Ni chuki binafsi, majungu, uroho wa madarka, jk usiogope utashinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni chuki binafsi, majungu, uroho wa madarka, jk usiogope utashinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 7, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Siku moja nilisikia Rijamaa Rimoja Rinasema , "VITA NI VITA MURA", sikujua huyu jamaa alikuwa na maana gani?. Kumbe vita ya maneno ndiyo mbaya kuliko hata ile ya kushika SILAHA. Nadhani hii inatokana na ukweli kwamba, kabla ya vita ya kushika mtutu ni lazima ianze ile ya maneno ambayo madhara yake ni makubwa.

  Ni vita hii ya maneno mengi yakiwa ya uongo kutoka vyama vya upinzani na nyingine ndani ya CCM wenyewe ndiyo inasababisha watanzania wengine tudanganyike na kuamini eti Serikali ya JK haifanya kitu na hakuna jambo la msingi la kufanya vita hii iwepo bali tu RAIS wangu JK awe ndiye wa kulaumiwa na lengo haliishii hapo bali eti mwisho wake na wengine wapate kuingia IKULU baada ya kushinda vita hii ya maneno.

  Kuna nini jipya katika vita ya maneno inayoendeshwa na makundi ndani ya CCM kama siyo chuki inayotokana na baadhi ya watu hao kukosa nafasi walizoaidiwa huku wengine wakiwa na hasira ya kupoteza nafasi zao baada ya kuonekana wazi hawakujiandaa kwa moyo wa dhati kuwatumika watanzania bali matumbo yao. Tujiulize swali hapa, hivi kweli wote wangeweza kupata kazi kwa ujumla wao? aidha kwa wale waliopoteza nafasi zao wanataka kutuambia kwamba walionewa au ni chuki ya kunyang'anywa tonge mdomoni? na kama walionewa si waseme wazi sisi tulionewa na ukweli ni huu.
  Nikija upande wa UPINZANI una macho mawili lakini umefunga jicho moja lillokuwa linaona mazuri yaliyofanywa na RAIS wangu KIKWETE na kubakiza jicho lile ambalo si kwamba linaloona mabaya tu bali linadiriki hata kukonyeza watanzania kuwa kataeni kufanya kazi zinazoelekezwa na Serikali ya JK. Yapo mambo mengi ambayo yamesemwa na wapinzani kuhusu Serikali na bila hatua tunazoshauriwa na wapinzani hawa kuchukua ni kuandamana, kugoma, kukataa kushiriki shuguli za maendeleo, kukataa kutii kuheshimu sheria na taratibu za nchi, kuwazomea viongozi kila wanapopita na pale wanapokuwa na wananchi kutekeleza majukumu yao. Je ndilo suluhisho? ama ni njama za kutaka tupoteze muda bila kufanya kazi ili lawama zizidi kumwendea Rais wangu?

  Sitaki kusema sana kuhusu hili la wapinzani kwa vile najua wao malipo yao yapo. Masema malipo yao yapo kwa vile tayari wameshatufundishwa kuwa Rais hatakiwi kusafiri, kazi ya kuwaletea maendeleo ni ya Serikali na siyo wananchi wenyewe, migomo ni haki ya kila mtu, maandamano ni haki bila kujali ni halali au la. Wameshatufundisha kuwa ni marufuku kuheshimu sheria za nchi na zaidi wameshatufundishwa kuwa kuwazomea/kuwakashfu/kuwadhihaki viongozi ndiyo demokrasia ya kweli. Hivyo basi watakapoingia madarakani wakatugeuka kutekeleza hayo bazi itabidi wakabiane na nguvu zaidi.


  JK PAMBANA VITA NI VITA TU, TUNAKUAMINI.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hata sijasoma li-thread lako....kinyaa!!
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mnamwamini wewe na nani?
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  content za hii thread nilishawahi kuziona kwenye post fulani hivi juzi kati.

  vipi ilikosa mvuto nini?

  na leo nimeishia kusoma maneno manne ya aya ya kwanza.

  pole sana.

  JK anatetewa na wale jamaa wa Kameruni tu.
   
 5. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hunatofouti na Gaddafi na Mtoto wake wakidai watawamaliza wapizani wao ilhali nchi inaanguka. Pole sana ndugu.
   
 6. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,672
  Likes Received: 2,207
  Trophy Points: 280
  jamaa hata akili za kuangalizia huna ? Kikwete kashindwa kudhibiti A town tu unamsfia? Nimesema mara nying juwa ukiwa mshabiki wa ccm yakubidi uwe chizi au uwe mwizi ili wasiingie wengine ukaishisa jela bila hata kuisumbua mahakama
   
Loading...