Ni dawa gani ya usingizi wanayoitumia wezi kupuliza madirishani?

Salaam jf.

Nilikuwa naomba uzoefu wenu wana jf, hasa katika hizi dawa wa wanazotumia wezi kuwaibia raia wema kuwapulizia madirishani wakati wa usiku wanapolala, kwanza nilikuwa nataka kufahamu jina lake na pili wapi wanapozipata lengo si kwa ajiri ya matumizi binafsi lengo ni kufahamu. Sababu wizi wa kuvunjiwa milango na madirisha umekithiri kibaya zaidi wezi wanathubutu kuwaibia walala hoi hadi maafisa wa serikali wenye silaha, juzi kati mh. Fulani ambaye anacheo kikubwa tu serikalini alipigwa vitu vyake vyote sebureni na mwengine kasafishwa sebure yote na watoto wa mjini, akiwemo pia mwanajeshi mstaafu nae alivunjiwa nyumba na wezi kusafisha sebure lakini kabla ya kuiba wezi walikunywa chai iliyokuwa sebureni na kuondoka. Inavyooshesha hii dawa inawapa kiburi sana, usishangae hadi usalama huwa wanapigwa.

Nasikia kuweka maji kwenye ndoo au beseni yana-neutralize hiyo dawa kwani inavutwa sana na maji!
 
Hiyo dawa haifai wadau wezi wanafika wanavuta viti wanakaa wanaorodhesha vitu vya kuiba na bei ya kuuzia
Nacheka kama mazuri vile.ila daah kweli wahuni sio watu.hivi haya matukio yanatokea mitaa gani.mbona pande hizi sijawahi kusikia wizi wa dizaini hyo
Mkuu, wezi hula makombo,hupakua wali uliolala maarufu kiporo, hula daku nk. Kiufupi ni washenzi sana. Tena hadi kukojoa mkojo kwenye vyombo, kwa ufupi hawana utu
 
Tehe tehe tehe hayo majamaa yaliyokunywa mpaka chai ni 'noma', ukweli lazima tuyapongeze kwa umafia walioufanya kwa sababu huwezi kwenda kwenye nyumba ya mtu kuiba halafu ukanywa mpaka chai ni 'noma'.

Nakumbuka wakati naishi Kunduchi, jirani yetu mmoja alikuwa mfugaji wa bata. Alikuwa na bata wengi kama utitiri. Kumbe basi wazee wa kazi siku nyingi walikuwa wanawamezea mate wale bata.

Siku ya siku wazee wa kazi wakatia 'maguu', nafikiri walitumia hiyo dawa ya usingizi kwa maana siku hiyo usingizi ulikuwa mtamu balaa! Wazee wa kazi kama kawaida yao, wakachukua bata wote hawakuacha hata manyoa...watu tunaamka asubuhi tunakuta banda leupe, dah siku hiyo nilicheka sana kwa sauti ya chini chini kwa sababu wazee wa kazi walikuja na 'kiroliroli'... tuliona tu alama za matairi ya gari, yani wazee wa kazi kwa jeuri walikuja mpaka na gari, ule mngurumo wa gari watu hatukusikia tunakoroma tu, ha ha haa ni 'noma!'
 
Ch
Sasa kama wanatumia hiyo dawa, nini kifanyike ili kuondoa usingizi?
Ikizidi waweza kulala hadi kufa?
Nini zuio?
Chloroform inatabia ya kuwa affirnity to water. Hivyo unapolala hakikisha ndoo ya maji unayo chumani tena iwe wazi na maji mengi. Wakikupulizia hiyo dawa basi moja kwa moja inavutwa kwenda kwenye maji.
Kamwe haitakuathiri, watashangaa tu wakigusa mlango mzee umekurupuka na kulianzisha varangati nao
 
Hao dawa yao IPO, wakiiba mbona watarudisha tena wakilia, dawa ya wezi ni kuwaroga tu Mimi huwa siendi police, iba uone
Dmkali acha utapeli wako huo,wadanganye hao hao wajinga wenzako.Huo utapeli haujaanza Leo sijawahi kuona ujinga huo popote.Mamia kwa maelfu ya kesi za wizi zimejazana mahakamani na mitaani kote nchini kwa nini usiende kufunga kazi uzimalize zote na wewe uwe bilionea kwa kulipwa kwa kazi nzuri uliofanya.
 
Back
Top Bottom