ya fisadi basi dialo anastahili kupewa nishani maalum kabisa!

Sent from my HUAWEI G510-0200 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom