Ni course gani nzuri kwa mtoto aliyehitimu kidato cha nne?

Underdog

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
334
434
Sabal-al-khair wanajukwaa,

Nina mwanangu anatarajia kuhitimu kidato cha nne mwezi wa November mwaka huu kama itampendeza M/Mungu. Miaka ya nyuma ilikuwa ni desturi kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne kwenda kusomea Computer wakati akisubiri matokeo ila kwa sasa naona mambo yamebadilika.

Naombeni mnishauri ni course gani fupi nimpeleke huyu mwanangu wa kike wakati akisubiri matokeo maana huwa wanatumia muda mrefu sana kusubiri matokeo na nahofia akikaa nyumbani wanaweza wakamtia mimba.

Natanguliza shukrani
 
Mpelekee computer hyo hyo bdaa ya matokeoo Pre form five ..sidhnii kama kuna kngne cha kusomea zaidii ya ivoo
 
Mbona wasiwasi mwingi juu ya mimba? Mtoto kasoma vizuri mpaka kumaliza form 4 hana chembe ya mimba. Kwa nini uanze kumhofia sasa?Aendelee kusaidia shughuli za hapo nyumbani na kozi nzuri sana kwake ni wewe na mama yake kumkalisha kikao na kumfundisha mbinu za maisha bora ya uadilifu. Kwenye kozi za kompyuta virusi havikosekani shehe!
 
Tusubiri wenye elimu wamalize kupanga baada ya kuivuruga elimu.Maana sasa elimu haijulikani ni nini hasa.
 
Mbona wasiwasi mwingi juu ya mimba? Mtoto kasoma vizuri mpaka kumaliza form 4 hana chembe ya mimba. Kwa nini uanze kumhofia sasa?Aendelee kusaidia shughuli za hapo nyumbani na kozi nzuri sana kwake ni wewe na mama yake kumkalisha kikao na kumfundisha mbinu za maisha bora ya uadilifu. Kwenye kozi za kompyuta virusi havikosekani shehe!
Hilo la kupata mimba nimetia tu kama chachandu mkuu, ila nilitaka kumuongezea maarifa tu sababu yupo interest na account ila sijajua nini cha kufanya ili nimsaidie
 
Back
Top Bottom