Ni changamoto gani unaipata kwa fundi wako wa nguo?

Zoe Closet TZ

New Member
Jun 1, 2021
2
1
Salam kwenu wapendwa.

Karibu sana kwenye page yetu ya Zoe Closet Tz, kwa kweli hili swali huwa najiuliza mara zote na sijawahi pata jibu, mafundi wa nguo shida inakuwaga nini?

Ofisi yetu inadeal na nguo za kike za kushona na za kawaida, na tunaelewa kushona nguo ni kazi yenye challenge kama kazi zingine, shida inakuja why lazima kuwe na uswahili uswahili?

Ni wanaenjoy au wanakuwa na stress zao za maisha ambazo binadam wote tumeumbiwa jamani. Na tabia zao huwa zinafanana fanana mara zote yani kama wanaambiana vile.

Kufanya story iwe fupi, kuna fundi wetu mmoja, ni fundi mwenye kazi nzuri, yani akikushonea nguo yako unasema mambo ndo haya, hana uchafu finishing nzuri tu.

Kazi inavutia, na anakuwaga na mood nzuri sana mda wa kupokea nguo yani, nikaja gundua hata hiyo mood si sababu nguo zinakuwa nyingi kuwa kapata kazi, no, anakuwa anashangalia advance unayompa kwa mda huo.

Sasa acha kazi yako hapo, mmekubaliana ndani ya siku 5 kazi inakuwa tayari, ..weee, hizo 5 mlizokubaliana lazima aongeze na zake 5, msumbuane weee, yani anashindwa elewa tukimpa kazi, na sisi tunakuwa tumepewa kazi jamani, yani unakuwa umeshahaidi wateja wako, inakwaza mnoooo, inaharibu trust pia, atleast mtu akiona alikuhaidi ndani ya siku 5 kazi unaipata alafu kiubinadam labda kapata kazi zingine au kasahau kushona kiustaarabu si unamtafuta mtu unasema?

Nimechelewa kushona, naomba ongezewa siku kadhaa, ili nami nimpange wangu. Sisi ni binadamu tunaelewana jamani, lakini hapana atakaa hizo siku 5, zinakuwa 7 unajiongeza labda ngoja week iishage tu, ntazipata hata jumatatu, wapii, kuna mda unamsusia unasema wacha akae nazo akimaliza atapiga, lakini wakumbuka ni nguo za wateja na ndo kazi yako, unapiga tena, hahaa na ukipiga ni mkali jamani, yani kama wewe ndo umemchelewesha. Na wewe unakuwa na hasira zako hapo

Sasa hapo azimalize, mkutane ukute kasoro umwambie, maana hapo nakuwa na hasira za kunichelewesha plus unakuta nguo ilitakiwa kuwa ndefu kapunguza vipimo imekuwa fupi, maana anakuwa ameshasahau maelezo mengine. Alafu wao ndo wawe sensitive, yaani anakuwa kafura hatari, insecurities za nini? I mean si ni maongezi tu fundi.

So naomba msaada wa kujua shida inakuwaga ipo wapi? Ukiacha wateja na sisi huwa tuna mambo yetu mengi lakini hapana, mafundi wetu wanaongoza jamani.

Tunaomba kujua,fundi wako ni wa aina gani? Sensitive,mkali, mstaarabu,ananuna tu,mswahili(uongo) tusaidiane hii stress please😂
Karibuni wakuu.
 
Back
Top Bottom