Ni chakula, tunda au kinywaji gani unaona kipo overrated/underrated?

Nikija kumjua aliyegundua hii combination nitamjengea kasanamu kadogodogo kuenzi mchango wake.
Hii kitu inakaa popote kuanzia; breakfast, lunch, supper, dinner.....
Ikilala, ukaamka nayo asubuhi halafu ipige mixer... 😀

Siku nikiona nataka kukata roho nitaomba hiyo kitu kwanza ndiyo nikalale kwa amani.
 
8yrs mishe zangu ni lake zone,ila nilivyokua nasikia story za utamu wa hawa samaki(nikiwa Dsm,home) naona tofauti na uhalisia,kwa minofu kweli wamejaza ila kwa taste binafsi hapana
Sheikh umezoea masamaki yalioungwa ma kutiwa udambu udambu mwingi. Sangara , sato, hongwe, mbofu, mbete, ngere, furu acha kabisaaa wachemshwe iwekwe limao na chumvi tuuu wale samaki wana mafuta yake. Kula na ugali wa mahindi mixa wa muhogo. Aseee ukikojoa bao hadi unaisikiamo na anaekojolewa ilo bao atakwambia mbona leo za moto ivooo
 
Sheikh umezoea masamaki yalioungwa ma kutiwa udambu udambu mwingi. Sangara , sato, hongwe, mbofu, mbete, ngere, furu acha kabisaaa wachemshwe iwekwe limao na chumvi tuuu wale samaki wana mafuta yake. Kula na ugali wa mahindi mixa wa muhogo. Aseee ukikojoa bao hadi unaisikiamo na anaekojolewa ilo bao atakwambia mbona leo za moto ivooo
Sheikh bao tena,haya bwana
 
Mleta mada ulikula pizza gani, au vile vidude wazenji wa forodhani waita pizza?

Githeri/Makande ni namna ya upishi tu na aina ya makande yenyewe (kuna ya mahindi mabichi, makavu na makavu yaliyokobolewa)...

Kwa sisi wapenda misosi, huwa hakuna msosi over or underrated labda uwe umechacha...

Ukitaka uenjoy wali ndondo basi kuna ule wali ndondo uliolala kwenye jokofu, au ulilala kwenye chungu halafu ile morning unaugonga na chai ya maziwa...

Kula mboga za majani zozote zile sijui mchunga, majani ya kunde, majani ya maharage, sukuma, kabichi (ukitaka uinjoi imiksiwe na nyama), kisamvu (hili dude kula kiporo chake na wali nazi)...

Nafasi hata haitoshi hapa...
 
Kwa upande wangu,

Underrated

Makande: Nimekuwa nikiona watu wakiyadharau sana makande eti kwamba ni chakula cha ajabu ila kwa mimi naona makande hayapewi heshima inayostahili. Jamii zote za makande kama; makande njugu, makande maharage zina mabalaa yake. Halafu itokee siku hiyo likachanganuwa na nyama na pak choi (Chainizi) kwa pembeni. Acheni wakuu, makande matamu bwana.

Zambarau: Huwa najisikia vibaya sana pale haya matunda yanapokuwa hayapewi thamani yake. Ni nadra sana kukuta sehemu panauzwa zambarau. Yaani huwa nikipita njiani naona mazambarau yamedondoka tu na watu hawana hata time nayo huwa najiuliza kwani haya matunda yaliwakosea nini wadau. Haya matunda yametukuza, yametutoa mbali sana.
Zambarau uliweke kwa kipoozeo liwe la bariiidi, aah, acheni aisee!

Overrated

Pizza:
Hiiiiii, haya mavitu sijui hata watu wanayapendea nini! Kuna siku nikaamua kujitoa kimasomaso nikanunua pizza bwana ili nami niliburudishe tumbo kimamtoni, aisee. Nilijutia sana hela yangu.

Mafenesi: Kwanza sijui ndo jina lake hilo! Madude flani matunda yake makuubwa yana mavipelevipele, vile vinyama flani vya ndani ndo vinaliwa. Haya matunda ni maarufu sana Dar, utayakuta wauzaji wameyaweka pembeni mwa barabara. Kuna siku nami nikaamua kuyajaribu, aisee ile harufu tu ilinishinda. Buku langu likawa limeenda bure maana nikipofika gheto nikayatupa kwenye mfuko wa taka.

Ma-apple: Haya madude yanaishi kistaa sana hapa mjini maana bei ya apple moja unanunua sahani ya wali. Haya madude yananitesa maana kuna kadada nisipokanunulia basi lazima itokee vita ya majimaji. Ila ladha yake ni sawa na mapeasi tu. Yaani kiufupi ma-apple ni mapeasi yaliyochangamka. Figure tu ndo inayapa kiki hapa mjini vinginevyo yanyekuwa yanauzwa fungu mia kama mapera.

Vipi kwa upande wako?
😂🤣🤣 Apple 🍎🍏 eti yanaishi kistaa
 
Underrated
Kiporo cha wali maharage


images.jpg
 
Back
Top Bottom