ni busara kuhamia kwa mwanamke?

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,889
3,412
Wakuu
mnakumbuka week iliyopita nilileta mada hapa jamvini inahusu kupendana na mwanamke msomi,wote mliochangia nilisoma na kuelewa comment zena na nashukuru sana kwa sababu kuna mambo mengi nilijifunza
uhusiano wangu na yule mwanamke umeendelea kukua siku baada ya siku,nilikuwa sijui kumbe yule mwanamke anatoka familiya ya kitajiri sana halafu ana nyumba nzuri sana na ya kifahari sehemu maarufu
mimi nina kajibanda kangu mahali uswahilini lakini hapendi kuishi pale,anataka nihamie kwake eti ile nyumba ya kwake itakuwa ya kwangu,nimejaribu kuongea na baadhi ya ndugu zangu ambao nawaamini wameniambia sio vizuri mwanaume kuhamia kwa mwanamke kwani nawadhalilisha ukoo wangu manake nakuwa kama nimeolewa na yule mwanamke
mwingine alisema nitakuwa sina say yaani kila kitu ni ndio mama
Jf ni jukwaa la magreat thinker naomba ushauri wakuu
 
Hongera kumbe ni mtunzi mzuri sana ongea na rizwani akakuombee page moja kwenye magazeti pendwa uendeleze kipaji chako!!!
 
He he he he "USITHUBUTU"

Tena narudia "USITHUBUTU" Speaking from experience......naishia hapo siendelei
 
hii topic imeshajadiliwa kwa marefu hapa MMU, use the search function utaiona
 
Nyumba yake itakuwaje ya kwako tena?

mwambie kama kweli amekupa akuruhusu uiuze then hela utakayopata ukajenge sehemu nyingine ndo muendelee kuishi hapo itakuwa kweli alipanga kukupa
 
Kwa sisi wanawake tulivyo mhhh
acha nijisemee nafsi yangu nahitaj nyumba niishi tuliyojenga yote au uliyojenga
thats how men should be ila ukihamia kwangu sijui nitakuonea at first itakuwa sawa ila baadae mhhh
sasa cha msingi we pangisha nyumba yako na yeye apangishe nyumba yake kisha tafuteni nyumba mpange kama mtashare kodi itakuwa vizuri sana
ni hayo ila kuhamia kwake mhhh+amekuzidi kiuchumi si vizuri jamani
 
He he he he "USITHUBUTU"

Tena narudia "USITHUBUTU" Speaking from experience......naishia hapo siendelei

nimejikuta nimecheka
vipi ulilazwa chini nini?au ulifukuzwa night kali?
Mzima?
 
nimejikuta nimecheka
vipi ulilazwa chini nini?au ulifukuzwa night kali?
Mzima?

Hapana, mimi nakushauri kwa moyo mmoja hamia, kutoka hapo mtafanya mambo pamoja, lakini kwa kuwa hamjaoana ndio maana kila mtu anakukataza lakini mkihalalisha hakuna tena ya kufukuzana...
 
Usithubutu kufanya hivyo hata siku moja kwani uwezekano wa kuwa mateka wa kimapenzi ni mkubwa sana.

Kama inawezekana hamieni pamoja kwenye nyumba mpya. Vinginevyo kila mtu abaki tu na kwake.
 
sioni tatizo kama itakuwa kwa muda mfupi afu ujipange uwe na kwako mkakae pamoja....italeta heshima zaidi kama mtaishi kwako na si kwake.. si unajua kama si yeye basi nduguze au ndugu zako waweza kuwa kisiki..
 
Kaka ukiona wewe unapendwa ujue kuna mjina katendwa huko..so take care bro..!!hao watu wanauwezo wa kusahau dakika moja na kukufukuza kama siyo wewe uliyekuwa unakula nae goodtime..!!
 
We hamia tuu kama hujashikishwa ukuta inawezekana kuna mwanaume kamjengea akija kukukuta ukuta utakuwa rafki yako wa karibu sana.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakuu
mnakumbuka week iliyopita nilileta mada hapa jamvini inahusu kupendana na mwanamke msomi,wote mliochangia nilisoma na kuelewa comment zena na nashukuru sana kwa sababu kuna mambo mengi nilijifunza
uhusiano wangu na yule mwanamke umeendelea kukua siku baada ya siku,nilikuwa sijui kumbe yule mwanamke anatoka familiya ya kitajiri sana halafu ana nyumba nzuri sana na ya kifahari sehemu maarufu
mimi nina kajibanda kangu mahali uswahilini lakini hapendi kuishi pale,anataka nihamie kwake eti ile nyumba ya kwake itakuwa ya kwangu,nimejaribu kuongea na baadhi ya ndugu zangu ambao nawaamini wameniambia sio vizuri mwanaume kuhamia kwa mwanamke kwani nawadhalilisha ukoo wangu manake nakuwa kama nimeolewa na yule mwanamke
mwingine alisema nitakuwa sina say yaani kila kitu ni ndio mama
Jf ni jukwaa la magreat thinker naomba ushauri wakuu

wee hawa wanawake unawajua unawasikia?? utapewa matusi wewe mpaka ushangae na roho yako. tulizana usioe kwa sababu msomi na ana nyumba nziri....ukishakiwa nae utaona vyakawaida tuu. tuliza isine jiaibisha bure kidume. kama dozi mpige huko huko uswaz.
 
sio busara kuhamia kwa mwanamke mm kama mwanamke na kushauri kama uyo mwanamke anakupenda ahamie kwako cz kam mtu anakupenda hawezi kujali sehemu unapoishi eti ni uswazi sidhani kam ukimpenda mtu kwa nzati utawza ivyo huyo anapenda uhamie kwake akupeleke peleke na ivyo kakuzidi elimu usikubali kaka
 
Achana na mawazo yakutafuta short cut. Maisha ni kujihangaisha, utapata vya jasho lako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom