Ni computer (system) gani inayochukua siku nne kufanya mabadiliko? Kwanini waziri mwenye dhamana asiwajibishwe?

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,088
Kuna watu wanaleta utetezi kua mitandao ambaayo haijabadilisha vifurishi ni kutokana na suala la programing, pia kwenye gazete wanasema inaeeza kuchukua siku zaidi ya nne, mpaka leo hii bado mitandao hiyo haijabadilisha vifurushi.

1. Je, ni kweli wataalamu wa serikali wanaamini kua system inachukua siku nne kubadilika? Huu ni uongo

2. Ni nani yuko nyumaa ya hiki? Serikali inafaidika na kuendelea kwa bei hii ambayo imeshasema zitolewe? Na kama haifaidiki ni kwamba hii mitandao ya simu imedharau agizo la serikali la kubadilisha bei na kudanganya kua mfumo unachelewa?

Kwanini viongozi wako kimya? Hata wabunge wetu hawasemi kitu?

Kuna mambo yana lazimisha sana kuondoa imani na serikali hasa pale unapoona viongozi hawajali hali za wananchi. Ndugulile asaidiwe
 
Zantel, TTCL mbona zimerudisha mapema tu, hao Vodacom, Airtel, Tigo, na Halotel wanajitia ukiziwi subiri uone kitakachowakuta kwa wateja wao.
 
Wajinga hawa wanatuona mazwazwa. Wanapima muelekeo kote kote. Kujua muitikio wa watu pande zote. Yaani huku kwa siku zote (Zantel na TTCL) na huku kupya (Tigo, Voda, na Halotel)
 
Wajinga hawa wanatuona mazwazwa. Wanapima muelekeo kote kote. Kujua muitikio wa watu pande zote. Yaani huku kwa siku zote (Zantel na TTCL) na huku kupya (Tigo, Voda, na Halotel)
Shida wadau wanasema ttcl network inasumbua
 
Hawa jamaa wanatusikilizia malalamiko yapungue. Yakipungua hawatabadirisha.
 
Toka nje ya hiyo temeke... Nenda kisarawe huko, au mkuranga na hiyo ttcl.. ndio utaelewa tunachomaanisha
Hehehehe nikafanye nn kisarawe,, mbn ttcl inafanya kazi vizuri tu nimeitumia ifunda huko na bado mambo ni byee
 
Back
Top Bottom