Ni dhahiri kuwa Taasisi za kifedha za kimataifa zinataka kufanya kazi na Rais Magufuli, zimempigia kampeni bila kificho

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,899
World Bank wameikopesha Tanzania mabillioni ya shilingi na wao furaha yao ni kuona wanalipwa hela zao kama zilivyo Taasisi zingine za fedha ambazo zingependa wateja walipaji wazuri, imeelezwa kuwa tangu Rais Magufuli aingie ameonyesha nidhamu ya hali ya juu sana kwenye ulipaji wa madeni ya Tanzania kwenye Taasisi za kifedha.

Wazungu pia pamoja na mambo mengine wameona Magufuli ni mkweli na mwenye misimamo isiyoyumba kitendo cha kuitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati kimevuruga Sera za upinzani zilizobainisha kuwa JPM anaharibu uchumi.

Wapinzani wanaweza wakafikiri kuwa kuisimanga Tanzania kwa mambo mazuri inayoyafanya kwa ajili ya watu wake ndio kutawafanya waingie Ikulu, hapana wajitafakari sana Mzungu ana urafiki wa masilahi na si vinginevyo hii ya Bank ya Dunia imewavua nguo wapinzani na wazodoaji wa JPM wanaoshinda kutwa mitandaoni kubeza juhudi za Serikali.
 
Nawaonea raha watakao tangaza nia kwa ticket ya CCM safari hii watapeta sana nyota wanayosafiria inang'aa mno.
 
Mabeberu wampigie magoti jpm? Ungeacha kupaka upepo rangi bro. Hakuna kitu kama hiyo. + mkopo nchi ndio ina request, si bank inatoa hovyo hovyo.
 
ilani_ccm_2015.jpg
 
Kesho wakitoa taarifa za umasikini kuongezeka mtasema ni mabeberu!!

Alafu hizi taarifa za ukuaji wa uchumi haziuziki kwa wananchi wa nchi hii maana hata mishahara tu mmeshindwa kuongeza huku madeni ya humu ndani(ya watumishi,n.k) hamlipi ila mnalipa madeni ya mabeberu.

Kumbuka hata wastaafu mafao wanasotea,mifuko mmeiunganisha baada ya kukopa na kulipa kwa kusuasua.

Ni watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri tu ndio wataridhika na huu utawala.
 
Si

Sisi si masikini tena
 
Ni vile nyie hamuanalyse. Ila kusema ukweli Magufuli kashusha uchumi. Kufikia hiyo lower middle income ni Asante kwa JK alitutoa GNI$ 500 mpaka GNI $720 kwa muhula wake wa kwanza. Sasa JPM katutoa $980 mpaka GNI 1,080 maximum. Halafu mnamsifia mfyuûuuuuuuuu.
 
Sasa kwann miaka 10 ya kikwete tusingie uchumi wa Kati? Jamaa kapigi only five yrs kafika kwny lengo.
 
Ni vile nyie hamuanalyse. Ila kusema ukweli Magufuli kashusha uchumi. Kufikia hiyo lower middle income ni Asante kwa JK alitutoa GNI$ 500 mpaka GNI $720 kwa muhula wake wa kwanza. Sasa JPM katutoa $980 mpaka GNI 1,080 maximum. Halafu mnamsifia mfyuûuuuuuuuu.
Tupe na GDP growth. Maana hii ipo highly affected na population growth.
 
Back
Top Bottom