Ni chakula, tunda au kinywaji gani unaona kipo overrated/underrated?

Kwa upande wangu,

Underrated


Makande: Nimekuwa nikiona watu wakiyadharau sana makande eti kwamba ni chakula cha ajabu ila kwa mimi naona makande hayapewi heshima inayostahili. Jamii zote za makande kama; makande njugu, makande maharage zina mabalaa yake. Halafu itokee siku hiyo likachanganuwa na nyama na pak choi (Chainizi) kwa pembeni. Acheni wakuu, makande matamu bwana.

Zambarau:
Huwa najisikia vibaya sana pale haya matunda yanapokuwa hayapewi thamani yake. Ni nadra sana kukuta sehemu panauzwa zambarau. Yaani huwa nikipita njiani naona mazambarau yamedondoka tu na watu hawana hata time nayo huwa najiuliza kwani haya matunda yaliwakosea nini wadau. Haya matunda yametukuza, yametutoa mbali sana.
Zambarau uliweke kwa kipoozeo liwe la bariiidi, aah, acheni aisee!

Overrated

Pizza:
Hiiiiii, haya mavitu sijui hata watu wanayapendea nini! Kuna siku nikaamua kujitoa kimasomaso nikanunua pizza bwana ili nami niliburudishe tumbo kimamtoni, aisee. Nilijutia sana hela yangu.

Mafenesi: Kwanza sijui ndo jina lake hilo! Madude flani matunda yake makuubwa yana mavipelevipele, vile vinyama flani vya ndani ndo vinaliwa. Haya matunda ni maarufu sana Dar, utayakuta wauzaji wameyaweka pembeni mwa barabara. Kuna siku nami nikaamua kuyajaribu, aisee ile harufu tu ilinishinda. Buku langu likawa limeenda bure maana nikipofika gheto nikayatupa kwenye mfuko wa taka.

Ma-apple: Haya madude yanaishi kistaa sana hapa mjini maana bei ya apple moja unanunua sahani ya wali. Haya madude yananitesa maana kuna kadada nisipokanunulia basi lazima itokee vita ya majimaji. Ila ladha yake ni sawa na mapeasi tu. Yaani kiufupi ma-apple ni mapeasi yaliyochangamka. Figure tu ndo inayapa kiki hapa mjini vinginevyo yanyekuwa yanauzwa fungu mia kama mapera.

Vipi kwa upande wako?
Underated
Ugali dagaa
Chai viazi vitamu
Chai mihogo

Overated
Chipsi mayai
Wali kuku
 
Sheikh umezoea masamaki yalioungwa ma kutiwa udambu udambu mwingi. Sangara , sato, hongwe, mbofu, mbete, ngere, furu acha kabisaaa wachemshwe iwekwe limao na chumvi tuuu wale samaki wana mafuta yake. Kula na ugali wa mahindi mixa wa muhogo. Aseee ukikojoa bao hadi unaisikiamo na anaekojolewa ilo bao atakwambia mbona leo za moto ivooo
Comments kama hivi ndo huwa zinasababisha mfumuko wa bei. Ukitaja mamno ya mabao mabao watu wanatengeneza fursa chap...😂
 
Underated
Ugali dagaa
Chai viazi vitamu
Chai mihogo

Overated
Chipsi mayai
Wali kuku
Maoni yangu 😂😂

Viati vitamu wala haviwi underrated, hivyo vinafaa kuwa underground hivyo hivyo. Huwezi kufananisha na mihogo kabisa.

Chipsi mayai...dah, hiyo kitu ukiigonga halafu ukapata na mirinda nyeusi barrriiiid. Wacha wadada wapate mimba kisa chipsi yai aisee, ni tamu.😂

Kwingine naunga mkono hoja.

Au nasema uongo ndugu zangu? 😂
 
Hili dude hili, aloooo.
Walikuwa wameweka kwenye vibebeo vya plastic, nilikula kama vinyama viwili tu, yakanishinda.
Sema fenesi Sio dude
20210615_160021.jpg
20210615_154915.jpg
 
Bora nipambane na makande au mdojolela, ila pizza sijui birian hapan kwa kweli siwezi.
 
Back
Top Bottom