Ni Dotto Mtema au Regia Mtema

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,273
3,749
jamani nimesikiliza mapitio ya magazeti kupitia radio ya magic, mtangazaji amesema raisi Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Dotto Mtema chanzo gazeti la Habari Leo
 
Yeah si vibaya wakimuita Dotto Mtema,Regia ni pacha,anaye pacha wake Kulwa(Remija).....
 
VIONGOZI WA MICHEZO NA WADAU WAMUAGA MAREHEMU DOTTO MTEMANYENJE !

WAZIRI wa habari utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (mwenye miwani) aikuaga mwili wa mbunge wa Viti maalum (CHADEMA), Dotto Mtemanyenje katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Simba ambayo Alhaj Ismail Aden Rage (suti) nyeupe naye alikuwa mmoja ya walioshiriki kuaga mwili wa marehemu Dotto Mtemanyenje ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Ifakara, pembeni mwa Rage (kulia) ni aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji Mkwawa.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ya Simba, Zitto Kabwe akimkumbatia pacha wa marehemu Dotto, Kulwa Mtemanyenje katika zoezi la kuaga mwili wa pacha mwenzake Regia (DoTo)ambaye pia alikuwa mwanachama wa Wekundu wa Msimbazi, Simba.

Ujumbe huo !

Mbunge wa Mbeya mjini (CHADEMA) ambaye pia ni msanii wa hip hop nchini, Joseph Mbilinyi 'Mr.11' naye pia alikuwemo.
MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI,
 
Lala salama kamanda Regia (Doto)
 
Ni kawaida Tanzania mapacha kuitwa Doto(Dotto ni mbwembwe tu hakuna double t!) na Kurwa ingawa wanakuwa na majina yao ya kawaida.
 
Doto na kulwa kila mahali wana jinsi yao ya kuwatambulisha,ukienda congo kinshasa hapo wanaitwa OMBA na SHAKO,Kwa wenzetu waarabu wakiwa wanaume huitwa Hussein na Hassan!
 
Miss you sister!
Msaada jamani kuna eneo nilipakana na marehemu, ingawa aliandika jina Remija au alimnunulia pacha wake 2011 nafikiri sasa muda umepita mjumbe ameona linakuwa pori analeta watu kuliuza. Please mwenye contact au jinsi ya kuwasiliana na nduguze aniwekee hapa naona sio vizuri kuona haki yake inapotea hivi hivi. Asanteni
 
Aisee umenikumbusha mbali sana..katika wabunge wa viti maalumu ambao kweli walikuwa makamanda basi huyu dada, wengine waliobaki ni mizigo tu kwa chama Mungu amrehemu huko aliko.Amina
NADHANI WALIOKUWA WANAMFAHAMU WATAKUJA.
 
Miss you sister!
Msaada jamani kuna eneo nilipakana na marehemu, ingawa aliandika jina Remija au alimnunulia pacha wake 2011 nafikiri sasa muda umepita mjumbe ameona linakuwa pori analeta watu kuliuza. Please mwenye contact au jinsi ya kuwasiliana na nduguze aniwekee hapa naona sio vizuri kuona haki yake inapotea hivi hivi. Asanteni

Good mama Joe,

Jitahidi wewe mwenyewe, nenda pale Kinondoni ofisi za CDM, waambie habari hii ili wao wakuunganishe na ndugu zake waliopo pale Tabata Chang`ombe. Njia hii inaweza kuepusha manyang`au walijitokeze. Au pata simu ya Mbunge Halima Mdee, naamini anaweza kusaidia hili jambo.

Ubarikiwe na Bwana Yesu wa Nazareti.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom