Ni dalili ya utapeli au ndo mwelekeo wa kupata ajira mpya?

Panctuality

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
726
1,044
Habarini wanajukwaa,hapo awali niliweka thread yenye kuonesha nia ya kubadili kituo cha kazi kwa fani hii hii ya uhasibu kwakuwa mahala nilipo mkataba unakaribia kuisha,kuna bwana mmoja humu jukwaani alini pm na kuhitaji contacts zangu, katika mazungumzo ya simu aliniunganisha na meneja wa GDM kiwanda cha kahawa Mlowo kama alivyodai na meneja huyo alidai kuwa accountant position iko wazi na kunitaka ni apply via email with required attachment

Sasa leo nimepokea email yao muda huu kunitaka nifike kesho tarehe 28 September for Interview but kutokana na geographical location kwa masaa bakia ngumu kufika huko mahala husika,nilipojaribu kuwapa taarifa kuwa Ni ngumu kufika ndipo serekasi nyingi zikaanzia hapa kwamba niweke mazingira ama nijiongeze ili ibaki tu kuitwa kuanza kazi bila hata ya kusailiwa.

Nimekwepa mishale mingi ya matepeli na nazifahamu zaidi ya mbinu zao 50.

Katika hili naona kama Ni mbinu ya 51 ushauri,maoni,onyo na tahadhari juu ya hili,nijitupie mtegoni ama laa,na mwenye mawasiliano halisi ya wafanyakazi ngazi za juu kiwandani hapo anisaidie ili Ni prove the case no 51ya mwaka 2021 juu ya makosa ya kimtandao.

Wanataka kunipiga ama veeep wakuu.
 
Back
Top Bottom