Ni Dar-es-Salaam or Dar -El-Salaam?

Mtoto wa Kishua

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
834
151
Nakumbuka nilipo kua primary school ,tulikua tunaandika mji wa Dar kama Dar-EL-Salaam , ila na shangaa baadae inakuja kuandikwa Dar-es-Salaam ipi ni sahihi wadau ?
 
Sijawahi kuona dar es salaam ikiandikwa dar el salaam.
Lakini dar el salaam ndio halisi maana neno el ni neno la kiarabu, na hao ndio waliolipa jiji hili jina hilo na tukajitupa mkono jina asilia mzizima.
 
Sawa, ila nakumbuka nikiwa shule miaka ya 80's ,tulikua tunaandika Dar-El-Salaam , nadhani ndio sahihi , hii Dar-Es-Salaam imekuja baada ya wengi kushindwa kupronounce "L" na ndipo ikabadilika.
 
Ni kweli Bujibuji hawakutaka jina lionekane la kiarabu ndio maana ikaondolewa El na kuwekwa Es na hii ilianza kabla ya miaka ya 80.
 
Sawa, ila nakumbuka nikiwa shule miaka ya 80's ,tulikua tunaandika Dar-El-Salaam , nadhani ndio sahihi , hii Dar-Es-Salaam imekuja baada ya wengi kushindwa kupronounce "L" na ndipo ikabadilika.

Neno Dar-El-Salaam ni neno la Kiarabu maana yake ni nyumba ya Amani yaani Dar (nyumba) -El- (yenye) Salaam (Amani) Au kiswahili kingine Mahali penye Amani (Utulivu) na hivyo neno Dar-El-Salaam , kwa kiswahili ni Dar-Es-Salaam kwa hiyo tofauti yake ni hii El haipo hapo lakini maana yake bado ipo hapo hapo nyumba yenye amani. Au mahali Penye Amani Dar-Es-Salaam jina lake la zamani ilikuwa inaitwa Mzizima.
 
Lugha yoyote huwa ina kua na vitu vidogo hubadilika. Pia kama neno likiazimwa kutoka lugha nyingine lazima itakua modified kufit kwenye adopte language yake.
 
Nakumbuka nilipo kua primary school ,tulikua tunaandika mji wa Dar kama Dar-EL-Salaam , ila na shangaa baadae inakuja kuandikwa Dar-es-Salaam ipi ni sahihi wadau ?

Jina Dar es Salaam linatokana na neno la kiarabu: دار السلام‎ (Maana yake: "nyumba ya salama au Amani" Dāru al-Salām).

Tanzania na Brunei wanatmia jina la Dar es Salaam ila Brunei wao ni jina la nchi, wanaandika hivi State of Brunei Darussalam au the Nation of Brunei, the Abode of Peace (Negara Brunei Darussalam)

Mzizima maana yake Mji ulio changamka (unao zizima kwa harakati zake) ila wazungu(Waingereza wao waliandika: "healthy town").
 
Sasa kwanini waondoe mzizima," healthy town", kulikuwa na nini? nafikiri turejee huko Mzizma kwani sasa hivi si nyumba ya amani bali ni "nyumba ya mafisadi".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom