Ni dalili gani za awali za kujua kuwa Mtoto wako uliyemzaa ni hasara kwa Taifa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
Naomba msaada wa ' dalili ' za kuweza kujua kuwa Mtoto aliyezaliwa hatokuja kuwa na faida kwa Taifa / Nchi nikimaanisha kuwa ni ' hasara ' tupu.

Nimeleta kwenu hili swali baada ya kila siku kujionea hawa Watoto wetu tunaowazaa sasa ni ' bogus ' kabisa kiasi kwamba kuna muda unafika hata unamkufuru Mungu kwa kusema ni Kheri Mkeo angekuzalia Mbuzi labda akikua ungemchinja na kumla kuliko kuzaa ' Toto ' ambalo halina faida.

Kwa wale ambao 24/7 huwa mnakuwa ni Watu wa Jamii mnaweza mkanielewa ninachojaribu kusema hapa na kwa mwendo huu ninaouona na jinsi kila siku tunavyozidi ' Kufyatua ' tu Watoto miaka 30 hadi 50 ijayo hawa Watoto wetu wanaweza kuiuza Tanzania kwa bei ya hasara kama wao walivyo hasara kwa Familia / Taifa / Nchi.

Nikipewa hizo ' dalili ' nitashukuru sana ili wenye hao Watoto tuanze ' kujiongeza ' kukabiliana na hizo ' hasara '.

Akhsanteni na naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom