Ni changamoto gani unaweza kukutana nayo kwa mara ya kwanza unavyotambulishwa ukweni?

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Kwa wale ambao wameshapitia hii hatua tayari na wana uzoefu hebu tupeane experience ni changamoto gani unaweza kukutana nayo siku utakapokwenda ukweni kutambulishwa.

Na jinsi gani unaweza kuiepuka hii changamoto ili usije ukaonekana kituko?

Pia soma:
 
Usiogope kuonekana kituko, mimi nilienda kama kumsindikiza msibani mara paa wazee wakaitwa na wanataka hela ya vinyo na mfukoni sina hata mkwanja. Ikabidi jamaa mmoja mkwilima anikopeshe
 
Usiogope kuonekana kituko, mimi nilienda kama kumsindikiza msibani mara paa wazee wakaitwa na wanataka hela ya vinyo na mfukoni sina hata mkwanja. Ikabidi jamaa mmoja mkwilima anikopeshe
Uliingilia pazuri sana. Unaonekana mwenye upendo na kujali kumbe umeenda kusoma upepo. Ukija kujitambilsha wakwe wanakuwa marafiki wa kawaida na unacheza na akili zao.

Mziki ni pale hujawahi fika, huwafahamu sura wala tabia zao. Ndo umeenda kujitambulisha. Halafu ukute wakorofi. Weeee!
 
Unayetaka kwenda kumposa ndio atakupa picha kamili ya huko uendako. Ongea naye vizuri.
 
Ni ngumu kufahamu Ni changamoto aina Gani utakutana navyo ila jambo la umuhimu siku hiyo ni muonekano wako na uongeaji wako pesa yako mfukoni ndio utatoa picha kamili ww ni mtu wa aina Gani maana kuna unaweza fika ukweni siku ya kwanza ukaambiwa umeme umeisha Shemeji unaweza kutususaidia chochote kile hapo wanakupima
 
Wajue unaoenda kwao ni watu wa aina gani. Kuna wengine ni watu wa mitungi sana, wengine walokole. Makabila mengine kama sisi Wamasai ukija lazima angalau paliwe nyama n.k

Fanya kautafiti na mtu anaeweza kukupa picha kamili ni huyo mwenza wako.
 
Inategemea inawezekana usikumbane na changamoto ya aina yoyote ila cha muhimu ni kujiweka smati na Pochi itune japo kidogo.
 
Uliingilia pazuri sana. Unaonekana mwenye upendo na kujali kumbe umeenda kusoma upepo. Ukija kujitambilsha wakwe wanakuwa marafiki wa kawaida na unacheza na akili zao.

Mziki ni pale hujawahi fika, huwafahamu sura wala tabia zao. Ndo umeenda kujitambulisha. Halafu ukute wakorofi. Weeee!

Baada ya hapo kilifata mahari wazeee hawakutaka kuchelewesha. Maswali yakaanza umeishi nae kwa muda gani? Yaani wale wazeee ni balaaa.
 
Mi kamwe sitojali wataniona vipi infact nashangaa sana wanaume wanaogopa kwenda ukweni

Kumbuka we ndo muoaji ndio kiongozi ukikataliwa kidume hukosi wa kuoa tofauti kidogo na mwanamke yaani kidume kuchukiwa ukweni hata haitusumbui tofauti na mwanamke

Sasa mzee gani.atamkataa.mkwe binti yake asiolewe na binti.gani atakubali.iwe hivyo kwanza huwa wanaulizwaga pindi wakitoa taarifa ya ujio wako "mwanangu umempenda huyu" na hata mahali ukiambiwa kubwa huwezi itoa we mwambie mchumba wako lazima wazee walegeze kamba
 
Back
Top Bottom