Usedcountrynewpipo
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,636
- 2,725
Umuhimu wa wanadiplomasia ulianza kuonekana mara baada ya kumalizika vita kuu ya pili ya dunia. Gharama ya kupigana vita ilionekana kuwa ni gharama kubwa sana kuliko gharama ya kuwahudumia wana diplomasia ambao walionekana kama chombo kikuu cha kufikia makubaliano katika migongano mbali mbali ya kimaslahi bila kumwaga damu.
Ndio maana mpaka leo popote duniani wanadiplomasia hawalipi kodi za aina mbali mbali ikiwemo VAT.
Pia ndio maana wanadiplomasia wana passport ambazo hazihitaji kugongwa viza ili kuwarahisishia kusafiri kwenda sehemu yeyote kwa urahisi duniani.
Sasa sitaki kuamini kama kweli waziri Mpango hajui umuhimu wa wana diplomasia kiasi cha kuthubutu kuwakata kodi. Nadhani ni kwa vile hajawahi kuona taifa likiingia kwenye machafuko ndio maana haoni umuhimu wa wana diplomasia. Ngoja tu nimkumbushe kidogo.
Miaka iliyopita wananchi wa Mtwara walidai gesi yao na vuguvugu la kujitenga lilianza. Wana diplomaisa walifanikiwa kuzima mzozo huo na kuliunganisha taifa.
Miaka iliyopita wana Kigoma walianzisha vugu vugu la kujitenga wakiadai hawanufaiki na kuwa Tanzania. Wana diplomasia walifanikiwa kuzima vugu vugu hilo na nchi ikawa moja.
In abscence ya wanadiplomasia ingebidi nguvu ya kijeshi itumike kuzima mavugu vugu hayo na ingekuwa ni gharama kubwa sana.
Kwa mifano hii michache ninamuomba Mh Mpango, kuachana na mpango wake wa kuwatoza kodi wabunge na wanadiplomasia wengine...
Hawa ni watu wa muhimu kwa amani na umoja wa taifa na Dunia kwa ujumla.