Ni bora kupitia hali ngumu ukiwa mikononi mwa Mungu

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
133
500
Habari zenu wadau,

Ngoja niwape story ya ndugu yangu mmoja hivi, ni binadam yangu ambae tulikua tumeshibana sana katika maisha ni mpambanaji wa kufa yaani jamaa alikua ni mtafutaj mno mno.

Alitoka kijijini akawa anaishi kwetu baadae akajipanga akaenda kujitegemea wilaya nyingine kwa jinsi tulivokua marafiki alitafutia kiwanja karibu na kwake nikanunua nikawa najipanga kujenga.

Siku moja nilimtembelea wakati ananisindikiza kuludi home akaniambia kuna mzee ana muonea wivu maendeleo yake ivo anataka kumuua.

Nikamuuliza kwanini akasema ndani ya mwez mmoja amepara ajari tatu ana usafiri wa pikipiki kwa ajili ya shuguli zake.

Nikamuuliza tena umejuaje km ni huyo mzee akasema alivopata ajar ya mwisho alienda kwa mganga akaambiwa ni huyo mzee anamtafta.

Pia akaniambia amepewa dawa na amechanjwa chale zitakazomlinda kwa nafsi yangu mimi na waganga ni vitu viwili tofauti.

Lakini sijui ni kwanini nilishindwa kumpa ushauri ambao ni tofaut ingawa moyo wangu ulinisukuma kumu eleza kwamba msaada wa mwanadam una mwisho.

Nikaludi home nikawa na mfadhaiko sana ila nikapanga nitakwenda siku nyingine nitakaa kaa nae nimpe ushauri aachane na waganga atafute msaada kwa mungu kupitia makanisa etc.

Kabla siku niliopanga kufika jamaa alipata ajar na kufa hapo hapo. Niliumiaa sana ingawa boda zinaua lakin kwa mazingira ya kijijini ambako hakuna lami wala magar meng ni nadra sana.

Jamaa kaenda ki mas hara sana aisee sasa nachojiuliza mwisho wake ulikuaje na wapi alipo ni bora kutegemea mungu hata km njia ya mungu ni ndefu.
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
5,983
2,000
Ujue maisha ni mchezo. Alivyokueleza ni kweli, ungemsaidia kwa kumtafutia kalumanzila wa uhakika. Wanaokuambia kimbilia kanisani ni waongo , wamebeba bonge la hirizi kiunoni au la kumeza kwa kuogopa aibu.
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,451
2,000
Ujue maisha ni mchezo. Alivyokueleza ni kweli, ungemsaidia kwa kumtafutia kalumanzila wa uhakika. Wanaokuambia kimbilia kanisani ni waongo , wamebeba bonge la hirizi kiunoni au la kumeza kwa kuogopa aibu.
Nakupinga mkuu Mungu yupo na anatenda ikiacha tu ego you can feel his presence naongea kwa uzoefu wa changamoto nilizopitia recently ningekua sina imani probably ningekua mwanga saivi
 

jojoe35

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
218
250
Katika hatari kubwa utakayojingiza Ni kufikiri changamoto unazopata zinaletwa na mwanadamu mwenzako.

Hapo umekwishaaaaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom