Naanza kusikia watu wanaanza ama kupotosha au kuboresha matamshi na ahadi ya mtukufu rais JPM pamoja na yale yaliyoahidiwa katika ilani ya chama cha mapinduzi kwamba watatoa Elimu Bure. Hivi sasa serikali inatoa Bilioni 18 kila mwezi kwenda kutoa huduma hiyo. Kumetokea wajuzi zaidi ya JPM wameanza kutwambia kwamba kilichokusudiwa ni Elimu bila Ada wala si elimu bure, ikiwa na maana mzazi achangie baadhi ya mahitaji ya shule isipokuwa ada. Mzee Magufuli kweli hawa wamekuelewa au wanataka kukuharibia? mwenye kujua zaidi tafadhali karibu!